Naomba kujua mshahara wa Rubani.

Baada ya hii ajali ya jana iliopelekea kupoteza maisha ya wanadamu wenzetu, nimejikuta nikiwaza sana kuhusu kumshauri mwanangu kusomea urubani.
Ni nini hasa kinachowavutia watu kusomea na kufanya urubani? je kazi hiyo ina maslahi makubwa kuliko kazi hizi unazofanya miguu yako ikiwa ardhini mfano udaktari, uhasibu, uanasheria, siasa, biashara n.k? Au ni ile status kwamba unarusha ndege? Au ni kusafiri nchi mbalimbali? Naomba mwenye kujua anijuze.
Ndege ni salama mara tisini zaidi ya gari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana ni mishahara ya kuridhisha, lakini kuna visa viwili hapa vinaonesha inawezekana kuna baadhi ya mashirika kuna shida kama sehemu nyingine tu.
1. Kuna rubani msaidizi mmoja ameshawahi kuzipiga kavukavu na rubani mkuu kisa kila siku anaambiwa ahesabie abiria wakati yeye kasomea kuendesha ndege. Kama sikosei ile siku walizuiwa kurusha ndege.
2. Kuna ajali ilitokea kama miaka miwili iliyopita, uchunguzi kupitia kiboksi cheusi ulionesha kabla ya ajali kulikuwa na ubishani kwenye chumba cha marubani, dakika chache baadae ndege ilishuka chini kwa nguvu. Yaani ni kama ajali ilitokea kwa makusudi. Historia ya rubani msaidizi ilionesha alikuwa na msongo wa mawazo. Siku chache kabla ya ajali kwa mujibu wa mpenzi wake, anasema amechoka kuwa msaidizi miaka nenda rudi, Kuna siku angefanya tukio LA kumfanya akumbukwe.
Na mwisho Kuna rubani mmoja hapa Afrika mashariki anafanya muziki pia, yaani ni msanii wa kuimba. Nadhani kazi ya urubani ingekuwa inamlipa sana PENGINE angetulia nayo hiyo tu.
 
Mshahara wa rubani katika mashirika mengi makubwa hutegemea na cheo/rank kwanza kisha aina ya ndege anayorusha na pia flying pay. Kwa wanaorusha ndege kubwa mshahara huanzia angalau dola 10000 baada ya kodi hapo jumlisha allowance ya nyumba malipo ya kuruka nk...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafiti zinaonyesha usafiri wa anga ni salama zaidi kuliko usafiri mwingine wowote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakubaliana na wewe Mkuu.

Na katika hili suala la Boeing 737 Max, kuna mambo mengi yanazungumzwa kwa hivyo huenda ni external factors ndo zimesababisha ajali, Maana kuna taarifa kuwa Ubalozi was Marekani ulitahadharisha RAIA wake kuhusu kutumia huo uwanja ambao ndege iliyopata ajali iliondokea.
 
Ajali ni ajali mbona hushangai inakuwaje mtu anaamua kuwa dereva wa basi au malori wakati kila ukipita barabara kuu hukosi kukutana na ajali,na pia kwanini uwazie marubani badala ya kuwashangaa abiria ambao wao ndio wengi zaidi wanapanda ndege, wakati kama unavyosema ndege zina ajali sana,cha muhumiu ni kujiandaa tu mkuu kwani hatujui siku wala saa na hujui kitakuja kwa mtindo gani na utakuwa sehemu gani...
 
Basi au lori lipo hapa ardhini mkuu. Likipata hitilafu yoyote ni rahisi kupaki pembeni na kutengeneza au kutafuta option nyingine. Pia basi au lori likipata ajali ni nadra dereva pamoja na abiria wote kufariki.
 
Nini kinachomfanya mtu apende kuwa mwanajeshi ilihali anatambua wakati wowote vita ikitokea ye ndio mtu wa kwanza kuwajibika!?

Nini kinachomfanya mtu apende kuwa Mlinzi/Bodyguard ilhali anatambua yeye ndio anaweza akawa shabaha eidha ya kwanza ama ya pili!?

Nini kinachomvutia mtu kuwa mvuvi ilhali anatambua kuwa maji hayana sakafu!?
dhiki na maisha.kwa urubani SAA zingine upenzi.
 
Baada ya hii ajali ya jana iliopelekea kupoteza maisha ya wanadamu wenzetu, nimejikuta nikiwaza sana kuhusu kumshauri mwanangu kusomea urubani.
Ni nini hasa kinachowavutia watu kusomea na kufanya urubani? je kazi hiyo ina maslahi makubwa kuliko kazi hizi unazofanya miguu yako ikiwa ardhini mfano udaktari, uhasibu, uanasheria, siasa, biashara n.k? Au ni ile status kwamba unarusha ndege? Au ni kusafiri nchi mbalimbali? Naomba mwenye kujua anijuze.
Mfumo wa kusave pesa kwa kushirikisha wengine na kukuza pesa ndan ya wiki moja
 
Baada ya September 11 vijana wengi walipoteza mwamko wa kazi hii. Niliona documentary ya British Airways wakiwafanyia crush course vijana waliomaliza six form na A au B ya Physics na Geography walikuwa na advantage lakini walichukua pia wenye first degree za masomo mengine wenye first class na upper second.

Ilikuwa course ya miezi 18 kwani walikuwa na shortage kubwa ya ma pilot.

Mshahara kwa walianzia ulikuwa £100,000 kwa mwaka.
 
Nafikiri si jambo jema kubeza kitu au jambo analopenda mtu mwingine. Urubani ni kazi au fani kama fani nyingine, na wapo wanaopenda wafanye hata kwa kujitolea ikibidi na wapo walioifuata kimaslahi tu. Hii ni kila fani mf ualimu, udaktari, uanamichezo, usanii n.k.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom