Nani anayetajwa na Mwenyekiti wa CCM Mwanza, Dkt. Diallo kwamba ana faili Hospitali ya Akili Milembe?

Kama ni kweli tuliongozwa na mtu ambaye mirembe wana kumbukumbu naye kwenye mafaili ya afya ya akili, basi mtanzania anaweza kuishi nchi yoyote duniani.
 
Dialo mnafiq kama wengine...NEC yao 2020 ilimpitisha huyo kichaa kwa asilimia 100% sikusikia hata kura iliyoharibika.!!

na kura zilikuwa za siri.?
 
Kuna watu walizoea sana maisha ya ujanja ujanja na wizi wizi...Yule jamaa aliwapiga pin sana lazima wamchukie tu....Watanzani mlitaka rais mkali na dictator mnaanza kulia kulia..

Hii nchi usipokuwa mgumu kama JPM mambo meeengi lazima yakugomee kuanzia kwenye uchumi, siasa, utamaduni na kila mahala..Lile Jamaa lilikuwa na maamuzi haijalishi mabaya au mazuri wakati wengine hiyo kuamua tu ni shida.

Dola lazima iogopwe na iheshiwe na watu wote, JPM aliipa dola heshima na michezo ya kipumbavu dhidi ya dola ikafa au kupungua....Watu kama Manji, Mo hawa waarabu na wahindi walikuwa wakiichezea hii nchi watakavyo na mpaka kuidharau dola wao na wajukuu zao..

JPM pamoja na mambo yake ambayo inaonekana wengine walikereka lakini alikuwa ni Rais aliyepaswa kuiongoza hii nchi kwa miaka zaidi ya 20....Kuteka, kuua ni moja pia ya kazi ya dola kwa wajinga wote wanaoweza kuhatarisha uhai na misingi ya nchi gizani huku mbele ya wananchi wanajiita wema...tutambue ni serikali pekee dunia inayoweza kujua mipango ya gizani ya kila raia wake..

RIP JPM.....tulitofautiana mitazamo kwenye mambo fulani lakini yapo mengi pia uliifanyia hii nchi na kufundisha watu hii nchi inataka kiongozi aina gani..
Kwahiyo huyu ndio alikuwa na file mirembe???????????
 
Mataga tulishatoa tamko kwamba TLS ni mgonjwa wa akili mkapinga ona Sasa Leo hii imethibitika kwamba alikua na file Milembe haya Sasa Chadema mjitafakari kumbe hata

Jiwe alikua mzima wa afya kabisa na alikua na akili timamu na mbaka Leo anaongoza nchi Kwa kishindo

Ni El mamvi tu ndio alikua mgonjwa tungempa nchi angefia Ikulu!

(In Bia yetu voices)

Nadanganya wadau?
Hivi huyu bia yetu nae AMEENDA ZAKE?(
 
Katika hali ya halisi ukiambiwa umechafua hali ya hewa ina maana umejamba. Kisiasa itakua umeongea jambo la kuwaudhi watu wengi kwenye siasa.

Wenye kumbukumbu watakumbuka enzi ya awamu ya nne iliyokuwa na kashfa nyingi za ufisadi hadi rushwa kuonekana kama ndio njia sahihi kufanikisha kila jambo Anton Dialo alistaajabisha watu kwa tukio moja. Enzi za awamu ya nne ilisemekana alimshitaki waziri wa maliasili enzi hizo kwa JK kwa kutoweza kumpa kitalu cha uwindaji baada ya kumpa dola za kimarekani kiasi fulani. Kuonesha jinsi rushwa ilikua kitu cha kawaida kwa wakubwa kufuatana na Dialo JK alimuamuru waziri huyo kumrudishia Dialo hela zake. Hakuna ushahidi kama JK aliwachukulia hatua yoyote vigogo hao.

Huyo Dialo enzi hiyo ya awamu ya nne alijilimbikizia vyeti feki hadi vya Phd huku kuna shaka ya yeye kufika japo kidato cha nne. Kuna mwandishi mmoja aliandika kitabu kuwaorodhesha watu mashuhuri wenye vyeti feki ambapo Anton Dialo ni mmoja wapo.

Kutokana na hila na kujilimbikizia sifa za uongo Anton Dialo ambaye pia ni mfanya biashara mkubwa akaweza kufikia kua naibu waziri.
Kwa ukweli kauli zake za kinafiki dhidi ya magufuli zimewaudhi wengi. Huyu ni mmojawapo ya watu wamekua wanasitiriwa ndani ya ccm kwa sababu ni mmoja ya wale waliyoigeuza ccm kama kampuni yao binafsi enzi za awamu wa nne.
Unakili dhahiri ccm imepoteza uhalali wa kuendelea kuaminiwa, Kama inalea wala rushwa na watu waliogushi. Hivyo chama hiki ambacho kinashikilia dola hakitatufikisha popote sababu ni kichafu.
 
Hivi huyu bia yetu nae AMEENDA ZAKE?(
Najua basi toka mtu pori jiwe apumzishwe chattle mabatini
Sijamuona humu Tena sijui ndio alikua concubine wa mwendakuzimu maana Kwa taarifa za chini chini kapata stroke maana hakuamini Kama jamaa atadanja ghafla na kumwacha mjane yatima!
😂😂😂😂
 
Mama samia na kamati kuu ya ccm wasimfumbie macho huyu Diallo.
Leo atamtukana kiongozi aliyepita kwa matusi km haya ila kesho napo atamtukana mama atakapostaafu.
Watu km hawa hawafai kuwa wenyeviti wa vitongoji.
Eti mwenyekiti wa ccm mkooa
Nani hajui uchafu wake??

Huku nikujipendekeza kishamba.
Kwani kosa lake liko wapi? Mwacheni aseme anachokijua, mnataka kumulisha maneno ya kusema?. Hata Kama aliyesemwa alikuwa na file mirembe, kuugua anaugua mwanadamu yeyote after all kila binadamu ana wazimu. Hayupo binadamu aliye timamu, sema tunatofautiana tu kiwango Cha wendawazimu mwenzetu kilizidi akafunguliwa file Mirembe, Kuna maajabu hapo?! Povu kwa Diallo la nini? Acha ushamba.
 
Angeanza na kulipa wafanyakazi wake. Katapeli benki nyingi pale Mwanza halafu anataka kuelekeza lawama kwa marehemu.
Marehemu nae aliwahi kukosea hakuna binadamu aliyekamilika ndiyo maana yatupasa kujifunza kutokana na makosa yake. Musiwe na wax flexibility Kama mishumaa.
 
Kwani kosa lake liko wapi? Mwacheni aseme anachokijua, mnataka kumulisha maneno ya kusema?. Hata Kama aliyesemwa alikuwa na file mirembe, kuugua anaugua mwanadamu yeyote after all kila binadamu ana wazimu. Hayupo binadamu aliye timamu, sema tunatofautiana tu kiwango Cha wendawazimu mwenzetu kilizidi akafunguliwa file Mirembe, Kuna maajabu hapo?! Povu kwa Diallo la nini? Acha ushamba.
Hawa mataga tuliokua tunawaambia kipindi kile jiwe ni mgonjwa wa akili na anatumia dawa za kupunguza wendawazimu walikua wanapinga sana na wakati ushahidi ulikuwepo wa wazi kabisa
Ilikua haiwezekani mtu anasema maendeleo hayana chama ila akifika kwenye Jimbo la mpinzani anasema hataleta maendeleo sababu wamechagua upinzani!

Kwa mwenye akili timamu lazima angejua tu yule jamaa dishi limeyumba kabisa!

Mataga vipi Bado mtaendelea kutuita sisi vibaraka wa mabeberu?

Haya na huyo Diallo naye katumwa na makondoo?
 
Bado najiuliza huyo mwanasiasa aliyetajwa na Dr. Anthony Diallo kwamba alikuwa na jalada hospitali ya Mirembe ni nani?

Na kwanini mifumo ilimruhusu kugombea?

Nawasalimu kwa jina la JMT!

=========
KWA UFUPI

Mahojiano kati ya Mhe Anthony Diallo Mwenyejiti wa CCM Mkoa wa Mwanza na Mtozi Alloyce Nyanda

1. Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Biashara yetu ya Star Tv, RFA iliharibika -Diallo

2. Sie hatukulipwa na CCM, waliolipwa ni Crew iliyokuwa inatembea na vifaa kama majukwaa, walipewa hela ya kula na kubeba vifaa, ukitazama vitabu vyetu kuna hela chama hadi leo haijalipa-Diallo Mwenyekiti wa CCM

3. Mgombea wetu wa wakati ule alisema atatusaidia na alisema hadharani tena mara mbili pale Kirumba na furahisha lakini tuliambulia misukosuko

4. Awamu ya 5 iliharibu sana protocal ya Chama, viongozi wa chama walikuwa wanawekwa mstari wa nyuma kabisa gari zinakuwa mwisho hata kama ukifika unakuta mtu amekata utepe-Anthony Diallo mwenyekiti wa CCM

5. Kuna kisa kimoja kiongozi wa CCM mkoa wakati flani tumeenda kumpokea Rais alipigwa kiwiko akadondondoka, awamu ya Tano ilikuwa inazuia viongozi wa CCM hata kuingia uwanja wa ndege wanaelezwa kubaki nje -Antony Diallo Mwenyekiti wa CCM

6. Kuna siku nimemwambia waziri mkuu, hivi unajisikia raha gani kuzungukwa na mabunduki maana umezungukwa na mabunduki kama ishirini sie, tumekuchagua ila unatuogopa ki vipi? -Antony Diallo

7. Swala hapa siyo katiba, swala ni kuchagua watu makini. Unawezaje kuchagua kiongozi katika nafasi kubwa ya uongozi huku ana rekodi ya mirembe? Tuwe makini kuchagua viongozi-Anthony Diallo

8. Kama nchi tumepitia katika kiza kifupi, tumepitishwa katika Black spot hapo Nyuma, Sasa angalau watu wana raha, furaha imerejea-Dkt Anthony Diallo

9. Hata mimi Nimeshughulikiwa kidogo, wakaniacha ila nimepata msukosuko-Anthony Diallo

10. katiba siyi ya Vyama ni ya wananchi kosa tulilofanya ni kugeuza katiba kuwa vyama na kuacha wananchi hata katika lile
bunge walitawala wananchi-Dk Anthony Diallo

11. Katiba siyo Tatizo , tatizo lipo kwa watu mnachagua Rais ambae hataki kufata katiba mtanfanya nini? Kwani katiba ya sasa ilikuwa inaruhusu mtu kuwekwa ndani bila utaratibu? Lakini yamefanyika-Anthony Mwandu Diallo

12. Rais Samia nimefanya nae kazi ni Rais makini na jasiri ni muumini wa utawala wa bora-Anthony Diallo

13. CCM tulijua haitashinda mwaka 2015 na wananchi wamegeuka wiki mbili tu baada ya kuamua hata kuunda makundi ya vijana kwenye maeneo mbali mbali waweke Star Tv ilibidi itumike nguvu

15. Kuna mambo hatukuweza kuyasema kwa sababu mfumo uliharibika kabisa. Tuliamua kunyamaza tuliamua ku play safe mode ili kesho uendelee kuishi na watoto wako.

View attachment 1849193
Unataka kusema alikuwa kichaa,mjomba ally mpanduji
 
Kuna watu walizoea sana maisha ya ujanja ujanja na wizi wizi...Yule jamaa aliwapiga pin sana lazima wamchukie tu....Watanzani mlitaka rais mkali na dictator mnaanza kulia kulia..

Hii nchi usipokuwa mgumu kama JPM mambo meeengi lazima yakugomee kuanzia kwenye uchumi, siasa, utamaduni na kila mahala..Lile Jamaa lilikuwa na maamuzi haijalishi mabaya au mazuri wakati wengine hiyo kuamua tu ni shida.

Dola lazima iogopwe na iheshiwe na watu wote, JPM aliipa dola heshima na michezo ya kipumbavu dhidi ya dola ikafa au kupungua....Watu kama Manji, Mo hawa waarabu na wahindi walikuwa wakiichezea hii nchi watakavyo na mpaka kuidharau dola wao na wajukuu zao..

JPM pamoja na mambo yake ambayo inaonekana wengine walikereka lakini alikuwa ni Rais aliyepaswa kuiongoza hii nchi kwa miaka zaidi ya 20....Kuteka, kuua ni moja pia ya kazi ya dola kwa wajinga wote wanaoweza kuhatarisha uhai na misingi ya nchi gizani huku mbele ya wananchi wanajiita wema...tutambue ni serikali pekee dunia inayoweza kujua mipango ya gizani ya kila raia wake..

RIP JPM.....tulitofautiana mitazamo kwenye mambo fulani lakini yapo mengi pia uliifanyia hii nchi na kufundisha watu hii nchi inataka kiongozi aina gani..

Unachekesha wewe,eti ni Serikali pekee ndiyo inayoweza kujua mipango ya gizani ya Raia wake!..Serikali ipi hiyo unaizungumzia wewe!
Kwa lipi!.acha ushabiki wa kipuuzi wewe.Watu Ndugu zetu walifungwa bila kosa lolote.JPM alikandamiza Raia kwa kuhofia kutokukubalika kwake,mtu muoga kupindukia.
Tuogope Dola kwa lipi!..hujui maana ya uhuru wewe wala huthamini Uhuru wako.Endelea kuogopa DOLA.
 
Mataga tulishatoa tamko kwamba TLS ni mgonjwa wa akili mkapinga ona Sasa Leo hii imethibitika kwamba alikua na file Milembe haya Sasa Chadema mjitafakari kumbe hata

Jiwe alikua mzima wa afya kabisa na alikua na akili timamu na mbaka Leo anaongoza nchi Kwa kishindo

Ni El mamvi tu ndio alikua mgonjwa tungempa nchi angefia Ikulu!

(In Bia yetu voices)

Nadanganya wadau?

Yeye mwenyewe betri yake ilikuwa imekaribia kuexpire na alijua hakuna tena Replacement sasa sijui CCM walimteua vipi kugombea.
 
Unachekesha wewe,eti ni Serikali pekee ndiyo inayoweza kujua mipango ya gizani ya Raia wake!..Serikali ipi hiyo unaizungumzia wewe!
Kwa lipi!.acha ushabiki wa kipuuzi wewe.Watu Ndugu zetu walifungwa bila kosa lolote.JPM alikandamiza Raia kwa kuhofia kutokukubalika kwake,mtu muoga kupindukia.
Tuogope Dola kwa lipi!..hujui maana ya uhuru wewe wala huthamini Uhuru wako.Endelea kuogopa DOLA.

unapoambiwa dola lazima iogopwe lazima uelewe nini kinaongelewa....bila shaka huelewi maana ya dola kuheshimika...na dola kutoheshimika..

Ni watanzania hawa hawa waliokuwa wanalalamikia matajiri kuonea watu, viongozi wa serikali kuonea watu, watu wenye nyadhifa kuonea watu, ndugu wa viongozi na matajiri kuonea watu na kunyanyasa watendaji wa serikali.

Ni watanzania hawa hawa walikuwa wakilalamikia dola ilivyokuwa haiheshimiwi na akina Manji na kundi lake mpaka kuwatusi mawaziri hadharani.

Watanzania hawa hawa walikuwa wakilalamikia uzembe makazini na ubwanyenye wa watendaji, vyombo vya dola viliogopa matajiri na viongozi kiasi hata cha kushindwa kutimiza majukumu, wenye nguvu ya rushwa walikuwa hawafanywi kitu.

Watanzania hawa hawa walikuwa wakilalamikia ukwepaji wa kodi na ujanjaujanja wa wafanyabiashara na serikali kupoteza mapato yake.......TUNAPOSEMA KUOGOPWA NA KUHESHIMIKA KWA DOLA NI PAMOJA NA WATU KUISHI NA KUFUATA SHERIA INAVYOTAKA...
 
Back
Top Bottom