Nani bado anabisha kuhusu S2KIZZY kuwa ndio producer namba moja Tanzania?

Kwa hii list huyo s2kzyy ni ka producer ka 2000 hakajakaa chini na kupambanua ngoma alizopiga mika mwamba yani kwa hizo banger za Mika jamaa itabidi afunge bakuli maana mika ndio katoa ngoma halisi za bongofleva ukiachana na wengine wakali kibao kma wakina lamar fish crab,master jay pia na nahreel kuna jamaa anaitwa duke touch wale jamaa walikua wana produce kweli sio hawa wapiga amapiano ambazo hata wahindi wanazipiga siku hizi sawa sawa useme wewe unajua english dunia nzima akati ni lugha ya dunia ongea lugha mbali mbali tukuone wewe mkalimani!!!
 
View attachment 2983488

Naona kuna watu wanaleta ubishi usio na msingi kuhusu ukubwa wa producer namba moja Tanzania S2KIZZY aka Zombie.

Lakini wote wanaobisha wanasukumwa na chuki hawana sababu ya msingi.

Ukweli ni huo Zombie ndio producer namba moja Tanzania na ni namba 2 kwa muda wote nyuma ya PFunk Majani.
Ukiangalia hii list ana amapiano 78/100 halafu anajiita best producer ever dogo amepagawa na upepo wa amapiano huyo!!! Mwambie apige nyingine beat kama la duke touch ya benpol nikikupata kama hapotei huyo
 
Watoto lazima wafanye vizuri kuliko waliowatangulia. Vijana wengi wa sasa wameshavunja rekodi nyingi tu za wakongwe. Sio kwenye muziki tu hata fields zingine rekodi zimevunjwa na vijana. Hata huko mbeleni rekodi ya s2kizy itavunjwa na vijana wengine wa wakati huo. Labda tu inaweza ikachukua sana muda endapo s2kizzy ataendelea kuwa kwenye ubora kwa miaka mingi.
 
I respect Mika ila namba hazimbebi
Mbona jigga na pac hawana number au michael Jackson ila wanabaki kuwa goats wa muda wote , na huwezi ona watu wenye number zao kma wakina drake , ed sheraan , CB na wengine kutaja respect za wakongwe DOGO s2kizzy haja respect wakongwe wa kazi wamepiga beat kali na wana uwezo mkubwa zaidi yake mfano NAHREEL ,mika hata lamar fish crab
 
Mimi nimekulia kwenye muziki, mastaa wengi uliokuwa unawasikia redio enzi unakua walikuwa wanakula ugali home ndio wanaenda kurekodi kwa majani. Huu muziki nimeushuidia toka day one so naelewa sana nachokizungumza.
Mfano staa gan?
 
Mbona jigga na pac hawana number au michael Jackson ila wanabaki kuwa goats wa muda wote , na huwezi ona watu wenye number zao kma wakina drake , ed sheraan , CB na wengine kutaja respect za wakongwe DOGO s2kizzy haja respect wakongwe wa kazi wamepiga beat kali na wana uwezo mkubwa zaidi yake mfano NAHREEL ,mika hata lamar fish crab
Tatizo la watoto wa 2000 wanaona views za YouTube ndo kila kitu, wakati youtube yenyewe imeanza 2005!
Muda huo akina Mika, Bon, Enrico, P na Mj washapika hits za kutosha!
 
Hitsong haiitaji YouTube kuwa hitsong. Nyimbo za Chino wanaman hazina namba kubwa online lakini balaa lake unalijua mtaani. Zombie ni shughuli nyingine.
Unajua ndio maana nikakuuliza maana ya hit song kwako ni ipi.

Chino amepata umaarufu kwa zali lakini si kwa ubora wa nyimbo zake. Bado chino hana hit songs. Watu wengi wanamjua chino lakini nyimbo zake hawazijui
Tofauti na hao wa kipindi hiko, nyimbo zilikua zinajulikana Ila wasanii hawajulikani
 
Ni kweli kwa sasa ndie prodyuza mkali sababu,hits za wasanii wakubwa zozote ni yeye.refer ngoma nyingi za wasanii wa WCB,wakina jaymelody,Jux,wakina chonjo kid,nak ni yeye
 
Aliyemzidi Zombie ni Majani tu. Hitsong za Zombie 2023 ni zaidi ya hits zote alizowai tengeneza Master Jay. Alafu mie nimezungumzia hitsong sijaongelea YouTube ndio maana nimemtaja majani ambae namba zake YouTube ni ndogo sana.
Zombie hana hit songs nyingi kuwazidi hao niliokutajia

Zombie anafana kazi na diamond na hii ndio sababu unamsikia na unaona hadi hizo nomination kwenye tuzo.

Ukweli usiopingika diamond ni msanii wa sasa lakini ndio GOAT kwenye muziki wetu huu, hivyo akifanya kazi kwa ukaribu na yoyote lazima aende mjini. Hata wakati diamond anafanya kazi na Sheddy clever, Sheddy clever alikua producer mkubwa sana, hata alipokua anafanya kazi na lizer, lizer alikua mkubwa sana

Ni tofauti sana na ilivyokua kwa hao kina majani, miika, master j, Ludigo, roy, n.k
Wao walimchukua msanii akiwa hata hajui key ni nn, na Wala hata kuingiza vocal tu hajui. Lakini waliweza kumtengeneza na kumfanya kuwa msanii mkubwa na hit songs za kutosha.
 
Kijana yuko vyema kwa muziki huu wa sasa tumlinganishe na vizazi vyeke labda
Hata wa sasa bado hayupo mbali sana na wengine kama abbah, moco, kimambo, lizer, troni n.k
Utofauti yeye anafanya kazi na Diamond. Diamond ni mkubwa hasa, akifanya kazi na yoyote hata uwe baunsa wake lazima uende town.

Kwenye video productions diamond alikua na Kenny, ikafikia kipindi wote tukaona Kenny ni director bora sana kuliko wote. But diamond alipoacha kufanya kazi nae tu, kenny kaanza kupotea. Hata siku diamond aache kufanya kazi na s2keezy, utaona s2keezy akipotea kabisa. Unamkumbuka Sheddy clever?
 
Kuna maproducer siku izi ???!! au maproducer wanao sample music 😇😇
Hakuna producer bongo asiyefanya sampling hajawai kutokea inaonekana unasikiliza sana naija music ndio maana unadhani sampling inafanywa miaka hii. Hujui muziki mkuu
 
Zombie hana hit songs nyingi kuwazidi hao niliokutajia

Zombie anafana kazi na diamond na hii ndio sababu unamsikia na unaona hadi hizo nomination kwenye tuzo.

Ukweli usiopingika diamond ni msanii wa sasa lakini ndio GOAT kwenye muziki wetu huu, hivyo akifanya kazi kwa ukaribu na yoyote lazima aende mjini. Hata wakati diamond anafanya kazi na Sheddy clever, Sheddy clever alikua producer mkubwa sana, hata alipokua anafanya kazi na lizer, lizer alikua mkubwa sana

Ni tofauti sana na ilivyokua kwa hao kina majani, miika, master j, Ludigo, roy, n.k
Wao walimchukua msanii akiwa hata hajui key ni nn, na Wala hata kuingiza vocal tu hajui. Lakini waliweza kumtengeneza na kumfanya kuwa msanii mkubwa na hit songs za kutosha.
S2KIZZY amefanya kazi kubwa na Nandy, Marioo, Rayvany, Lui, Weusi, Chino, Zuchu, Billnas, Darasa, Maluma etc
Lui, Chino hawakuwa wasanii wakubwa ila kwenye zama hizi ngumu za muziki Zombie kawafikisha mjini.
 
Watoto lazima wafanye vizuri kuliko waliowatangulia. Vijana wengi wa sasa wameshavunja rekodi nyingi tu za wakongwe. Sio kwenye muziki tu hata fields zingine rekodi zimevunjwa na vijana. Hata huko mbeleni rekodi ya s2kizy itavunjwa na vijana wengine wa wakati huo. Labda tu inaweza ikachukua sana muda endapo s2kizzy ataendelea kuwa kwenye ubora kwa miaka mingi.
Ni suala la wakati, lakini sio ubora. Ndio maana hata leo hii mchezaji mzembe kabisa kama Lukaku anasajiliwa kwa dau kubwa kuliko alilowahi kusajiliwa Ronaldo de lima
 
S2KIZZY amefanya kazi kubwa na Nandy, Marioo, Rayvany, Lui, Weusi, Chino, Zuchu, Billnas, Darasa, Maluma etc
Lui, Chino hawakuwa wasanii wakubwa ila kwenye zama hizi ngumu za muziki Zombie kawafikisha mjini.
Ndio nakuuliza hao lui na chino wana hit songs zipi? Na nimekueleza kitendo Cha yeye kufanya kazi kwa ukaribu na diamond, lazima utamsikia sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom