Nani anastahili tuzo ya Nobel katika marais 6 tuliowahi kuwa nao Tanzania?

Mbetewa,
Kuna haki za binadamu kisiasa, haki za binadamu kijamii, haki za binadamu kiuchumi, ni kundi lipi unaongelea ili tupate maarifa mkuu.
Magufuli alipigana dhidi ya kero kwa wananchi, akawanyima "haki za binadamu" wale waliokuwa wanaishi kwa kutumia kero hizo!
 
Tuzo za za Nobel ziko nyingi, wewe unaongelea Tuzo gani?
Ya Amani?
Ya Fasihi?
Ya Biolojia/madawa?
Ya Physics ?
Ya Kemia?
Ya Sayansi ya Uchumi?
Tuzo ya kimataifa ya Nobel iliyoanzishwa na Bw Alfred Bernhard Nobel, Mswidi mbobezi wa kemia, uhandisi, mvumbuzi, mjasiriamali na mdiakonia (matendo ya huruma (philanthropist)) imetoa tuzo hiyo kwa Wanafizikia watatu kwa mpigo.

Swali:
Katika safu ya marais 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unadhani nani kati yao angeweza kustahili tuzo hiyo maarufu?

Kwa sababu zipi?

Kwanini imeshindikana?

Afrika Kusini wana Laureate 3, Liberia 2, DR Congo 1, Ethiopia 1, Kenya 1, Tanzania tumekwama wapi na juhudi zote nzuri za #AMANI YA NCHI, #ULINZI WA AMANI YA DUNIA, #UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA, #MIUNDOMBINU BORA, #MUUNGANO WA PEKEE DUNIANI, #OAU, #KUANZISHWA KWA NON ALIGNED MOVEMENT, #SOUTH SOUTH COMMISSION, #SADC, #EAC, na mengine mengi mazuri kimataifa. Ni Mwl. Nyerere ndiye aliingiza China kwenye kundi la mataifa yenye kura ya turufu katika Umoja wa Mataifa. Aidha alikuwa mmoja wa washauri wa Malkia wa Uingereza lakini hata tuzo ya heshima ya juu Uingereza ya "Sir" hakuwahi kuipewa. Naomba nikope maneno ya Paulo Mtume aliyeuliza hivi "Enyi Wagalatia mmerogwa na nani? Wagalatia.3:1"

Yote hayo na mengine mengi mazuri ya Tz bado Kamati ya Nobel haizioni tu?

Angalizo:
Changia mawazo yako kwa kutuonyesha hekima na busara zako ili tufaidike na maarifa yako, usichangie jazba za kuonyesha kejeli, dharau na matusi, utakuwa umetunyima maarifa yako.
 
Big Ben aliokoa taulo la Tz kudondoka mbele ya wakwe (Breton woods) kwa kulipa madeni na kurejesha uhusiano.
Tuzo za za Nobel ziko nyingi, wewe unaongelea Tuzo gani?
Ya Amani?
Ya Fasihi?
Ya Biolojia/madawa?
Ya Physics ?
Ya Kemia?
Ya Sayansi ya Uchumi?
 
Nobel hutolewa kwa mtu aliye hai tu. Leo hii Nyerere ana vigezo vya kuipata lakini anakosa sifa kwa vile hayuko hai. Mawazo ya Nyerere ya wakati huo yalikuwa hayakubaili nchi za Magharabi; lakini leo hii yanakubalika wakati yeye mwenyewe hayupo kuyazungumzia. Hasa hili swala la uhuru na kujitegemea!
Tuzo za za Nobel ziko nyingi, wewe unaongelea Tuzo gani?
Ya Amani?
Ya Fasihi?
Ya Biolojia/madawa?
Ya Physics ?
Ya Kemia?
Ya Sayansi ya Uchumi?
 
Mh Kikwete hii tuzo anachukua mwaka 2024 kila kitu kipo kwenye makaratasi

Secret zone
Tuzo za za Nobel ziko sita, unaongelea tuzo gani?

1.Ya Amani?
2.Ya Fasihi?
3.Ya Biolojia/madawa?
4. Ya Physics ?
5. Ya Kemia?
6. Ya Sayansi ya Uchumi?
 
Kikwete alikosa ya MO atapata ya NOBEL?? Magufuli angeendela kuishi hadi kumaliza kipindi chake, alikuwa na nafasi kubwa sana kwenye tuzo ya MO.
Tuzo za za Nobel ziko sita, unaongelea tuzo gani?

1.Ya Amani?
2.Ya Fasihi?
3.Ya Biolojia/madawa?
4. Ya Physics ?
5. Ya Kemia?
6. Ya Sayansi ya Uchumi?
 
Ila pia, sina hakika kama Tuzo hii ni ya nchi za Magharibi au ya jumuiya za kimataifa, Alfred B. Nobel ni Mswedish ambayo ni nchi iliyokuwa rafiki wa Tz wakati huo wa mawazo hayo ya Mwl Nyerere yaliyopingwa na Magharibi yalipokuwa yakitoka.

“Having come into contact with a civilization which has over-emphasized the freedom of the inpidual, we are in fact faced with one of the big problems of Africa in the modern world. Our problem is just this: how to get the benefits of European society – benefits that have been brought about by an organization based upon the inpidual — and yet retain African’s own structure of society in which the inpidual is a member of a kind of fellowship.”

Julius Kambarage Nyerere as quoted in the New York Times Magazine on 27 March 1960. -
Tuzo za za Nobel ziko sita, unaongelea tuzo gani ya Nobel?

1.Ya Amani?
2.Ya Fasihi?
3.Ya Biolojia/madawa?
4. Ya Physics ?
5. Ya Kemia?
6. Ya Sayansi ya Uchumi?
 
Tuzo za za Nobel ziko sita, unaongelea tuzo gani ya Nobel?

1.Ya Amani?
2.Ya Fasihi?
3.Ya Biolojia/madawa?
4. Ya Physics ?
5. Ya Kemia?
6. Ya Sayansi ya Uchumi
Umenikumbusha wakati anakabidhiwa nchi na mzee ruksa,Hali ilikuwa mbaya sana.lakini Big Beni akafanya Mambo makubwa
1.kuanzisha TRA
2.shetia ya TISS 1996
3.ete,etc
 
Tuzo za za Nobel ziko sita, unaongelea tuzo gani ya Nobel?

1.Ya Amani?
2.Ya Fasihi?
3.Ya Biolojia/madawa?
4. Ya Physics ?
5. Ya Kemia?
6. Ya Sayansi ya Uchumi?
Mama Samia Suluhu Hassan 100%
 
Tuzo za za Nobel ziko sita, unaongelea tuzo gani ya Nobel?

1.Ya Amani?
2.Ya Fasihi?
3.Ya Biolojia/madawa?
4. Ya Physics ?
5. Ya Kemia?
6. Ya Sayansi ya Uchumi?
Yawezekana kilichomkwamisha Mwl kutopewa tuzo ya Nobel ni uamuzi wake binafsi wa kuipiga Uganda, kung'oa na kupandikiza uongozi 1979, uamuzi ambao aliuchukuwa baada ya Jumuiya za Kimataifa kumkalia kimya hata alipoziandikia barua kwamba nchi yake imevamiwa hivyo wachukuwe hatua kumuagiza adui aondoke kwa amani. Kimya cha Jumuiya za Kimataifa huenda kilichukuliwa na Mwl kama muhuri na saini ya Jumuiya hizo kwamba jitetee/jihami, ilhali baada ya uamuzi huo wa Mwl, Jumuiya hizo zikaja kupiga kelele baada ya kuona uwezo wa kivita wa Tz kwamba Mwl ameenda hadi chumbani kwa adui kinyume na mila na desturi za Jumuiya za Kimataifa ambazo Tz iliziridhia kwa kuwa mwanachama. Yawezekana Jumuiya za Kimataifa zilidharau Tz kwamba haina silaha za kumdhibiti adui hivyo Mwl angesurrender na hivyo kusingekuwa na vita au vita vingehamia kwenye meza-mduara za Jumuiya hizo kutafuta suluhu (ambayo huenda Mwl alistukia janja hiyo kwamba labda Jumuiya hizo zilitaka kumpa adui mkoa wa Ziwa Magharibi sasa Kagera), kumbe wasijuwe kwamba yawezekana kweli Mwl hakuwa na silaha lakini kumbe alikuwa na ujuzi, akili na utaalam wa silaha za adui na zile ambazo adui hana na kwamba falsafa ya vita ya Mwl ilikuwa ni stratejia ya kumpiga adui kwa kutumia silaha zake mwenyewe kwa asilimia kubwa. "Vamia, teka, chukuwa, shambulia, songambele" Yawezekana Jumuiya za Kimataifa zilitumia sababu hii kumuona Mwl kwamba hastahili tuzo ya Nobel, kwamba ni mvamizi kama adui alivyokuwa mvamizi pia (Balance of Perspective).

Hiyo ya Mwl ni tofauti na JK ambaye alivamia Anjuan, akang'oa na akakabidhi kwa Comoros KWA KIBALI CHA JUMUIYA ZA KIMATAIFA akiwemo mkoloni Mfaransa.
 
Tuzo za za Nobel ziko sita, unaongelea tuzo gani ya Nobel?

1.Ya Amani?
2.Ya Fasihi?
3.Ya Biolojia/madawa?
4. Ya Physics ?
5. Ya Kemia?
6. Ya Sayansi ya Uchumi?
Katika waliokua wana stahili ni mwalimu nyerere, lakini kwangu mwenye na kustahili zaidi ni Benjamin Wiliam mkapa!
Sababu ziko nyingi sana, lakini yule mzee ndie amejenga structure ya nchi yetu, na tutaenda na vision yake kwa kipindi kirefu sana.

Hata atokee nani ajaribu kubadilisha muundo aliyounda mkapa atashindwa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuzo za za Nobel ziko sita, unaongelea tuzo gani ya Nobel?

1.Ya Amani?
2.Ya Fasihi?
3.Ya Biolojia/madawa?
4. Ya Physics ?
5. Ya Kemia?
6. Ya Sayansi ya Uchumi?
Ali Hassan Mwinyi Baba wa demokrasia. Aliondoa mifumo ya kijamaa na kuweka hii ya kisasa..
 
Tuzo za za Nobel ziko sita, unaongelea tuzo gani ya Nobel?

1.Ya Amani?
2.Ya Fasihi?
3.Ya Biolojia/madawa?
4. Ya Physics ?
5. Ya Kemia?
6. Ya Sayansi ya Uchumi
Nyerere hata kumfikiria wasingemfikiria kwa politics zake za kijamaa ingawaje naamini alikuwa kiongozi mzuri,kwa hawa wazungu ujamaa sio mbaya tuu,ujamaa is considered evil na hawana compromise na hilo, nakumbuka i was in states when Mwalimu passed away, nikaona in one newspaper wameandika Julius Nyerere a long time dictator .......nilishangaa sana na sikuamini nilichoona siku hiyo
 
Back
Top Bottom