Life After Life: Je, wajua Magufuli huko alipo anayaona yote? Je, tuendeleze 'double standards' ya 'cherry picking' au tuiachie Karma iwashughulikie?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,544
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huwa naweletea makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" Makala ya leo ni kuhusu dhana ya kitu kinachoitwa "Life after Life", ambapo najikita kwenye maswali haya Je, wajua kuwa, binadamu hata baada ya kufa, bado anaendelea kuishi?. Mfano rais Magufuli, japo amekufa, ni amekufa kimwili tuu, ndio hatuko naye, lakini kiroho JPM, bado tuko nae, na huko alipo, bado yuko hai kiroho na kwa kutumia macho ya roho, anayaona mambo yote yanayoendelea kwenye Tanzania yake?.

Je, hiki tunachokifanya kwa baadhi ya wale aliowapenda, are we doing him right?, are we fair to him kwa hawa vijana wake?. Na kama issue ni viongozi waliofanya uovu kipindi cha awamu ya tano, wako wengi wamefanyiwa uovu, Ben Saanane alipotezwa baada ya kuposti kitu humu jf, Azory Gwanda alifuatwa na gari nyeupe ya mkonga ikampeleka hadi shambani kuchukua ufunguo wa nyumba kwa mkewe, wakaenda nae kwake kumpekua, wakaondoka nae and that is the end of him, hakuna majambazi yoyote yanamchukua mtu na kwenda kumpekua kisha kutokomea nae!.

Tundu Lissu alipigwa risasi mchana kweupe kwenye eneo la high security area huku likilindwa na CCTV, mpaka leo hakuna taarifa zozote za uchunguzi. Kumetokea matukio mengi tuu ya kutisha na kusikitisha yaliyotokea Awamu ya 5, swali ni je tuendelee kuwashughulikia kwa double standards kwa kutumia mfumo wa cherry picking kwa kuchagua baadhi tuu wa kushughulikia na wengine kuwa spaired, au tuiachie karma ndio iwashughulikie? kwasababu kwenye karma, hakuna mswalie Mtume, kila jiwe litapinduliwa!.

Muumini wa Karma na After Life
Naomba kuanza kwa kujitambulisha kuwa mimi sio tuu ni muumini wa karma, pia ni muumini wa after life na reincarnation. Hivyo rais Magufuli japo ametutoka na hatupo nae tena, ametutoka kimwili tuu, lakini kiroho bado tuko nae, na huko alipo anayaona yote yanayoendelea baada ya yeye kutangulia mbele ya haki, na anaona jinsi mnavyowatenda baadhi ya viongozi vipenzi wake kwa kuwa persecute kwa kuwa prosecute, kwa kuwadhalilisha!, Jee huku ndiko kumuenzi? Suppose yeye mwenyewe angekuwepo hai, na madudu ya Ole Sabaya yakaibuliwa, Jee Ole Sabaya angetendwa alivyo tendwa majuzi?. Hivi hatuwezi kumprosecute mtu with dignity?. Mjue Magufuli huko aliko bado yupo na anaona yote tunavyowatenda watu watu, asije akakasirika na akamlilia Mungu, watu wengine wakaitwa!.

Mimi na utetezi za haki za binaadamu, sikuanza leo, nilipigania adhabu ya kifo ifutwe, hata wahalifu, watesaji na wauwaji wanastahi kutendewa haki na dignity!
Naomba kujitanabaisha kuwa mimi ni mtetezi huru wa haki za binaadamu, humu jf nina mabandiko zaidi ya 100 ya utetezi wa haki, na kwenye gazeti la Mwananchi la kila Jumatano, na Nipashe la kila Jumapili, nina safu ninaandika makala za utetezi wa haki za binaadamu. Japo siungi mkono matendo ya kihalifu au uhalifu wa aina yoyote, ukiwemo uhalifu wa Ole Sabaya, lakini siungi mkono udhalilishaji wa aina yoyote anaofanywa na jeshi la polisi, magereza, vyombo vya uchunguzi, ofisi ya DPP, na vyombo vya utoaji haki, mahakama, mfano jana pale Mahakamani, Ole Sabaya ameletwa huku amefungwa pingu, as if ni kibaka! Kama haitoshi, akachuchumalishwa as if kumzuia asitoroke!. Huu ni udhalilishaji, huyu ni mmoja wa viongozi vipenzi wa JPM. Kabla hajateuliwa DC, alikuwa anakabiliwa na kesi mbaya ya jinai kufanya tukio la kihalifu kwa kujifanya TISS, JPM akamnasua kwa kumteua kuwa DC ikabidi DPP akaifuta hiyo kesi kwa nolle. Sasa kwa vile kuna ahadi ya kumuenzi JPM kwa mazuri yake, then tumuenzi kwa mtindo wa boga, ukipenda boga, penda na ua lake, na kwasababu sasa JPM hayupo, tukiamua kuwatupa watu wake, then tuwatupe kwa kutumia mtindo wa kumtupa jongoo, ukitupa jongoo, usitupe na mti wake!. Kama tulimpenda JPM, na tukaahidi kumuenzi, then tuwapende na watu wake aliowapenda, hivyo Ole Sabaya, awe treated fairly with dignity huku tukikumbuka kuwa Magufuli anayaona yote tunavyowatenda viongozi vijana wake!, huko aliko, asije akakasirika, akamlilia Mungu, watu wakaitwa bure!.

Life after life in Christianity: Mwili wa nyama ndio unakufa na kugeuka mvumbi, mwili wa roho, haufi, na unaishi milele!.
Hii dhana ya after life, karma and reincarnation sio dhana ya kwenye imani ya dini kuu mbili, za Kikirsto na Kiislamu, hii ni dhana ya dini ya Hinduism na Budhism ila kwenye ukiristo pia ipo.

Uhai ni nini na kifo ni nini?
Mwili wa binadamu una sehemu kuu mbili, mwili na roho. Sehemu ya kwanza ni huu mwili wa nyama, ambao umeumbwa kwa udongo ukapuliziwa pumzi ya uhai, na siku ukifa, kinachokufa ni mwili huu wa nyama, unazikwa kaburini, humo ndani unaoza na kurudi kuwa mavumbi. Sehemu ya pili ya mwili ni roho, life force, uhai hii ni pumzi Mungu aliyoipulizia kwenye ule udongo hivyo mwili kupata uhai. Hii ni Roho ya Mungu, the spiritual body, the astral body, mwili wa nyama unapokufa, roho haifi, bali roho huacha mwili na kurudi kwa Mungu. Hivyo kifo ni kitendo cha mtu kukata roho ni kitendo cha roho kuacha mwili, hiyo roho, haifi bali inatoka na ndio inayokwenda mbinguni mbele ya Mungu, ndiyo inayohukumiwa, ndio inayokaa peponi au motoni.

Je, baada ya kifo, hiyo Roho inakwenda kuishi wapi?
Kama ulivyo mwili una sehemu mbili ya mwili na roho, mwili wa nyama na mwili wa roho, vivyo hivyo dunia ina sehemu mbili, Ulimwengu wa Kidunia, the physical world, na Ulimwengu wa Roho, the Spiritual World, mtu akifa, roho ikiacha mwili, mwili unabaki kwenye ulimwengu wa dunia, unazikwa unaoza na kugeuka kuwa mavumbi, Roho inakwenda kwenye ulimwengu wa Roho kuendelea kuishi milele, being mbinguni, peponi, kuzimu, toharani, au jehanum kwenye ziwa la moto wa milele, hii subject nyingine lakini roho hazifi kwa sababu roho ni Mungu. Hivyo mwili huo wa roho, unaona kila kitu kinachoendelea hapa duniani.

Ufufuko wa miili na uzima wa milele, miili itakayo fufuliwa ni miili ya roho, ile miili ya nyama ikiisha zikwa, that is the end
Wakristu tunakitu tunaita fumbo la imani, tunaamini Yesu alikufa, Yesu alifufuka na Yesu atakuja tena kuwahukumu wazima na wafu, na ufalme wake hautakuwa na mwisho, ambapo kutatokea ufufuko wa miili na uzima wa milele, miili itakayohusika kwenye ufufuko wa miili ni miili ya roho na sio hii miili ya nyama. Kuna wengi pale wapendwa wetu wanapokufa, tunawazika kaburini, na kwa kadri ya uwezo, mwili unavishwa vizuri, kaburi linajengwa vizuri, na kuna watu huenda makaburini kufanya ibada za wafu, bila kujijua, hivyo wale wanaochoma miili kuonekana kama hawamtendei haki marehemu, ukweli ni kwamba, roho ikiisha acha mwili, that is the end of body, mwili hauna issue tena, unarudi mavumbini, mambo yote ni roho. Hivyo ninaposema Magufuli yupo na anaona kila kitu, ni kweli yupo na anaona.

Jee Roho za Waliokufa Huweza Kurejea Duniani?.
Yes, kwanza kwa wale wanaokufa katika mazingira ya kutatanisha, miili yao isipatikane wakazikwa rasmi, baadhi yao roho zao hubaki duniani, zikitanga tanga na sometimes zikisumbua, hizi zinaitwa "wondering spirits", kuna baadhi ya majumba hayakaliki kwasababu kuna roho zinasumbua, majumba haya huitwa "hauted houses". Kuna baadhi ya wafu huwatokea walio wazima ama kwenye ndoto, ama kwa visions kama Bikira Maria alivyowatokea wale watoto kule Fatima, Louedes Ufaransa. Mara nyingi wafu hurejea kama mizimu, hivyo kuna wengi wanalindwa na mababu bila ya wao kujijua, uthibitisho ni vitu vinavyoitwa miraculous escapes, inatokea ajali mbaya ya kutisha, gari linabondeka na kuwa chapati, halafu unakuta watu wametoka wazima, hata scratch hawana!.

Je, kwenye ahadi ya kumuenzi Magufuli tumuenzi kwa yote au tuchague mazuri tu?
Kwavile rais Magufuli hakuwa malaika, alikuwa ni binadamu, hivyo ana mazuri yake, na pia ana mabaya yake ya kibianadamu kama binaadamu mwingine yoyote, hakuna aliye mkamilifu, hivyo tumuenzi Magufuli kwa mema na mazuri yake kwa kuyaendeleza, halafu yale ya kibinaadamu, tumuachie mwenyewe, tuwe tumemzika nayo siku ile pale Chato na tusiyazungumzie mabaya yake ili kuepuka kumzungumzia vibaya marehemu, ili kumuacha marehemu apumzike kwa amani, ila kwenye kuzungumzia mabaya hayo kwa lengo la kutoa angalizo kwa kuwasaidia waliopo ili yale mabaya hatarishi yenye bad karmic consequenses yaepukwe, yasije yakajirudia, tukaja kujikuta tunapoteza wengine, maana karma haijui cha nani wala nani, ikifika stage ya karma kula kichwa, karma inakula kichwa!. Kwa vile tuna wazee wa kusoma karma trends humu, tunawajibu wa kuwasaidia viongozi wetu, waliongoze vizuri taifa letu kwa kuepuka kufanya makosa ya nyuma.

Baada ya Bwana Yesu kufa kwa mateso ya kusulubiwa na kifo msalabani, wanafunzi wake walijifungia kwa kuhofia na wao kusulubiwa, ndivyo ilivyo kwa Baadhi ya Watu wa Magufuli
Vivyo hivyo baada ya kifo cha Magufuli, kuna baadhi ya watu walilia kwa mengi wakiwemo wamachinga, Magufuli aliwaruhusu kufanya biashara popote, matokeo yake kwenye baadhi ya maeneo sasa ni balaa!. Siku Wamachinga wakiondolewa, watalia tena na kumkumbuka Magufuli, na wao pia watauliza kama kufukuzwa kwao ndiko kumuenzi Magufuli?. Ili kuwaelimisha watu wa aina hii, ni lazima waelimishwe kuwa hata Magufuli hakuwa mkamilifu, ataenziwa kwa mazuri tuu, hili la kuwaruhusu machinga kufanyabiashara popote, sii miongoni mwa mazuri ya kuenziwa, bali watawekewa utaratibu rasmi wa machinga kufanyabiashara bila kuwa kero kwa wengine.

Vivyo hivyo kwenye wateule wa JPM, kuna baadhi ya viongozi Magufuli aliwapenda sana, matokeo yake wakavimba vichwa, wakajiona kama miungu watu, wanaweza kufanya lolote na wasifanywe chochote, na hawakuamini kama Magufuli naye ni binadamu tuu, leo yupo, kesho anaweza asiwepo, au anaweza kufa. Mmoja wa wa watu hawa ni Comred Ole Sabaya, siku ya mazishi ya Magufuli, mmoja kati ya waliolia sana ni Ole Sabaya, inawezekana alilia kwa mengi, uchungu wa kufiwa na mtu unaempenda sana, au wasiwasi wa nini kitampata baada ya nguzo na egemeo lake kuanguka, ndio maana mkamuona akifanya juhudi kubwa, ikiwemo kwenda Clouds kujisafisha, but very unfortunately, haikusaidia, sasa yuko korokoroni aki treatiwa kama kibaka!.

Viongozi wahalifu kipindi cha Awamu ya Tano ni wengi, sio Sabaya pekee. Kama tumeamua kushughulika nao, tuwashughulikie wote
Kwenye awamu ya Tano, viongozi waliotenda mambo ya ajabu ajabu ni wengi, sio Ole Sabaya peke yake, kama awamu hii ya 6 ya Mama Samia, imeamua kuwashughulikia, then iwashughulikie wote. Tuache kufanya double standard ya cherry picking kuwashughulikia baadhi, na kuwaacha wengine, tena baadhi yao Mama Samia kaamua kuendelea kuwabeba mfano mzuri ni RC mmoja alimuamuru RPC wake kuwa namna ya kupunguza msongamano magerezani, ni kuwapiga risasi na kuwaua papo hapo vibaka wote!, na kujiproud kwa ushujaa wake jinsi alivyo muua kibaka kwa kumpiga risasi mbili za kichwa na kumuua papo hapo, kisha akajipongeza kwa kunywa bia mbili!.

Rais Mama Samia Kaanza Vizuri, Angeweza Kuibwaga Mizigo Yote ya Magufuli, Lakini Kafanya Uungwana Mkubwa ya Kuwatumbua, Kiungwana na Kistaarabu huku Akiwapooza Baadhi
Kwa vile kuna viongozi Rais Magufuli aliwapenda, Rais Mama Samia halazimiki kuwapenda, ndio maana tangu Rais Samia alipoingia tu, ameanza vizuri, mfano kitendo cha kuutengua uteuzi wa Dr. Bashiru kutoka Katibu Mkuu Kiongozi, na kumpa ubunge, japo ni demotion ya kistaarabu, lakini angalau amempooza kwa ubunge. Kiukweli Mama Samia ni muungwana sana na mstaarabu sana, mimi ni miongoni mwa watu wa mwanzo kuupongeza uamuzi huo, nikazitolea pongezi zangu hewani kupitia Sauti ya Ujerumani na BBC Swahili. Ubunge wa Bashiru Ali, wachambuzi wanasemaje? | DW | 01.04.2021

Kwavile hili ni bandiko la life after life, yaani Magufuli huko aliko anayaona yote tunayawatendea aliowapenda, kama wakati wa Magufuli, sisi Watanzania, tuliwavumilia, na sasa wakati wa Samia, pia tuendelee tuwavumilie, na hata kama ni kuwaadhibu, Mungu anatufundisha tusilipize visasi, tusiwasulubishe kwa udhalilishaji kama alivyofanyiwa Ole Sabaya, kitendo cha kutoteuliwa, kutoka mtu uliekuwa everthing, then he is reduced to nobody ni adhabu tosha, itoshe, kwasababu no one knows kwa sasa kule mbinguni Magufuli amepewa wadhifa gani, inawezekana yuko karibu sana na Mungu, hivyo akiona jinsi tunavyowatendea wale aliowapenda kama Sabaya, akakasirika na kumuomba Mungu, awaite baadhi ya watu!. Kama yeye mwenyewe aliweza kuitwa na sasa hayupo, then anyone anaweza kuitwa anytime, lets not risk viongozi wengine kuitwa. Hao waliofanya uovu, baada ya kutoteuliwa, itoshe, tuiachie Karma iendelee kushughulika nao.

Nawaaga kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Kazi Iendelee.

Paskali
 
Pascal utaharibu mambo Wengine wameomba msamaha tayari

Kheri James aliomba msamaha kwa aibu lakini alijitahidi kidogo, Usimsagie kunguni maana Wengine waliropoka tu hawakufanya kwa vitendo kama Ole Sabaya

Unazidi kuwasagia watu kunguni

Unapotaka kujenga utaifa upya lazima uwashughulikie mtu kama Sabaya

Akiwashughulikia Bashiru na Polepole hapo sasa ndio Climax unakuwa umejenga Taifa moja la upendo na Amani aliloliacha Mwalimu Nyerere

Marehamu akishakufa amekufa tu

Pascal kwa mujibu wa Biblia, Maisha ya mwanadamu ni kama jani tu hunawiri na kusinyaa baadae linakatwa

Mwendazake hayupo, Huyu angepewa mitano tena ilikuwa balaa Tanzania

Hebu Fikiria magazeti yalikosa soko yaligeuka magazeti ya kuuzia vitumbua, Maana walikuwa wanachora Madaraja na SGR kila siku Front page

Nani alisoma magazeti, Leo hapa nataka nikanunue gazeti nisome watu aliowaumiza Sabaya,

Ni mwisho wa enzi
 
Ukiwa unaadhibiwa huna muda na mambo mengine. Ana damu za watu wengi sana wasio na hatia, kuanzia waliookotwa kwenye viroba ( wengine ni vyombo vya ulinzi wakidaiwa ni wasaliti), waliopotea wasijulikame walipo, walionyongwa ( RIP Lwajabe) waliopigwa risasi, waliotiwa sumu( RIP Mr Ben,RIP Mahiga), waliotekwa na kuteswa, walioua kama wahanga kwa makosa ya eatu wengine( huko Mkiru sio chini ya watu 400, huko Mwanza na Arusha), waliodhulimiwa mali na kuchukiliwa pesa zao na kusababisha kufariki kwa pressure

Tusidanganyane huko ni adhabu tu hana muda wowote wa kuona chochote.
Mkuu Pasco Jiwe sasa hivi ananyukwa makonzi na kina Azory na Ben. Anaomba msaada kwa mzee wa Lupaso lakini anamkwepa.
 
Marehemu kuwa anayaona yanayoendelea hapa juu ya ardhi haimaanishi kwamba ule ubinadamu wake hauwezi kutumiwa kwa watu kujifunza mema yake na kuyaendeleza na wakati huo huo kuhakikisha upungufu wake hauendelei kurithiwa na wengine walio hai.

Marehemu yoyote anastahili kutetewa kwani hana uwezo wa kujitetea lakini ule ukweli kuhusiana na maisha yake ni lazima utambulike kwa watu, ndio maana wenye maono huacha vitabu vikiongea kwa niaba yao.
 
Huu uzi umepoteza maana kwenye hii paragraph.

Mimi na Utetezi za Haki za Binaadamu, Nilipigania Adhabu ya Kifo Ifutwe, Hata Wahalifu Wanastahi Kutendewa Haki na Dignity!.
Naomba kujitanabaisha kuwa mimi ni mtetezi huru wa haki za binaadamu, na kwenye gazeti la Nipashe la kila Jumapili ninaandika makala za utetezi wa haki za binaadamu, japo siungi mkono matendo kihalifu ya uhalifu wowote, ukiwemo uhalifu wa Ole Sabaya, lakini siungi mkono udhalilishaji wa aina yoyote anaofanyanywa na polisi, magereza, mahakamani na vyombo vya uchunguzi, jeshi la polisi, vyombo vya uchunguzi, ofisi ya DPP, na vyombo vya utoaji haki, mahakama, mfano jana pale Mahakamani, ameletwa huku amefungwa pingu, as if ni kibaka!. Kama haitoshi, akachuchumalishwa as if kumzuia asitoroke!. Huu ni udhalilishaji, huyu ni mmoja wa viongozi vipenzi wa JPM. Kabla hajateuliwa DC, alikuwa anakabiliwa na kesi ya jinai kujifanya TISS, JPM akamteua, ikabidi hiyo kesi ife. Kwa vile kuna ahadi ya kumuenzi JPM, then tumuenzi kama ukipenda boga, penda na ua lake, na ukitupa jongoo, usitupe na mti wake!, kama tulimpenda JPM, na tukaahidi kumuenzi, then tuwapende na aliowapenda, hivyo Ole Sabaya, awe treated with dignity huku tukikumbuka kuwa Magufuli anayaona yote tunavyowatenda viongozi vijana wake

Wakati mwingine pasco huwa unajitoa ufahamu. Sabaya ni jambazi kama majamnazi wengine. Ni mnyanganyi kama wanyang'anyi wengine. Ni mtesaji kama watesaji wengine. Tofauti hapo ni cheo alichokuwa nacho. Ambacho kakitumia vibaya. Sabaya si mtu wa kumwonea huruma. Mwacheni alipe kwa alichowatendea watu.
 
Mkuu acha kutisha watu kisaikolojia! Tanzania inaongozwa kwa utawala wa sheria. Katika hili kila mtu yuko chini ya sheria, hivyo yeyote anayetenda kinyume na sheria anakuwa anatenda jinai

Kumbuka kosa la jinai halina limit ya muda, uaweza kuja shitakiwa kwa uhalifu wako hata miaka 20 ijayo

Hata ingetokea hii nchi ikatawaliwa na Rais wa kutoka upinzai baada ya Magufuli kustafu(kama angekuwa hai) sio ajabu wangekuwa kundi moja na Sabaya kweye hizi kesi

Kuna watu wanaloloma ooooh! Mama anatenda kinyume na Mwendazake, lakini wanasahau kuwa Mama aafuata katiba ina inavyomuongoza, na hicho ndicho alichoapa katika kiapo chake hivyo hawezi tenda kinyume na katiba

Tutafte namna nyingine ya kumtetea Mwendazake ila si kwa kuhalalisha maovu yake!
 
Back
Top Bottom