Naomba kujuzwa kwanini marehemu anaombewa?

Naomba kujuzwa kwanini marehemu anaombewa?

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,151
Reaction score
20,068
Kwanza niseme mimi ni deist kwa sasa(imani yangu bado inakua)

Nina uelewa kiasi flani kuhusu uislam na misingi yake, lakini pia nina ufahamu mkubwa wa ukiristo, ukiachia mbali ndio mfumo wa imani niliokulia, lakini pia ndio mfumo wa maisha ninaouishi.

kuna utaratibu wa watu kupeleka ndugu zao waliokufa katika nyumba za ibada kuwaombea kabla hawajazika.

Naomba kujua mantiki (logic) ya hicho kitendo. imani inazungumzia walio hai na inawataka wao wakiwa hai waamini.

Kama maombi kwa marehemu yanaweza au yanabadili hatima yake, kuna haja gani mtu kuamini akiwa hai wakati hata akifanya mabaya bado siku akifa ataombewa na atasamehewa na huyo Mungu?

naomba kujua kwa imani yako umuhimu wa maombi kwa marhemu.

Natanguliza shukrani.
 
Kwanza ...

Kama walijisahau au walisahau kujiombea , maombi yatasaidia kama Mungu atayapa thamani maombi ya wanaomwombea.
Inawezekana mtu huyo alifanya mazuri kwa watu wanaomwombea na watu hao wanamwomba Mungu amtazame kwa jicho la rehema. Mungu ni mwingi wa rehema.

Ndio sababu tunaamrishwa tutende mambo mema. Kwa sababu mambo hayo ni akiba isiyooza.
 
Kwenye Ukristo wa Kiprotestant hakuna maana yoyote ya kumuombea mtu akiwa amefariki maana Biblia inakataza kabisa ibada za wafu.

Ila ibada ile ya siku ya msiba ni kwa ajili ya kuwafariji tu na kuwakumbusha wanadamu umuhimu wa kumkumbuka Mungu kabla ya umauti ndio maana huwa yanasisitiswa mahubiri zaidi kuliko sala.

Ibada ile siku ya msiba ni muhimu kwa sababu kubwa kwamba ni kipindi kigumu sana kwa wafiwa kuondokewa na mtu wa karibu(kama umeshawahi kufiwa utalijua hili) na jamii ya kiroho inabidi iwe karibu sana na wafiwa.

Jambo jingine nafikiri ni busara tu ya viongozi wa kidini kuzuia mabalaa yanayoambatana na misiba, kwa maana misiba hutumiwa sana na washirikina kufanya mambo yao mazito kwa waliobaki, lakini pia kupenyeza imani zao za kishirkikina.

Ibada ya Kimungu isipofanyika hupelekea watu waliofiwa kugeukia upande mwingine wa kishetani kufanya matambiko na matambiko ya misibani huwa yana nguvu sana kufunga hata vizazi vinne alivyoviacha marehemu.

Binafsi naunga mkono ibada hizi siku za misiba, japo si katika kuwaombea waliokufa wasamehewe dhambi au kupunguziwa adhabu, ila kwa ajili ya kuwalinda hawa waliobaki kiroho, maana zisipofanyika shetani ata-take advantage na matambiko lazima yatafanyika tu.
 
Galatians 6:7, Inasema apandacho mtu ndicho atakachovuna, Hivyo mwanadamu hana mamlaka ya roho ya mtu ,Ezekiel 18:4 Mungu anasema roho zote ni mali yake yeye , hivyo hutoa hukumu bila kushawishiwa na kiongozi yeyote wa dini.
ANAYETEGEMEA KUOMBEWA AKIFA IMEKULA KWAKE, Aokoke aishi ktk mapenzi ya Mungu Hakika atakuwa salama.
 
Marehemu haombewi ile ibada ya mazishi baadhi ya vifungo hutoka kwenye biblia, so ile ibada huwa kwa walio hai. Ndo maana mchungaji hunukuu vifungu ka uliumbwa kwa udongo na mavumbini utarudi na kumalizia kuwa siku ya mwisho Yesu atamfufua marehemu siku ya mwisho.
 
Katika maombi kwanza uelewe kuna kukubaliwa au kukataliwa.inawezekana ikasaidia kama yatakubaliwa au isisaidie kama yatakataliwa.akili kichwani mwako
 
ibada huwa kwaajili ya wale wazima kuwakusha kutenda mema na pia kuwathibitishia kuwa njia yetu ni moja
 
Wazee wetu walikua na elimu ya kuongea na roho za marehemu zama hizo nasio jambo la ajabu kwa wenye elimu na nafani ya kiroho
 
Kwa hiyo unapo muombea maombi yote yanafika kama vile angukuwepo haï
 
Maiti nimwili sio roho
Mwili unakufa roho inakua hai kwahiyo tofauti ni kwa mwili tu
 
Ibada yoyote itakayo fanywa kwa ajili ya maiti inamfikia bila shaka
 
Ibada inapaswa kuwa ya kumshukuru Mungu kwa maisha ya huyo mtu hapa duniani na kuifariji familia huku ikitukumbusha tuluobakia jukumu letu la kumtumikia Mungu

Kumuomba Mungu amsamehe marehemu huo ni wendawazimu. Ukristo unasema wazi kutubu ukiwa hai, ukishakufa hakuna namna yoyote ya kupunguza adhabu ya Mungu kwako

Makanisa hasa RC (ambalo mimi naabudu) sijui wanatoa wapi huu utaratibu wa kuwaombea marehemu ndani ya vitabu vya Mungu
 
Kwanza niseme mimi ni deist kwa sasa(imani yangu bado inakua)

Nina uelewa kiasi flani kuhusu uislam na misingi yake, lakini pia nina ufahamu mkubwa wa ukiristo, ukiachia mbali ndio mfumo wa imani niliokulia, lakini pia ndio mfumo wa maisha ninaouishi.

kuna utaratibu wa watu kupeleka ndugu zao waliokufa katika nyumba za ibada kuwaombea kabla hawajazika.

Naomba kujua mantiki (logic) ya hicho kitendo. imani inazungumzia walio hai na inawataka wao wakiwa hai waamini.

Kama maombi kwa marehemu yanaweza au yanabadili hatima yake, kuna haja gani mtu kuamini akiwa hai wakati hata akifanya mabaya bado siku akifa ataombewa na atasamehewa na huyo Mungu?

naomba kujua kwa imani yako umuhimu wa maombi kwa marhemu.

Natanguliza shukrani.
Umesema wewe sasa ni imani gani?
 
Back
Top Bottom