M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,020
Sidhani kama ni sahihi kuwaweka Chadema kwenye kundi moja na hizo taasisi 2 ulizozitaja.Chadema wanasema hawakupeleka majina NEC,nani alipeleka?
NEC wanasema Mnyika kama katibu mkuu aliwapelekea majina tena yaliyopewa baraka na kamati kuu ya Chadema. Hii ni kweli au sio kweli?
Spika anadai hawezi kuvua ubunge wabunge ambao kwa mujibu wa katiba ya JMT sasa hivi hawana chama maana walishatimuliwa Chadema. Kisa tu NEC ya Wilson Mahera ilimpa majina. Ok kama NEC ilimpa majina bado wanasifa za kuwa wabunge kama ibara ya 67(b) na 71(e) inavyoweka wazi?
Au ndio kusema undavaundava tu hata kwenye mambo ya kuzingagia Katiba na sheria?
Chadema wanaweza kuupa ukweli umma wa watanzania ili tujue nani alipeleka majina? Nahisi kuna jinai inanukia, kama haipo kuna mtu mkubwa Cdm mpenda dili anahusika,Tanzania nzima inamfahamu.
Chadema washatoa ushahidi kuwa hawakupeleka majina na kama yamepelekwa ni kwa njia ya jinai. Wanataka jinai ichunguzwe na vyombo husika. Vyombo vimepiga kimya.
Chadema wamesha play part yao. The ball is out of their court.
NEC na Bunge wanahitajika sasa ku authenticate maamuzi yao. Bado hawajafanya hivyo.
The ball is now in these 2 institutions' courts.