Naomba kujua mshahara wa Rubani.

TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
2,359
2,000
Baada ya hii ajali ya jana iliopelekea kupoteza maisha ya wanadamu wenzetu, nimejikuta nikiwaza sana kuhusu kumshauri mwanangu kusomea urubani.
Ni nini hasa kinachowavutia watu kusomea na kufanya urubani? je kazi hiyo ina maslahi makubwa kuliko kazi hizi unazofanya miguu yako ikiwa ardhini mfano udaktari, uhasibu, uanasheria, siasa, biashara n.k? Au ni ile status kwamba unarusha ndege? Au ni kusafiri nchi mbalimbali? Naomba mwenye kujua anijuze.
 

The Technologist

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
640
1,000
Nini kinachomfanya mtu apende kuwa mwanajeshi ilihali anatambua wakati wowote vita ikitokea ye ndio mtu wa kwanza kuwajibika!?

Nini kinachomfanya mtu apende kuwa Mlinzi/Bodyguard ilhali anatambua yeye ndio anaweza akawa shabaha eidha ya kwanza ama ya pili!?

Nini kinachomvutia mtu kuwa mvuvi ilhali anatambua kuwa maji hayana sakafu!?
 

TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
2,359
2,000
Nini kinachomfanya mtu apende kuwa mwanajeshi ilihali anatambua wakati wowote vita ikitokea ye ndio mtu wa kwanza kuwajibika!?

Chukulia mfano hapa kwetu tangu 1970's hakujawa na vita. Na hata vita ikitokea, bado mwanajeshi ana asilimia kubwa ya kuweza ku survive kuliko ajali ya ndege inapotokea

Nini kinachomfanya mtu apende kuwa Mlinzi/Bodyguard ilhali anatambua yeye ndio anaweza akawa shabaha eidha ya kwanza ama ya pili!?

Urahisi wa kazi yenyewe mkuu. Huhitaji kusomea miaka na miaka ili uwe bodyguard. Tofauti na urubani

Nini kinachomvutia mtu kuwa mvuvi ilhali anatambua kuwa maji hayana sakafu!?

Huyu nafikiri hana option nyingine ndio maisha aliyoyachagua/aliyorithishwa. Rubani anakua na option nyingi tuu za nini cha kusomea. Sasa najiuliza kwanini watu wanachagua urubani?
 

TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
2,359
2,000
in

ilawezekana huo ndio ukawa mshahara wake ila i believe watakua na incentives nyingi sana

Ndio nataka kujua hizo incentives ni kiasi gani mkuu hasa ukizingatia pia mashirika ya ndege mengi yako taabani kifedha
 

ccm mtoto wao

JF-Expert Member
Dec 19, 2018
563
500
Ajali ajali tuu kwan kwann mtu anataka kuwa dereva wa basi,lori au bodaboda wakati anajua kifo njenje, hata jkiwa mhasibu unaweza tumwa safari ya kikazi kenya pia ukapata ajali, kifo hakiepukiki ndugu yang.

get well soon tl
 

busha

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
1,640
2,000
usiogope somesha mtoto urubani mengine ni ajali kazini mkuu
IMG-20190311-WA0006.jpeg
IMG-20190311-WA0002.jpeg
IMG-20190311-WA0003.jpeg
IMG-20190311-WA0004.jpeg
IMG-20190311-WA0005.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

The Technologist

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
640
1,000
Mkuu ukifanya research katika ndege ambazo zinafanya safari na mabasi na vyombo vingine unaweza kukuta Ndege inaongoza kwa kuwa na ajali chache.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom