Nani anayetajwa na Mwenyekiti wa CCM Mwanza, Dkt. Diallo kwamba ana faili Hospitali ya Akili Milembe?

Huyo ni muathilika,
Kama ni jasiri angesema kipindi jiwe yupo hai.
Hana jipya!!!!!!!!!!!

Kauli yako inaviashiria vya unafiki.

Ni ani aliyethubutu kuuongelea utawala wa mwendazake alafu akaachwa hai.

Ben saa8 ni mfano mwema.
 
Dialo ana makando kando mengi sana huko Mwanza. Ni Nani asiemjua? Ni mhuni na pia ni anatuhuma nyingi tu za uovu pia. Sishangai
Aliwadhihaki wapiga kura wake 2015 wakampiga chini.
Watumishi wake wanalalamika hawalipwi mishahara.
Nimiongoni mwawatu wakwepa kodi mkubwa.
Saiz anaanza kutudanganya muhun mkubwa huyo alijua MAGUFULI anaangalia ukabila. Angekuwa shupavu angeongea wakati MAGUFULI alipokuwa hali ningempa 5.
 
hata kwenye interview ya kazi hutakiwi kimsema vibaya boss aliyepita. hawa viongozi mbona ni bogus sana. anaona anapatia kumbe ni mjinga tu.
 
hata kwenye interview ya kazi hutakiwi kimsema vibaya boss aliyepita. hawa viongozi mbona ni bogus sana. anaona anapatia kumbe ni mjinga tu.
Imeandikwa wapi usimseme aliyepita?Muache aseme ili waliopo wajirekebishe.Hiyo ya kusema marehemu hasimangwi imepitwa na wakati.
 
Una kila kiashiria cha uoga.Kuna kipindi kumnyamazia mjinga ni silaha tosha.Hivi kipindi cha Magufuli nani angeweza kumkosoa hadharani?Ni wachache na kwa taaaaaabuuuu walithubutu.Nani angetaka risasi "salasini na nane" zimpate mwilini?Think twice.😝😝😝😝
Acha uongo, mbona akina Membe,na Nape waliokuwa wanaongea.Diallo hafai kuwa Kiongozi kama ni mwoga kiasi hiki,inamaana Magufuri asinge kufa,angelifanyaje?Diallo ni fisadi tu anajulikana tokea akiwa maliasili,alikuwa wakisafirisha magogo na biashara nyingi ya magendo.magufuri aliwakomesha,nieli tungempata kichaa mwingine kama Magufuri, anayeweza kulinda na kutetea lasilimali za Watanzania
 
Acha uongo, mbona akina Membe,na Nape waliokuwa wanaongea.Diallo hafai kuwa Kiongozi kama ni mwoga kiasi hiki,inamaana Magufuri asinge kufa,angelifanyaje?Diallo ni fisadi tu anajulikana tokea akiwa maliasili,alikuwa wakisafirisha magogo na biashara nyingi ya magendo.magufuri aliwakomesha,nieli tungempata kichaa mwingine kama Magufuri, anayeweza kulinda na kutetea lasilimali za Watanzania
Uongo wangu ni upi mtumishi wa Bwana?Nimetoa mfano wa Lissu and the likes.Wengine hadi walifanya jogging wakajikuta wamevuka mipaka na hawakurudi hadi leo.Ulitaka Diallo awe msukuma wa kwanza kuwa mjinga?Kwanza hata wachawi wa kile Kijiji wangemloga.😝😝😝😝😝
 
Bado najiuliza huyo mwanasiasa aliyetajwa na Dr. Anthony Diallo kwamba alikuwa na jalada hospitali ya Mirembe ni nani?

Na kwanini mifumo ilimruhusu kugombea?

Nawasalimu kwa jina la JMT!

=========
KWA UFUPI

Mahojiano kati ya Mhe Anthony Diallo Mwenyejiti wa CCM Mkoa wa Mwanza na Mtozi Alloyce Nyanda

1. Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Biashara yetu ya Star Tv, RFA iliharibika -Diallo

2. Sie hatukulipwa na CCM, waliolipwa ni Crew iliyokuwa inatembea na vifaa kama majukwaa, walipewa hela ya kula na kubeba vifaa, ukitazama vitabu vyetu kuna hela chama hadi leo haijalipa-Diallo Mwenyekiti wa CCM

3. Mgombea wetu wa wakati ule alisema atatusaidia na alisema hadharani tena mara mbili pale Kirumba na furahisha lakini tuliambulia misukosuko

4. Awamu ya 5 iliharibu sana protocal ya Chama, viongozi wa chama walikuwa wanawekwa mstari wa nyuma kabisa gari zinakuwa mwisho hata kama ukifika unakuta mtu amekata utepe-Anthony Diallo mwenyekiti wa CCM

5. Kuna kisa kimoja kiongozi wa CCM mkoa wakati flani tumeenda kumpokea Rais alipigwa kiwiko akadondondoka, awamu ya Tano ilikuwa inazuia viongozi wa CCM hata kuingia uwanja wa ndege wanaelezwa kubaki nje -Antony Diallo Mwenyekiti wa CCM

6. Kuna siku nimemwambia waziri mkuu, hivi unajisikia raha gani kuzungukwa na mabunduki maana umezungukwa na mabunduki kama ishirini sie, tumekuchagua ila unatuogopa ki vipi? -Antony Diallo

7. Swala hapa siyo katiba, swala ni kuchagua watu makini. Unawezaje kuchagua kiongozi katika nafasi kubwa ya uongozi huku ana rekodi ya mirembe? Tuwe makini kuchagua viongozi-Anthony Diallo

8. Kama nchi tumepitia katika kiza kifupi, tumepitishwa katika Black spot hapo Nyuma, Sasa angalau watu wana raha, furaha imerejea-Dkt Anthony Diallo

9. Hata mimi Nimeshughulikiwa kidogo, wakaniacha ila nimepata msukosuko-Anthony Diallo

10. katiba siyi ya Vyama ni ya wananchi kosa tulilofanya ni kugeuza katiba kuwa vyama na kuacha wananchi hata katika lile
bunge walitawala wananchi-Dk Anthony Diallo

11. Katiba siyo Tatizo , tatizo lipo kwa watu mnachagua Rais ambae hataki kufata katiba mtanfanya nini? Kwani katiba ya sasa ilikuwa inaruhusu mtu kuwekwa ndani bila utaratibu? Lakini yamefanyika-Anthony Mwandu Diallo

12. Rais Samia nimefanya nae kazi ni Rais makini na jasiri ni muumini wa utawala wa bora-Anthony Diallo

13. CCM tulijua haitashinda mwaka 2015 na wananchi wamegeuka wiki mbili tu baada ya kuamua hata kuunda makundi ya vijana kwenye maeneo mbali mbali waweke Star Tv ilibidi itumike nguvu

15. Kuna mambo hatukuweza kuyasema kwa sababu mfumo uliharibika kabisa. Tuliamua kunyamaza tuliamua ku play safe mode ili kesho uendelee kuishi na watoto wako.


View attachment 1849193
By default Ni Jiwe
 
A.D katoa ya moyoni na lazima hisia zake ziheshimiwa.Tatizo kuna watu wanataka watu waseme uongo kwa marehemu ili kumpamba wakati ukweli unafahamika .Kwa mujibu wa imani yangu najua marehemu aliyo yafanya hawezi kupona na adhabu za kaburini na siku ya kiyama.Sasa hivi yupo anaogelea virungu huko.Namsapoti AD 100%

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
huyu kichaa sisi tunamwitaji sana , watoto wanasoma bure, kajenga zahati 7000 nchi nzima, kajenga mashule nchi nzima, watoto wetu wanakaa kwenye Madawati, wakina mama wanazalia kwenye vitanda, kuchaa kajenga meli maziwa yote , kajenga viwanda 200 vikubwa kasambaza umeme vijijini, kajenga reli ya umeme, kichaa huyu tunamhitaji kajenga bwawa la nyerere, kajenga barabara nchi nzima, kajenga barabara za juu ubungo tulikuwa tunakaa masaa 6 kuingia mjini kichaa huyu tunamhitaji kanunua ndege wakina mbowe wanapanda kwenda kumzika profesa bukoba, kajenga masoko makubwa dodoma , morogoro, kajenga stendi kubwa ya mabasi Afrika mashariki, tunamwitaji sana kichaa wa aina, wafanyakazi hewa wanao lipwa bila kufanya kazi kawaondoa tunamwitaji sana kichaa wa aina hii, aliye punguza wizi na rushwa na kuleta nidhamu kazini kichaa wa aina hii watanzania tuna mpenda sana tunamhitaji sana, alie kuwa anatumbua wazembe ,kichaa alie wafanya majambazi waache ujambazi wawe raia wema tunahitaji sana, kichaa alie tuomba tuombe Mungu kwa kufunga na kuomba corona ikatoeka tanzania. Tunakuhitaji sana. Mungu Kukumbuke umeweka Historia na Alama ktk taifa letu. kuna wa kufuta Mema yako .
 
Back
Top Bottom