My people, you can't be serious! Yaani kila mwanaume anaweza kuwa baba? Kila mtu anaweza kuvaa uhusika wa baba mzazi kwa mtoto? Hakuna kama MAMA, hakuna kama BABA. Their roles to children are irreplaceable. Majukumu ya mzazi wa kiume/kike huwezi kuyakasimu kwa mtu yeyote. Kuna wakati mtoto anafanya ukorofi na ukaidi kiasi kwamba kama anayemlea si mzazi wake anaweza akadhani mtoto anamdharau kwakuwa siyo mzazi wake, na hatimaye kupunguza upendo kwa mtoto. Hivi mnajua mtoto anaanza kukua na kujengeka kisaikolojia akiwa tumboni kwa mama yake? Mwanamke mjamzito asipokuwa treated vizuri na mume wake, mtoto tumboni anaathirika, hii inaonyesha kina baba tuna umuhimu mkubwa sana hata wakati wa ujauzito.
Wanaume wenzangu nadhani mmewahi ku-date wasichana wenye 'dad issues', ni wasumbufu balaa. Wengi wanakuwa diehard feminists. She will blame you for every mistake her dad did decades ago. Hii inaonyesha majukumu ya baba mzazi ni muhimu.
Kuna wakina baba wenye kasoro zao (kutelekeza familia, kukataa watoto, nk) na kina mama(kutesa watoto,kuzaa na kutupa watoto, kutelekeza) wenye kasoro vilevile.Kusema mama ni muhimu kuliko baba ni sawa na kusema kuku alitangulia ndo likafuata yai. Ni kitendawili. Naamini mtoto yeyote aliyelelewa na single parent, kuna kitu anapungukiwa, hata kwa kiasi kidogo.
Ukweli ni kwamba mtoto anakamilika akipata malezi mazuri ya baba na mama. Baba yangu uko juu, hakuna kama wewe, umenipa dira ya maisha. You have taught me how to be a man. Mama hakuna kama wewe, umenifundisha upendo na kuwaheshimu wanawake.