Kama una mpango wa kuwa padre, basi na usioe. Lakini kama utakuwa mtu wa kawaida, na hauna dosari yoyote (wewe ni rijali), ni lazima uoe. Watu wanafikiri kuoa ni option, la hasha, kuoa ni lazima! Labda uende kwenye daraja nililotaja hapo juu (upadre), ndipo utakuwa exempted kwenye ndoa (kuoa)!
Unakumbuka maneno ambayo Mungu aliwaambia Adam na Hawa mara tu baada ya kuwashusha pale bustani ya Edeni? Nakukumbusha; aliwaambia, zaeni mkaongezeke, mkaijaze dunia. Na ndicho kilichotokea. Kuoa, dhumuni lake kubwa ni kupata watoto, na si vinginevyo (kama wengi wanavyochukulia)
Unaweza kusema, kwani kupata watoto mpaka nioe? Si naweza kuzaa tu na mwanamke halafu nikachukua watoto! Jibu ni kwamba, hao watakuwa sio watoto halali, maana umezini!
Sisi sote ni zao la Adam na Hawa, sasa hebu fikiria, nao wangesema kila mtu aishi kivyake; mwanaume analala peke yake na mwanamke peke yake, labda hata nyumba tofauti! Je, sisi leo tungekuwepo?
Unachojaribu kufanya ni ubinafsi (selfishness), unahofia gharama na mikwaruzano mingine katika maisha (kama ilivyotokea kwa jamaa aliyeleta uzi), hizi ni changamoto za kawaida kwenye maisha, tunapaswa kukabiliana nazo. Oa, pata watoto, timiza jukumu la kuilea familia kama baba. Mbona mimi nafurahia sana kuitwa baba wa familia, baba mwenye mji, nk. Wewe hufurahii?!