Naomba kujuzwa kwanini marehemu anaombewa?

Naomba kujuzwa kwanini marehemu anaombewa?

Ukiona unashiriki au unaongoza kuombea marehemu basi ww bila shaka ni mpumbav maana kama marehemu wangekuwa wana ombewa basi ni wazi shetani angebaki peke yake Jehanamu
Kwanini unazuia huruma ya Mungu...Huruma ya Mungu haina mipaka...
 
sikuuliza kupata uzoefu wa kifo, nimeuliza kujua kwa nini marehemu hua wanaenda kuombewa. uwe unasoma unaelewa kabla hujakurupuka kuchangia

Mkuu tatizo wewe mwenyewe mtata, unasema hauamini ukristo wala uislam wakati unataka kujadili jambo linalowahusu hao watu.

Kwa upande wa protestant, marehem/maiti haombewi...ile ni ibada ya mazishi kama ilivyo ndoa n.k
Hiyo imani ya mtu akitolewa mochwari unayoipendekeza imeegemea kwenye upande au falsafa ipi?
 
Ibada inapaswa kuwa ya kumshukuru Mungu kwa maisha ya huyo mtu hapa duniani na kuifariji familia huku ikitukumbusha tuluobakia jukumu letu la kumtumikia Mungu
Ni sawa kabisa...

Kumuomba Mungu amsamehe marehemu huo ni wendawazimu.
Kwanini unafikiri ni uendawazimu....? Hivi ni nani wa kuzuia huruma ya Mungu kwa watu wake? Yesu anasema Yeye aniaminiye mimi hatokufa bali ataishi Milele....Yohana 11:25
Hakuna ambaye hatendi dhambi... Hata uwe Mkristo vipi lazima kuna kuanguka..ndio maana kuna toba na Rehema...Je! Yule aliyepata ajali ya ghafla na kufariki ila alimwamini Kristo japokuwa alikuwa na mapungu, unafikiri huyu atenda jehanam....Hapa ndio umuhimu wa kyziombea Riho hizi ili zipate Rehema kwa Mungu....

Ukristo unasema wazi kutubu ukiwa hai, ukishakufa hakuna namna yoyote ya kupunguza adhabu ya Mungu kwako
Sio kweli...Soma kitabu cha Wamakabayo uone jinsi sala za walio hai zinavyo wasaidia roho za marehemu..

Makanisa hasa RC (ambalo mimi naabudu)
Hapana wewe si Catholic...Hakuna Mkatoliki ambaye hajui umuhimu wa kuombea Roho za Marehemu ili zipate rehema kwa Mungu..
sijui wanatoa wapi huu utaratibu wa kuwaombea marehemu ndani ya vitabu vya Mungu
Umesha sema vitabu vya Mungu...Kumbe unajua utaratibu wote upo kwenye vitabu vya Mungu ehh...

Yap! Utaratibu huo upo wazi kwenye Biblia
 
Lazaro alipofariki hakwenda yeye kwa yesu ili afufuliwe bali ni walio hai walimwombea kwa Mungu na Mungu ili mwenye huruma alimfufua. Halikadhalika wafu hawana uwezo tena wa kuomba ila kama sisi tulio hai tutawaombea kwa Mungu, Mungu atawafufua na kuwaondolea azabu ya kaburi. Katika biblia hakuna sehemu yesu alimfufua mtu pasi na maombi toka kwa wafiwa. Wafiwa waliomba kwa yesu naye aliwasikiliza vilio vyao na kuwafufua wapendwa wao.
Nashangaa watu wanataka kuzuia huruma ya Mungu....
 
Inavyo takiwa ajiombee mwenyewe alipo kua hai kufanya mambo mema ya ibada kwenda kufanya ibada kama hakufanya yeye mwenyewe hana haja kufanyiwe ila tuna fan ya ili watu wajue umuhimu wake kwani kama hujafanya mwenyewe hata uombewe vipi ni bure
 
Wewe ndo ******** hujui unachokiandika.halafu wewe si Mkatoliki maana hatuna Wakatoliki Matutusa wasioijua Biblia umeamua kujifanya mkatoliki.Acha na sisi wewe.Mnatusema sana lkn Mwisho wa siku kitaeleweka tu Mjinga ni nani na Mwerevu ni nani??.
Mkuu nipe maandiko matakatifu kuthibitiaha utetezi wako. Makanisa yetu yanapopotoka, waumini tuna haki ya kuhoji

Nina mengi tu ya kulihoji kanisa langu Katoliki kama ni halali ktk maandiko. Ibada ya kuabudu ufundi idols ijumaa kuu huku ikiwa imekatazwa wazi ktk amri ya pili ya Mungu ni jambo la kushangaza. Kuabudu mkate na Divai tunavunja wazi amri ya pili

Nahitaji kufundishwa sana, la sivyo ni halali kusema kwamba kanisa langu liko nje ya misingi ya ukristo

Haya ni maoni yangu binafsi mkuu. Niko tayari kukosolewa kwa maandiko ya biblia takatifu
 
kila dhambi unayotenda lazima ulipe malipizi yake hapa duniani. ukifa hujakamilisha malipizi una umeshatubu kwa Mungu, basi utapata adhabu ya muda huko kuitwako TOHARANI. sala zetu tulio duniani zinawasaidia marehemu kufupisha muda wa kukaa TOHARANI. kumbe ni sawa kuwaombea marehemu; rejea 2 Wamakabayo 12:43-46. asante anza sasa kuwaombea ndugu zako wote.
Unajua mkuu baadhi ya Wakristo wana Biblia ile pungufu ambayo Martin Luther alipunguza baadhi ya Vitabu...Haya mambo hawayajui...Tuendelee kuwaelimisha
 
Lakini wakristo wao mchungaji huwafutia madhambi waumini wao wao wa me chukua sehemu ya mungu
 
Lakini Biblia inaonyesha wote walioomba waliomba wafu wao wafufuliwe si kupunguziwa adhabu au kusamehewa dhambi.

Kwa nini kipindi hiki tusiombe kufufuliwa wapendwa wetu badala yake tunakesha machana na usiku kuomba wapunguziwe adhabu??
Unafikiri huu Mstari unamanisha nini.
Yohana 11:25
Yesu akamwambia Mimi ndio ufufuo na Uzima, yeye aniaminiye mimi hatakufa bali atakuwa na uzima....Unafikiri ni uzima wa hapa Duniani..??
 
Kwanza niseme mimi ni deist kwa sasa(imani yangu bado inakua)

Nina uelewa kiasi flani kuhusu uislam na misingi yake, lakini pia nina ufahamu mkubwa wa ukiristo, ukiachia mbali ndio mfumo wa imani niliokulia, lakini pia ndio mfumo wa maisha ninaouishi.

kuna utaratibu wa watu kupeleka ndugu zao waliokufa katika nyumba za ibada kuwaombea kabla hawajazika.

Naomba kujua mantiki (logic) ya hicho kitendo. imani inazungumzia walio hai na inawataka wao wakiwa hai waamini.

Kama maombi kwa marehemu yanaweza au yanabadili hatima yake, kuna haja gani mtu kuamini akiwa hai wakati hata akifanya mabaya bado siku akifa ataombewa na atasamehewa na huyo Mungu?

naomba kujua kwa imani yako umuhimu wa maombi kwa marhemu.

Natanguliza shukrani.
Kuwaombea na kuwaomba wafu hayo ni mafundisho ya kipagani ndani ya ukristo kimsingi hayana mashiko yoyote kimaandiko zaidi tu ya kumkufuru Mungu

Anaepaswa kuombewa na kuongozwa sala ya tobani mgonjwa sio marehemu, Mungu wetu ni wa walio hai wala si wa wafu, mfu hana habari yoyote ile ni kama tu ilivyokuwa kwako kabla hujazaliwa
 
Hakuna kitu kinachoitwa toharani mkuu.
Huenda neno hilo toharani halipo moja kwa moja kwenye Biblia...Ila mantiki na maana ya Toharani ipo wazi kwenye Biblia..

Ni mafundisho ya kipagani tu yaliyopenyezwa ndani ya kanisa.
Hapana...Siyo ya Kipagani..ila yapo wazi kwenye Maandiko Matakatifu...

Roho ya mpinga Kristo ilianza kufanya kazi kipindi kirefu,
Kipindi kirefu ni kipindi gani..? Kuwaombea ndugu zetu Mungu awapatie Rehema ni kumpinga Kristo...? Mungu ni mkatili kiasi hicho...?
hata wakati wa mitume kama kina Paulo ilikuwa imeshaanza,
Una uhakika na hiki ulichoandika..? Hiyo Roho ipoje? Inampingaje Kristo...?
ndio iliyopachika haya mafundisho ya utawala wa Kirumi ndani ya Ukristo.
Unaweza ukatupa ushahidi wa haya..?
 
Wewe ndo ******** hujui unachokiandika.halafu wewe si Mkatoliki maana hatuna Wakatoliki Matutusa wasioijua Biblia umeamua kujifanya mkatoliki.Acha na sisi wewe.Mnatusema sana lkn Mwisho wa siku kitaeleweka tu Mjinga ni nani na Mwerevu ni nani??.
Usilolijua ni sawa na usiku wa giza
 
Mkuu nipe maandiko matakatifu kuthibitiaha utetezi wako. Makanisa yetu yanapopotoka, waumini tuna haki ya kuhoji

Nina mengi tu ya kulihoji kanisa langu Katoliki kama ni halali ktk maandiko. Ibada ya kuabudu ufundi idols ijumaa kuu huku ikiwa imekatazwa wazi ktk amri ya pili ya Mungu ni jambo la kushangaza. Kuabudu mkate na Divai tunavunja wazi amri ya pili

Nahitaji kufundishwa sana, la sivyo ni halali kusema kwamba kanisa langu liko nje ya misingi ya ukristo

Haya ni maoni yangu binafsi mkuu. Niko tayari kukosolewa kwa maandiko ya biblia takatifu
Sina muda wa kupoteza na wewe.....Hivi unafikiri uta catch-up attention ya watu kwa kujiita ati wewe ni Mkatoliki..? Unajitoa ufahamu kabisa na kutufanya sisi ni wajinga kiasi cha kushindwa kung'amua Mkatoliki ni yupi na yupi ni mamluki....

Hebu nenda kalale bana .
 
Kuwaombea na kuwaomba wafu hayo ni mafundisho ya kipagani ndani ya ukristo kimsingi hayana mashiko yoyote kimaandiko zaidi tu ya kumkufuru Mungu
Kwahiyo Biblia pia inamafundisho ya Kipagani...?

Anaepaswa kuombewa na kuongozwa sala ya tobani mgonjwa sio marehemu,
Yes! Ule mwili unarudi Mavumbini ila Roho inamrudia Mungu aliyeitoa.. Mhubiri 12:7

Mungu wetu ni wa walio hai wala si wa wafu,
Unajua Biblia tusisome kama Kasuku.....Yohana 11:25 ....Ahadi hiyo ya kuwa hai unafikiri ni uhai gani hasa Yesu alikuwa anatuahidi...???? Labda huamini kuwa kuna maisha baada ya kifo...
mfu hana habari yoyote ile ni kama tu ilivyokuwa kwako kabla hujazaliwa
Roho yake bado ipo hai...Ipo kwa Mungu..

Mhubiri 12:7 Nao mwili hurudi mavumbini ulikotoka nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa....

Mbona maandiko yapo wazi jamani..
 
Lazaro alipofariki hakwenda yeye kwa yesu ili afufuliwe bali ni walio hai walimwombea kwa Mungu na Mungu ili mwenye huruma alimfufua. Halikadhalika wafu hawana uwezo tena wa kuomba ila kama sisi tulio hai tutawaombea kwa Mungu, Mungu atawafufua na kuwaondolea azabu ya kaburi. Katika biblia hakuna sehemu yesu alimfufua mtu pasi na maombi toka kwa wafiwa. Wafiwa waliomba kwa yesu naye aliwasikiliza vilio vyao na kuwafufua wapendwa wao.
Kuna haja gani ya kutenda mema duniani sasa wakat hata nikifa nina dhambi mtaniombe? Acheni kudanganya watu nyie Mungu alisema mfu hana alijualo na aliagiza kutenda mema ukiwa hi
 
Back
Top Bottom