Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
- Thread starter
- #161
Wana JF,Tuzo za za Nobel ziko sita, unaongelea tuzo gani ya Nobel?
1.Ya Amani?
2.Ya Fasihi?
3.Ya Biolojia/madawa?
4. Ya Physics ?
5. Ya Kemia?
6. Ya Sayansi ya Uchumi?
Mimi nafikiri pale tutakapotambua umuhimu wa Sayansi na Teknolojia na kuvitengea bajeti nono ili kuibua na kukuza ubunifu ndipo kama taifa tuanze kuota ndoto ya tuzo hii kutinga Tz, otherwise kama Mtanzania akitokea kuipata basi lazima atakuwa Mwanadiaspora au aliye naturalize nje ya Tz. Hapa Tz siasa inachukuwa rasilimalifedha na rasilimaliwatu wengi kuliko maelezo. Leo hii Wahandisi wabobezi wanahamia kwenye siasa, Madaktari bingwa wanahamia kwenye siasa, Wachumi nguli wanakimbilia siasa, Wakulima mahiri wanaishia kwenye siasa, Maaskari waandamizi wanahamia kwenye siasa (Leo hii Pensheni ya Mwalimu wa Shule ya Msingi aliyestaafu 30.06.1997 kwa hiari katika umri wa miaka 55 inalingana kabisa na Pensheni ya Brigadier General). Tz imewekeza muda, rasilimaliwatu na rasilimalifedha kwa kiwango kikubwa kwenye Siasa kuliko kwenye Sayansi na Teknolojia, tuzo itapatikanaje? Ukiangalia hata kwenye Mifuko ya Pensheni wakati haijaunganishwa kuwa mbili tu, tulikuwa na Mifuko takriban 12 na kila moja ilianzishwa kwa sheria ya Bunge (Act of Parliament) kwamba walikuwa hawataki kuwa wamoja, lakini katika hiyo 12 ni Mfuko wa Pensheni ya Wanasiasa ndiyo ulikuwa unalipa Pensheni nono sana kuliko Mifuko yote, hii ilifanya wataalam ambao wangetuletea Tuzo ya Nobel kutelekeza taaluma na career zao kukimbilia siasa ili wawe wanachama wa Mfuko huo ili wanapostaafu wawe na Pensheni nono.