Rais Samia atakuwa Rais wa pili mwanamke Barani Afrika kushinda Tuzo ya Nobel

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,272
9,716
Ndugu zangu Watanzania,

Tunzeni hili andiko, shikeni haya maneno, kamateni haya maandishi kuwa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan atakuwa na kuingia katika historia ya kuwa Rais wa pili mwanamke Barani Afrika kuchukua na kushinda Tuzo ya Nobel baada ya Rais mstaafu wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf kuwa Rais wa kwanza mwanamke Barani Afrika kushinda Tuzo hii ya juu na ya heshima kabisa Duniani kwote, ambayo ilianza kutolewa miaka 122 iliyopita yaani mwaka 1901.

Ambapo kwa sasa zaidi ya watu elfu moja wameshapokea na kushinda Tuzo hiyo na mwaka huu tukishuhudia mwanaharakati kutoka Iran, Narges Mohammad na ambaye anatumikia kifungo chake akishinda tuzo hii.

Ikumbukwe ya kuwa Tuzo hii hutolewa kwa mtu binafsi, kikundi, Taasisi au shirika kwa kutambua mchango wake katika kuleta matokeo chanya katika jamii na Dunia nzima kwa ujumla. Watu kama akina Nelson Mandela, Dr Martin Luther King junior, Barack Obama ni miongoni mwao watu waliowahi kushinda Tuzo hii ya Aman.

Rais wa Liberia alishinda Tuzo hii kutokana na suala la Amani pamoja na kumpigania mwanamke kupata haki na kushiriki katika uongozi, japo Tuzo hii aligawana na wenzake wawili ambapo mmoja ni kutoka libelia na mwanaharakati kutoka Yemen.

Tukirejea kwa Rais samia unaona Anastahili kabisa kushinda Tuzo hii ya heshima kutokana na mapinduzi makubwa aliyoyafanya katika kila secta na kurejesha ndoto na matumaini kwa baadhi ya watu ambao walikuwa wamekata Tamaa ya maisha.

Mfano katika Elimu Tumeona Rais samia akihakikisha kuwa mtoto wa kike anapata Elimu bila shida ya aina yoyote ile,tuliona kuna mabinti walikuwa wamekatishwa masomo kutokana na changamoto mbalimbali zilizowakabili lakini alipoingia madarakani akatoa nafasi ya pili kwa mabinti wengi kupata Elimu na kutimiza ndoto za kupata Elimu.

Na ikumbukwe kuwa ukimpatia au kumuelimisha mtoto wa kike unakuwa umeielimisha familia nzima,jamii na Taifa zima kwa ujumla wake.

Tumeona Rais samia katika kuwapunguzia vikwazo na vishawishi watoto wa kike ametoa fedha za kutosha kuhakikisha kuwa mabweni yanajengwa ya kutosha ili wasome kwa utulivu na amani, jambo ambalo tumeona likileta matokeo chanya kwa watoto wengi wa kike kupenda shule na kuongeza ufaulu na kufanya vizuri katika masomo.

Sasa je hamuoni hili ni jambo linalohitaji pongezi sana kutoka kwa kila mtu mwenye kutambua umuhimu wa Elimu hasa kwa mtoto wa kike? Kwa ufupi ni kuwa Rais samia amemuondolea mtoto wa kike vikwazo vya kupata elimu kwa kumuwekea mazingira mazuri na yenye kuleta hamasa katika kusoma na kujifunza.

Rais samia huyo huyo kwa ujasiri wake Tumeona akipanda mbegu ya amani katika Taifa letu na mioyo ya watanzania, kwanza amekuwa ni mtu wa haki, kwa kutenda haki na kuhubiri haki wakati wote.

Tumeshuhudia akiviasa vyombo vyetu vya usalama hasa jeshi la polisi kuwatendea haki Watanzania, pasipo kuonea watu hadi akafikia kuunda tume ya haki jinai ili kuangalia namna bora ya kuboresha sheria zetu katika kuhakikisha kuwa haki inatendeka kwa watanzania wawapo katika mikono ya vyombo vyetu vya usalama hususani jeshi la polisi.

Ni yeye Rais samia amekuwa akikemea habari za kumkamata mtu kwa uonezi au pasipo kuwa na ushahidi au kuwabambikia watu kesi kwa uonevu tu.

Tumeona Rais samia akipambana na kufanya juhudi za kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendeshwa kwa kuzingatia misingi ya kidemokrasia na utawala bora yenye kuzingatia sheria na katiba yetu. Ndio maana tumeona kwa sasa watu wanazungumza kwa uhuru bila hofu wala wasiwasi wa aina yoyote ile.

Ndio maana vyombo vya habari vinaandika habari bila hofu na vinatoa na kuchapisha habari bila shida. Leo siyo jambo la ajabu kuona CCM na CHADEMA wakikaa mezani kuzungumzia mustakabali wa Taifa letu kidemokrasia, siyo ajabu kuona viongozi wetu wakila chakula meza moja huku wakitabasamu na kushikana mikono na kupiga picha ya pamoja mwisho wa mazungumzo.

Hii yote ni kazi ya Rais Samia ni akili na maono ya Rais Samia, ni uvumilivu na ustahimilivu wa kiuongozi wa Rais Samia. Ni hekima busara na uzalendo wa Rais Samia katika kulitanguliza mbele Taifa letu na maslahi ya Taifa letu.

Ni ushujaa na ujasiri wa Rais Samia katika kujenga umoja wa kitaifa, kwa kuwa wapo wasiopenda juhudi hizi za Rais Samia, wapo waliotaka tuishi kwa matabaka, wapo waliopenda tuishi kwa kuogopana, wapo waliotaka tuishi kwa visasi, chuki, vinyongo, maumivu, majeraha na machozi katika mioyo yetu.

Jambo ambalo Rais Samia Amelikataa kutokana na kuwa na hofu ya Mungu na kutambua kuwa uongozi na vyote vya Duniani ni vya kupita na hivyo yatupasa kuishi kwa kupendana na kuwa na matendo mema yenye huruma na kuhurumiana na kusaidiana kama Taifa badala ya kukwamishana sisi kwa sisi.

Embu niambieni ndugu zangu ni vipi na kipi kinachoweza kumnyima Rais amia Tuzo hii ya amani, kosa gani alilolifanya kwetu Watanzania mpaka tuseme hastahili? Kipi ambacho alikifanya Ellen Johnson Rais wa Liberia ambacho Rais samia hajafanya?

Mbona amefanya zaidi ya hao wote? Hatujaona akiwasamehe watu wengi waliofungwa kipindi cha nyuma na uchaguzi ili watoke na tuanze mwanzo mpya wa kujenga Taifa letu? Hatujaona akija na R 4?

Hatujaona akiwarudisha watu kutoka uhamishoni na kuwahakikishia usalama wao mpaka muda huu? Nani amedhurika au kujeruhiwa wakati wa Rais Samia? Nani amepoteza maisha mikononi mwa serikali ya Rais Samia pasipo hatua za kiupelelezi kufanyika na haki kutendeka?

Vyombo vingapi vya habari vimefunguliwa kutoka kifungoni? Nani amefanya haya yote kama siyo mpendwa wetu Rais samia? Afanye nini mama yetu na Rais wetu tutambue dhamira yake njema kwa Taifa letu.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Labda tuzo ya Dr.Mo Ibrahim ya Distinguish leadership of Africa na sio tuzo ya Nobel.

Tuzo ya Nobel inapewa watu wenye mchango mahsusi sana Duniani au Kwa jamii yake.
 
Huyu huyu ambae amempeleka TAMISEMI mkwe wake ili wahakikishe wanakwapua ushindi na kufanya uchafuzi baadala ya uchaguzi?!!

Huyu huyu ambae utawala wake umewazuia CHADEMA kwenda Ngorongoro na hata kamati ya bunge la Ulaya inayohusika na mambo ya Afrika?!!

Aendelee tu kukusanya Phd fake,bora hata wakina Babu Tale na Msukuma wananunua kwa hela zao kuliko anaegawa rasrimali!!
 
Dingilai Mwashambwa unaupiga mwingi. Mama amefanya makubwa ikiwamo maridhiano na Mbowe. BAWACHA ni mashahidi kwa jinsi wanavyomkubali mama.
Bawacha wanamkubali sana Rais samia ndio maana uliona walivyorukaruka sana siku ile amekwenda kuzungumza nao siku ya wanawake.wameahidi kumpa kura za ndio kwa kishindo uchaguzi ujao.
 
Binafsi namuona Mwabukusi ndiyo anastahili hii tuzo ya Nobel. Samia Kuna masuala 2 yamemharibia:

1. Kuwahamishia wamasai Ngorongoro.

2. Kushindwa kuunda katiba mpya ili kuruhusu demokrasia kuchukua mkondo wake.

3. Kuwauzia waarabu bandari.
 
Tuzo hiyo ataipewa kwa lipi aliloitendea dunia au Tanzania?

Nyerere mwenyewe aliisikia kwemye redio.

Jalafu mbona wewe mwasha mbwa unaweka namba ya simu?

Wenzio wanateuliwa sio kwa kiweka namba bali hutumia njia za hirizi, ushirikina na uchawi. Acha kuweka simu nenda kwamzmsisi, ukirudi hukai mwezi unapewa ukuu wa mifugo aina ya nguruwe kakonko vijijini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom