Naomba kujuzwa kwanini marehemu anaombewa?

Naomba kujuzwa kwanini marehemu anaombewa?

Mimi nakupa mtazamo ktk uislam
KUMUOMBEA MAITI
1_mungu wetu ambaye ni ALLAH ni mwenye huruma sana anaweza kubadili hatima ya maiti kutokana na amuombaye yukoje mbele zake

2_ ile ya kumuombea ina onyesha huruma mlionayo kwe mwenzenu basi ALLAH ambaye ni mwabudiwa wetu huwahurumi nyinyi na kusamehe makosa mlio wahi kuyafanya
 
Lazaro alipofariki hakwenda yeye kwa yesu ili afufuliwe bali ni walio hai walimwombea kwa Mungu na Mungu ili mwenye huruma alimfufua. Halikadhalika wafu hawana uwezo tena wa kuomba ila kama sisi tulio hai tutawaombea kwa Mungu, Mungu atawafufua na kuwaondolea azabu ya kaburi. Katika biblia hakuna sehemu yesu alimfufua mtu pasi na maombi toka kwa wafiwa. Wafiwa waliomba kwa yesu naye aliwasikiliza vilio vyao na kuwafufua wapendwa wao.
 
Hivi mtu una uhakika gani kuwa matendo mema uliyoyafanya yanatosha na kufanya kuwa ni lazima wewe uingie peponi?
 
Kwanza niseme mimi ni deist kwa sasa(imani yangu bado inakua)

Nina uelewa kiasi flani kuhusu uislam na misingi yake, lakini pia nina ufahamu mkubwa wa ukiristo, ukiachia mbali ndio mfumo wa imani niliokulia, lakini pia ndio mfumo wa maisha ninaouishi.

kuna utaratibu wa watu kupeleka ndugu zao waliokufa katika nyumba za ibada kuwaombea kabla hawajazika.

Naomba kujua mantiki (logic) ya hicho kitendo. imani inazungumzia walio hai na inawataka wao wakiwa hai waamini.

Kama maombi kwa marehemu yanaweza au yanabadili hatima yake, kuna haja gani mtu kuamini akiwa hai wakati hata akifanya mabaya bado siku akifa ataombewa na atasamehewa na huyo Mungu?

naomba kujua kwa imani yako umuhimu wa maombi kwa marhemu.

Natanguliza shukrani.
kila dhambi unayotenda lazima ulipe malipizi yake hapa duniani. ukifa hujakamilisha malipizi una umeshatubu kwa Mungu, basi utapata adhabu ya muda huko kuitwako TOHARANI. sala zetu tulio duniani zinawasaidia marehemu kufupisha muda wa kukaa TOHARANI. kumbe ni sawa kuwaombea marehemu; rejea 2 Wamakabayo 12:43-46. asante anza sasa kuwaombea ndugu zako wote.
 
Lazaro alipofariki hakwenda yeye kwa yesu ili afufuliwe bali ni walio hai walimwombea kwa Mungu na Mungu ili mwenye huruma alimfufua. Halikadhalika wafu hawana uwezo tena wa kuomba ila kama sisi tulio hai tutawaombea kwa Mungu, Mungu atawafufua na kuwaondolea azabu ya kaburi. Katika biblia hakuna sehemu yesu alimfufua mtu pasi na maombi toka kwa wafiwa. Wafiwa waliomba kwa yesu naye aliwasikiliza vilio vyao na kuwafufua wapendwa wao.
Lakini Biblia inaonyesha wote walioomba waliomba wafu wao wafufuliwe si kupunguziwa adhabu au kusamehewa dhambi.

Kwa nini kipindi hiki tusiombe kufufuliwa wapendwa wetu badala yake tunakesha machana na usiku kuomba wapunguziwe adhabu??
 
kila dhambi unayotenda lazima ulipe malipizi yake hapa duniani. ukifa hujakamilisha malipizi una umeshatubu kwa Mungu, basi utapata adhabu ya muda huko kuitwako TOHARANI. sala zetu tulio duniani zinawasaidia marehemu kufupisha muda wa kukaa TOHARANI. kumbe ni sawa kuwaombea marehemu; rejea 2 Wamakabayo 12:43-46. asante anza sasa kuwaombea ndugu zako wote.
Hakuna kitu kinachoitwa toharani mkuu.

Ni mafundisho ya kipagani tu yaliyopenyezwa ndani ya kanisa.

Roho ya mpinga Kristo ilianza kufanya kazi kipindi kirefu, hata wakati wa mitume kama kina Paulo ilikuwa imeshaanza, ndio iliyopachika haya mafundisho ya utawala wa Kirumi ndani ya Ukristo.
 
We unashangaa kuombewa maiti, mbona kuna wengine wanomba hizo maiti ziwasaidie? Utasikia 'flan flani' utuombeee!
 
Kwanza niseme mimi ni deist kwa sasa(imani yangu bado inakua)

Nina uelewa kiasi flani kuhusu uislam na misingi yake, lakini pia nina ufahamu mkubwa wa ukiristo, ukiachia mbali ndio mfumo wa imani niliokulia, lakini pia ndio mfumo wa maisha ninaouishi.

kuna utaratibu wa watu kupeleka ndugu zao waliokufa katika nyumba za ibada kuwaombea kabla hawajazika.

Naomba kujua mantiki (logic) ya hicho kitendo. imani inazungumzia walio hai na inawataka wao wakiwa hai waamini.

Kama maombi kwa marehemu yanaweza au yanabadili hatima yake, kuna haja gani mtu kuamini akiwa hai wakati hata akifanya mabaya bado siku akifa ataombewa na atasamehewa na huyo Mungu?

naomba kujua kwa imani yako umuhimu wa maombi kwa marhemu.

Natanguliza shukrani.
Mkuu swali lako zuri na majibu yake yapo hapa

Naomba usome ukiwa umetuliza kichwa na fikra afu utoe mang'amzi.

2 Timotheo 1:16-18

16 Bwana aihurumie jamaa ya Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha rohoni mara nyingi, wala hakuona haya kwa kuwa nilikuwa kifungoni, 17 ila mara tu alipofika Roma, alianza kunitafuta kwa bidii mpaka akanipata. 18 Bwana amjalie huruma katika Siku ile! Nawe wajua vizuri mengi aliyonifanyia huko Efeso.

Soma tena na tena hadi uelewe

Kwa ufupi
Paulo anamwandikia Timotheo hii barua ila pia anaambatanisha na maombi mawili makubwa

1. Maombi ya rehema kwa familia ya Onesiforo(verse ya 16) na anamwelezea jinsi gan huyu Onesiforo alivokua mwema kwake huko rumi na efeso na anamwambia Timotheo kuwa ww ni shahidi wa wema huo.

2. Maombi ya rehema kwa Onesiforo na kuwa Mungu amjalie huruma katka siku ile(maana ake siku ya hukumu)

swali ni kwamba hapa Onesiforo yupo wapi? Mbona inaonekana kama hayupo na familia yake? afu kwann aombewe huruma siku ile ya hukumu tofauti na maombi ya familia yake.

Nikisema kuwa hapa Onesiforo alikua marehemu ntakua nimekosea? Jibu ni HAPANA

shida ni kuwa watu husoma Biblia sana ila huwa hatufanyi reasoning, hatutafakari vema.

Ila pia unaweza peleka hyo verse kwa mchungaji wako naye aitafakari.

cc
 
Ibada inapaswa kuwa ya kumshukuru Mungu kwa maisha ya huyo mtu hapa duniani na kuifariji familia huku ikitukumbusha tuluobakia jukumu letu la kumtumikia Mungu

Kumuomba Mungu amsamehe marehemu huo ni wendawazimu. Ukristo unasema wazi kutubu ukiwa hai, ukishakufa hakuna namna yoyote ya kupunguza adhabu ya Mungu kwako

Makanisa hasa RC (ambalo mimi naabudu) sijui wanatoa wapi huu utaratibu wa kuwaombea marehemu ndani ya vitabu vya Mungu
Wewe ndo mpumbavu hujui unachokiandika.halafu wewe si Mkatoliki maana hatuna Wakatoliki Matutusa wasioijua Biblia umeamua kujifanya mkatoliki.Acha na sisi wewe.Mnatusema sana lkn Mwisho wa siku kitaeleweka tu Mjinga ni nani na Mwerevu ni nani??.
 
Hakuna kitu kinachoitwa toharani mkuu.

Ni mafundisho ya kipagani tu yaliyopenyezwa ndani ya kanisa.

Roho ya mpinga Kristo ilianza kufanya kazi kipindi kirefu, hata wakati wa mitume kama kina Paulo ilikuwa imeshaanza, ndio iliyopachika haya mafundisho ya utawala wa Kirumi ndani ya Ukristo.

Kaka ni swala la muda tu utakuja kuelewa maandiko na misingi sahihi ya Ukristo,
Hao wakatoliki ndio waliokuwa na hiyo Biblia unayotamba nayo sasa, wao wangeamua wangeweza kufanya chochote na kuharibu hayo maandiko, lakini hawakufanya hivyo, ila waliotoka ndani ya Ukatoliki ndio wakaanza kutoa baadhi ya vitabu, ukae ukijua katika vitabu alivyovipunguza Martin Luther hata Kitabu cha Jakobo na Ufunuo alivitoa na kisha kuvirudisha baadae

Hoja yangu ni kuwa, Wakatoliki huwa hawakurupuki na huwa wanaitafsiri Biblia kwa kina kirefu ambacho madhehebu mengine inawachukua miaka kuiona hiyo kweli

Ulokole ulipoanza hasa hapa Tanzania, walikuwa na Biblia tu lakini siku zimeenda na wameanza kurudi kwenye Ukatoliki kwa mlango wa nyuma, Ilikuwa si rahisi kwa Mlokole kumkuta na Mafuta, Maji, Nguo na vitu vingine vikiwa kama silaha ya maombezi, kwa Ukatoliki ni vitu vya kawaida kwa walokole haikuwa kawaida

Wakatoliki wanaamini Yesu ni Mungu, kama Aliombwa kufanya vitu fulani na akavifanya inakuwaje sasa akiombwa asiweze kufanya?
 
Kwenye Ukristo wa Kiprotestant hakuna maana yoyote ya kumuombea mtu akiwa amefariki maana Biblia inakataza kabisa ibada za wafu.

Ila ibada ile ya siku ya msiba ni kwa ajili ya kuwafariji tu na kuwakumbusha wanadamu umuhimu wa kumkumbuka Mungu kabla ya umauti ndio maana huwa yanasisitiswa mahubiri zaidi kuliko sala.

Ibada ile siku ya msiba ni muhimu kwa sababu kubwa kwamba ni kipindi kigumu sana kwa wafiwa kuondokewa na mtu wa karibu(kama umeshawahi kufiwa utalijua hili) na jamii ya kiroho inabidi iwe karibu sana na wafiwa.

Jambo jingine nafikiri ni busara tu ya viongozi wa kidini kuzuia mabalaa yanayoambatana na misiba, kwa maana misiba hutumiwa sana na washirikina kufanya mambo yao mazito kwa waliobaki, lakini pia kupenyeza imani zao za kishirkikina.

Ibada ya Kimungu isipofanyika hupelekea watu waliofiwa kugeukia upande mwingine wa kishetani kufanya matambiko na matambiko ya misibani huwa yana nguvu sana kufunga hata vizazi vinne alivyoviacha marehemu.

Binafsi naunga mkono ibada hizi siku za misiba, japo si katika kuwaombea waliokufa wasamehewe dhambi au kupunguziwa adhabu, ila kwa ajili ya kuwalinda hawa waliobaki kiroho, maana zisipofanyika shetani ata-take advantage na matambiko lazima yatafanyika tu.

And the thread is closed
 
Huwezi kupata jibu sahihi humu, hakuna member wa jf aliyewahi kufa na kurudi tena humu kuthibitisha hilo. Wote wanaochangia ni mbwembwe za wachungaji na kutetea imani zao.
sikuuliza kupata uzoefu wa kifo, nimeuliza kujua kwa nini marehemu hua wanaenda kuombewa. uwe unasoma unaelewa kabla hujakurupuka kuchangia
 
Kwenye Ukristo wa Kiprotestant hakuna maana yoyote ya kumuombea mtu akiwa amefariki maana Biblia inakataza kabisa ibada za wafu.

Ila ibada ile ya siku ya msiba ni kwa ajili ya kuwafariji tu na kuwakumbusha wanadamu umuhimu wa kumkumbuka Mungu kabla ya umauti ndio maana huwa yanasisitiswa mahubiri zaidi kuliko sala.

Ibada ile siku ya msiba ni muhimu kwa sababu kubwa kwamba ni kipindi kigumu sana kwa wafiwa kuondokewa na mtu wa karibu(kama umeshawahi kufiwa utalijua hili) na jamii ya kiroho inabidi iwe karibu sana na wafiwa.

Jambo jingine nafikiri ni busara tu ya viongozi wa kidini kuzuia mabalaa yanayoambatana na misiba, kwa maana misiba hutumiwa sana na washirikina kufanya mambo yao mazito kwa waliobaki, lakini pia kupenyeza imani zao za kishirkikina.

Ibada ya Kimungu isipofanyika hupelekea watu waliofiwa kugeukia upande mwingine wa kishetani kufanya matambiko na matambiko ya misibani huwa yana nguvu sana kufunga hata vizazi vinne alivyoviacha marehemu.

Binafsi naunga mkono ibada hizi siku za misiba, japo si katika kuwaombea waliokufa wasamehewe dhambi au kupunguziwa adhabu, ila kwa ajili ya kuwalinda hawa waliobaki kiroho, maana zisipofanyika shetani ata-take advantage na matambiko lazima yatafanyika tu.
Heshima kwako mkuu.
 
Hakuna logic yoyote ni Umizimu tu hasa unaoendekezwa na kanisa katoliki
Wewe akili yako itakuwa na matatizo! Inamaana katika dini zote umeona wakatoliki ndio wanaofanya ibaada wakati wa msiba? Hebu tumia busara katika kujadili mambo, usijadili kwa mihemko
 
Roma Catholic ndo wanaamini mtu akiombewa basi atafutiwa dhambi zake. Huwa sielewagi mafundishi yao kabisaa
 
Ni kuwafariji wafiwa ila hamna lolote pale.Ule mwili ni kama boksi la simu unapoitoa simu yako na kubakiwa na boksi tupu na kwenda kulitupa.Ukifa umekufa lile ni kasha tu au boksi.Wakati mwingine inasaidia watu kwenda kwenye ibada ili waombewe.
Nani kakudanganya...Labda ile Biblia ya vitabu 66 ya Martin Luther
 
Back
Top Bottom