Uchaguzi 2020 Nani mkweli kati ya hawa watu? Spika, NEC au CHADEMA?

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Chadema wanasema hawakupeleka majina NEC,nani alipeleka?

NEC wanasema Mnyika kama katibu mkuu aliwapelekea majina tena yaliyopewa baraka na kamati kuu ya Chadema. Hii ni kweli au sio kweli?

Spika anadai hawezi kuvua ubunge wabunge ambao kwa mujibu wa katiba ya JMT sasa hivi hawana chama maana walishatimuliwa Chadema. Kisa tu NEC ya Wilson Mahera ilimpa majina. Ok kama NEC ilimpa majina bado wanasifa za kuwa wabunge kama ibara ya 67(b) na 71(e) inavyoweka wazi?

Au ndio kusema undavaundava tu hata kwenye mambo ya kuzingagia Katiba na sheria?

Chadema wanaweza kuupa ukweli umma wa watanzania ili tujue nani alipeleka majina? Nahisi kuna jinai inanukia, kama haipo kuna mtu mkubwa Cdm mpenda dili anahusika,Tanzania nzima inamfahamu.
 
Nakunukuu:"NEC wanasema Mnyika kama katibu mkuu aliwapelekea majina tena yaliyopewa baraka na kamati kuu ya Chadema"

Sasa mkuu kama NEC wanadai ya kwamba wamepokea majina kutoka chadema yenye baraka za kamati kuu,kwani kikao cha kamati kuu kinaweza kufanyika kwa kificho?Kuna kikao cha kamati kuu cha chadema ambacho kimewahi kukaa?Si lazima taarifa zingevuja ya kwamba kuna kikao cha kamati kuu kilikaa?
 
Tume hawakupaswa kubishana na chadema Bali kujadiliana nao, maana zile nafasi ni za chadema, Wana haki ya kupeleka watu ama lah.taarifa za ndani zinadai NEC walitoa fomu za uteuzi kwa Mara ya pili Tena kupitia kina mdee wajaze nje ya utaratibu na kufoji saini ya mnyika
 
Chadema wanasema hawakupeleka majina NEC,nani alipeleka?

NEC wanasema Mnyika kama katibu mkuu aliwapelekea majina tena yaliyopewa baraka na kamati kuu ya Chadema. Hii ni kweli au sio kweli?...
Mkuu mbona unahangaika?

Hivi ni nani mwenye uwezo wa kwenda kumtoa mahabusu na kuamuru kesi ifutwe kati ya chadema spika na neki?
Hapo unaona kabisa sio chadema isipokua kuna idara ilio nyuma ya spika
Maana wemeweza hata kuzifanyia mafekeche saini za hata ya katibu mkuu mnyika
Wakaandaa orodha ya majina na kuyapeleka neki
Lakini jua lazima spkia atakua anatoa muongozo kwenye idara fulani na muongozo unafuatwa
Huu ni usanii wa kiwango SiGarA
 
Hadi sasa, CHADEMA wanasema wanaenda mahakamani.

Spika kawashauri CHADEMA waende mahakamani.

Tume, japo hawasema, nao wanashauri CHADEMA waende mahakamani. Hata sheria pia inataka hivyo.

Kwa hiyo, CHADEMA, NEC na Spika wanaongea lugha moja kwa Sasa, na hivyo wanakubaliana kwamba Wabunge ni halali hadi happy mahakama itakaposema vinginevyo.

Yajao ndiyo hayo
 
Hakukuwa na haja ya chadema kwenda mahakamani kwa maoni yangu.chadema kwenda mahakamani wanajiingiza kwenye mtego.kesi itachukua 5 year

Hivi unadhani kwamba CHADEMA hawajui wanachokifanya?

Sidhani kama wanaingia mtegoni ila ni mbinu ya kuhakikisha kwamba hili jambo linaisha kwa Baraka za Mahakama kwamba Wabunge ni halali au la, ila uwezekano upo mkubwa sana kwamba mahakama itasema ni halali, na hatimaye mjadala kufungwa ili kuepusha 'mihimili kugongana'😀
 
Hakukuwa na haja ya chadema kwenda mahakamani kwa maoni yangu.chadema kwenda mahakamani wanajiingiza kwenye mtego.kesi itachukua 5 year
Kwa nini ichukue miaka 5? Mahakama kuu inatakiwa itoe amri, haraka tujue ukweli nani alifoji hiyo baru?
 
Hivi unadhani kwamba CHADEMA hawajui wanachokifanya?

Sidhani kama wanaingia mtegoni ila ni mbinu ya kuhakikisha kwamba hili jambo linaisha kwa Baraka za Mahakama kwamba Wabunge ni halali au la, ila uwezekano upo mkubwa sana kwamba mahakama itasema ni halali, na hatimaye mjadala kufungwa ili kuepusha 'mihimili kugongana'😀
Vipi kama ikionekana Chadema hawakupeleka majina? Uhalali utatoka wapi?
 
Jambo ambalo naamini mimi ni Chadema wamepeka majina maana Kama Chadema wangekuwa hajapeleka majina na tunavyowaaminia makamanda (Halima & wenzie) wasingekubal kwenda bungeni lakini yanaweza kuwa hayajapelekwa na Mnyika
 
Back
Top Bottom