Gharama ya kumsomesha mtoto awe rubani unaijua? ATCL rubani anapata 6m kama mshahara na kila akiruka analipwa kiasi fulani. Kwa mashirika ya nje rubani anapata kuanzia $10,000 na kila akiruka kuna posho mpaka $500. Bado analipiwa kila kitu huko aendako hio posho ni ya mfukoni tu.Baada ya hii ajali ya jana iliopelekea kupoteza maisha ya wanadamu wenzetu, nimejikuta nikiwaza sana kuhusu kumshauri mwanangu kusomea urubani.
Ni nini hasa kinachowavutia watu kusomea na kufanya urubani? je kazi hiyo ina maslahi makubwa kuliko kazi hizi unazofanya miguu yako ikiwa ardhini mfano udaktari, uhasibu, uanasheria, siasa, biashara n.k? Au ni ile status kwamba unarusha ndege? Au ni kusafiri nchi mbalimbali? Naomba mwenye kujua anijuze.
Wengi wanaendesha ndege kwa kupenda na si Kwa sababu ya mshahara mkubwa