Uchaguzi 2020 Nani mkweli kati ya hawa watu? Spika, NEC au CHADEMA?

Toka wamemfanyia Lissu hujuma siamini Tena mifumo yetu ya utoaji haki na usimamizi wa sheria credibility Yao ni questionable kwangu Mimi naona wanaweza fanya lolote na wasifanywe chochote.
 
Cha msingi ni kukaa kimya mpaka taifa litakapopata mtawala anaejalu haki umoja maridhiano na utu kwasasa hatuna hizo tunu. Sheria zetu katika awamu ya tano Zina macho zinaamua Nani aadhibiwe Nani aachwe japo kosa ni lilelile.
 
Vipi kama ikionekana Chadema hawakupeleka majina? Uhalali utatoka wapi?
Uhalali wa nini tena jamaa yetu?
km kulinda tu kura CDM haikulinda na Halima Mdee akashuhudia wizi
wapo Kina Silinde Katambi, Mwambe, Waitara, Gekul na wengine walifanyiwa vitimbi na wamepita kwa vitimbwi mpaka wameukwaa uwaziri na unaibu, kwanini wasikubali yaishe
watake wasitake Waliopitishwa wamepita na posho na Magari wanayakwaa sasa hivi kabla ya Febr 2021
Na CDM ikikataa wasiwakilishwe sawa watawawakiisha Watanzania waliobaki
Dalili ya Chama hiki kupotea naiona kabisa hasa baada ya kuondoe uwezekano wa wakubwa kushtakiwa
 
Kama mtu alichapwa risasi 30 na bado akafukuzwa ubunge na mahakama ikabariki unadhani ni kipi kingine ambacho hawawezi kufanya?
Maelezo yako ni butu, hayana mantiki kabisa. Kwa hiyo mtu akipigwa risasi akapona alafu hauzulii bungeni aachwe tu? Wakati anafanya ziara Ulaya na Usa? Kisa nini? Jikite kwenye mada toa pumba zako.
 
Ukumbuke kuwa Mtendaji Mkuu wa NEC, tarehe 23 alisema hawajapokea majina toka CHADEMA. Tarehe 23 ni kabla au baada ya tarehe 19?

Sent using Jamii Forums mobile app
Jombaa mm binafsi nakuelewa vizuri sana. Kwa kumzibitishia huyo ndugu kwa hizo tarehe na yeye kustick kwenye ushahidi wa gazeti la mwanachi!! Ni vyema ukatupia kakideo ka mahela akitoa ufafanuzi kwa hayo mambo.
 
Kwa hiyo kama walikuwa wanatendewa dhuluma kama unavyodai, ndio wafoji saini kuonesha kuwa katibu mkuu wa chama ameidhinisha!? Vipi Nusrat Hanje naye alitolewa gerezani na Chadema ili kufanikisha naye awe mbunge!?
Je unaweza kuthibitisha kwamba saini ilifojiwa!? Hata hivyo, umetoka njenya wazo kuu, ambalo ni kwamba huoni kitendo cha wanachama wenu 19 kuridhia kuunga mkono juhudi, vyovyote vile, ni ishara kukataa ubabe usio na tija wa chama chako!!?
 
Tukubaliane kuwa chadema ilipeleka majina NEC, nao NEC wakawasilisha kwa Bw. Job.

Sasa chadema wamewavua uanachama hao covid 19..

Kinachofuata ni nini? Bw Job na NEC wanasemaje kwa mbunge akivuliwa uanachama wake.

Huyu bwana Job nadhani ni Dikteta zaidi kuliko yeyote kwa sasa.. eee huyo mwingine anaweza kuwa na 2.

Maana yeye anaamini kishamuapisha mtu basi hadi afe ama hilo bunge lifike kikomo.
 
Huu mjadala ni wa kitoto sana.

Wakati uchaguzi unaanza tulishuhudia wanachama wa CHADEMA wakilalamika kwa wakurugenzi wa uchaguzi kunyimwa fomu kwa kile kinachodaiwa kuwa wameshachukua fomu ya ubunge kwenye majimbo X. Hivyo wakurugenzi wa uchaguzi hawatoi fomu hiyo tena kwa wagombea wa CHADEMA.

Waliochukua fomu walidaiwa kuwa walifika kwenye ofisi za wakurugenzi wa uchaguzi wakiwa na barua za CHADEMA zilizogongwa mhuri wa katibu wao wa jimbo/mkoa.

Hili sakata liliwakumba wagombea kadhaa wa udiwani kupitia CHADEMA, siwakumbuki kwa majina nafikiri baadhi ya majimbo ni Ubungo na Kibamba.

Je kesi hizi ziliishaje? Wale wagombea feki walichukuliwa hatua gani ? Barua zenye mihuri ya CHADEMA walipewa na nani?

Mwishoni wagombea halali walipewa fomu kwa amri kutoka juu nafikiri. Ni NEC waliona mapungufu hayo nchi nzima au nani alitoa suluhisho sikumbuki.

Kilikuwa ni kituko kwa wakurugenzi kuwanyima fomu wagombea kwa kisingizio cha kuwa tayari mwanachama wao ameshachukua fomu tena kwa barua halali ya uteuzi kutoka kwenye chama chao wenyewe.

Sasa turudi kwenye hili. NEC wamepokea barua halali kutoka kwa Mnyika. Mnyika anasemaje? Kama anakataa, je alazimishwe kuwa aliandika? Kama barua ilikuwa feki kwa nini NEC isikubali yaishe na wakisikilize chama cha CHADEMA ili haki itendeke. Barua halali ya majina halali ipelekwe NEC. Kama CHADEMA hawataki kupeleka majina, je walazimishwe?

Kama wasipopeleka majina, Je sheria au Katiba inasemaje kuhusu hilo.

Imefikia kipindi kila chombo kifanye jukumu lake na kiache ubabaishaji. Nchi hii ina wasomi na ni aibu kuonekana kituko kwa mambo yanavyofanyika bila weledi.

Kuwa mzalendo ni pamoja na kusema ukweli sio kutetea ubabaishaji hata kama ni kwa manufaa yako.

Asalaam
Mkuu umetutendea haki mkuu ubarikiwe.Pale NEC inahusika na huu uchafuzi 100%.sijaelewa mantiki ya NEC kubishana na uongozi wa chadema kuhusu viti maalumu.Walipaswa kuwasikiliza maana ndo wenye wabunge
 
Je unaweza kuthibitisha kwamba saini ilifojiwa!? Hata hivyo, umetoka njenya wazo kuu, ambalo ni kwamba huoni kitendo cha wanachama wenu 19 kuridhia kuunga mkono juhudi, vyovyote vile, ni ishara kukataa ubabe usio na tija wa chama chako!!?
Wenye kosa ni NEC, wao migogoro ya ndani haiwahusu walipaswa kucheki na mnyika.
 
Nadhani CDM wanapaswa kuiandikia NEC barua kuijulisha kwamba hao wabunge wamepoteza sifa za kuendelea kuwa wabunge sababu wamefukuzwa chama.
Halafu NEC ndio walijulishe bunge.
Hapana mkuu, utaratibu kwa Sasa ni spika kuitaarifu tume juu ya wabunge hao kukosa sifa ya kikatiba ya kuwa na chama
 
Usisahau kuwaza pia kwamba ile "Team 19," akiwemo yule mbunge wa zamani kindakindaki wa Kawe wangeweza kuunga mkono juhudi kweli, tena kirahisi hivyo, tena haraka hivyo??? Najaribu tu kukuwazisha na hili usilisahau!? In fact, hatua ya Mr Spika ya kuwatetea inapaswa kupongezwa sana kwa sababu ya uthubutu wa akina dada hawa, dhidi ya "hujuma & rafu" (kama si kiinimacho) ambazo kidogo watendewe.
Kuwapongeza kina mdee kwa uasi ndani ya chama Chao ni kukosa uzalendo.Mwanachama yeyote anapaswa kuheshimu taratibu za vyama vyao
 
Maelezo yako ni butu, hayana mantiki kabisa. Kwa hiyo mtu akipigwa risasi akapona alafu hauzulii bungeni aachwe tu? Wakati anafanya ziara Ulaya na Usa? Kisa nini? Jikite kwenye mada toa pumba zako.
Mwambie mama yako na mapaja yake .
 
Nadhani CDM wanapaswa kuiandikia NEC barua kuijulisha kwamba hao wabunge wamepoteza sifa za kuendelea kuwa wabunge sababu wamefukuzwa chama.
Halafu NEC ndio walijulishe bunge.
Ninavyofahamu CDM wakiwavua uanchama wanatakiwa kulitaarifu Bunge na/au NEC hatimaye Spika huijulisha NEC kuhusu nafasi wazi za mbunge/wabunge kwa sifa ya kukosa chama.
Naweza kusahihishwa/kukosolewa.
Ajabu ya CCM Mpya ni kuwatetea hawa Viti Maalum ili wapate fedha za misaada.Donor county!
 
Nakunukuu:"NEC wanasema Mnyika kama katibu mkuu aliwapelekea majina tena yaliyopewa baraka na kamati kuu ya Chadema"

Sasa mkuu kama NEC wanadai ya kwamba wamepokea majina kutoka chadema yenye baraka za kamati kuu,kwani kikao cha kamati kuu kinaweza kufanyika kwa kificho?Kuna kikao cha kamati kuu cha chadema ambacho kimewahi kukaa?Si lazima taarifa zingevuja ya kwamba kuna kikao cha kamati kuu kilikaa?

Kati ya wale wabunge 19 kuna mbunge mmoja alipigiwa simu na kiongozi mkubwa wa chadema na alimwambia wamepata nafasi 19 but watachaguliwa kwa kanda because viti ni vichache sana

Hiyo ilikuwa ni 2 weeks before sakata lote kutokea so maybe chadema walikubaliana kukubali au ni kweli walipeleka
 
Back
Top Bottom