Ndani na nje ya chama tawala nani? Angefaa kuliongoza hili taifa pendwa bila migogoro ya ovyo nani? Mnayemwamini kupita kiasi ambaye ataweza kuifikisha nchi yetu kwenye maendeleo ya kueleweka , maendeleo ya kweli
Tuna watu wengi na makini sana kwenye taifa letu na wengine wanaonekana kabsa hawana uchu wa madaraka wamewaachia wenye uchu watoane roho na kuvuana utu na wana elimu ya kutosha ya uongozi na vipawa vikubwa vya kusikilizwa na kueleweka
Nani? Ungependa awe raisi wa Tanzania ambaye unaamini lazima atafanya vizur kwenye uongozi wake
Kizuri hakikosi kasoro hatusemi kama atafanya mazuri 100% hapana lakini at least 80-85% tutajie hapa nani? Anaweza kulisongesha gurudumu hili Kwa nguvu zote
Taja unayemwamini hata kama hajawahi kuwa mbunge au waziri labda ni diwani huko wewe mtaje!! Tu au labda aliwahi kuwa hata raisi miaka iliyopita tutajie
Na ukimtaja kwa chaguo zuri utaweza kukutana naye kwenye kinyang’anyiro cha uraisi 2025-2030-2035-2040 na kuendelea mda bado upo
Na jaribu kumuelezea uliyempendekeza japo kwa maneno 10 mpaka 30 ukizidisha ni sawa, sifa zake ambazo zimefanya umpendekeze, asante
———————————————————————————
———————————————————————————
Uzi uliishia hapa, huku chini ni update za mapendekezo ya wengi na wachache waliopendekeza viongozi wazuri wa taifa letu pendwa.
Tuendelee kuwapendekeza
———————————————————————————
———————————————————————————
———————————————————————————
mpaka sasa mapendekezo mengi yanaenda kwa LUHAGA MPINA
Who is MPINA—kamuangalie U-tube video zake akiwa anahunguruma akiwa bungeni
Vipi? Jimboni kwake ananufaisha jamii na wanajamii wake?
LUHAGA MPINA
jamaa hana skendo yeyote huyuu ya upigaji?
Hawa sio official tutawabadilisha wakitokea wengine wanaovutiwa na watu wengi kuwazidi L.MPINA anafatiwa na HAMFREY POLEPOLE tena anafatiwa na TUNDU .A. LISSU
Ila wakwanza ni LUHAGA MPINA— nipo U-tube napapasa taarifa zake huyu mwamba ni mtu kweli jamaa najaribu kutafuta na skendo zake naona kuna maeneo anahusishwa nayo kama kawapora wananchi ngoja nifatilie vizuri
TUENDELEE KUWAPENDEKEZA TUNAOWAAMINI