Nani anastahili tuzo ya Nobel katika marais 6 tuliowahi kuwa nao Tanzania?

Mama Samia Suluhu Hassan 100%

1. Wananchi, wamekubali tozo, lini na wapi watanzania walitangaza kuikubali tozo?

2. Tanzania Kuna vibrant democracy, mbowe kabambikiwa kesi, wakimbizi wakisiasa kibao

3. Walobambikwa makesi wamejaa mahabusu

4. Hakuna uhuru wa habari

5. Hakuna uhuru wa kujumuika, kupashana habari na kuelimisha

6. Hakuna vyama vya siasa kufanya siasa

7. Uhuru wa mavazi hususani ya kikatiba hakuna

Nk
 
Ally Hassan Mwinyi

1. Mshauri wa hovyo kuliko wote, hajawahi kuwakemea wavunja katiba wote ikiwemo Magufuli na mkapa

2. Huyu ndiye aliyempigia debe mwanaye ashinde zanzibar kwa nguvu za Dola

3. Alifungulia majizi ya madini na Mali asili kumbuka enzi ya kifo cha katabalo na mbuga ya lolyondo

4. Unafiki mwingi, watu wanapotea, wanapigwa risasi, wanabambikiwa makesi, nk yupo tuliii hovyohovyo kabisa

Huyu mzee hajawahi kuinua ulimi wake kukemea uovu, mnafiki sana kwa ccm yake. Nimbinafsi Kwake na watoto wake.
 
Nobel hutolewa kwa mtu aliye hai tu. Leo hii Nyerere ana vigezo vya kuipata lakini anakosa sifa kwa vile hayuko hai. Mawazo ya Nyerere ya wakati huo yalikuwa hayakubaili nchi za Magharabi; lakini leo hii yanakubalika wakati yeye mwenyewe hayupo kuyazungumzia. Hasa hili swala la uhuru na kujitegemea!
Tatizo alikuwa ni mwizi wa kura,huu ni uchaguzi mkuu wa mwaka 1995😁😁😁
 
Mie ningeigawa katikati kwa Mkapa na Kikwete! Namkubali Nyerere lakini utawala wake sikuushuhudia sana! Mkapa na Kikwete kila mmoja ana mengi mazuri ya kukumbukwa kwa wananchi, Sera nzuri za kiuchumi za Mzee wa Lupaso zilifanya tufutiwe madeni yaliyokuwa mzigo mkubwa na kikwazo cha maendeleo yetu, Mkapa pia alifungua milango mingi ya ajira na kuleta nafuu ya maisha! Kikwete aliboresha sana maisha ya wananchi, Alisaidia sana kuondoa vikwazo vingi vilivyokuwepo kwa wananchi kupata elimu ya juu, ambapo mambo ya urasimu kupitia multriculation yaliondolewa vyuoni, vyuo vya elimu ya juu vingi vilianzishwa! Alitoa mikopo mpaka kwa wanafunzi hewa! Aliajiri kila mwaka na kuna makundi waliingia ajirani moja kwa moja toka vyuoni, adha za kusota vijiweni bila ajira walizipata wachache mno! Alipandisha madaraja na mishahara kila mwaka na zaidi alilipa hadi watumishi hewa, na bado mtaani fedha ilicheza vizuri! Kwa hakika hawa wawili natoa 50/50 ! Mh. Samia Suluhu sio rais mstaafu hivyo hatuwezi kumjaji kwa pamoja na hawa wastaafu, yeye tutamjaji baada ya kumaliza muda wake!
Mkuu umenikumbusha mbali, enzi zetu hizo za matriculation, hujaufaulu hata kama umefaulu NECTA hujadahiliwa kuingia chuo kikuu, kilikuwa kigezo cha kuwakamata wale walioiba mitihani ya NECTA. Enzi hizo zikirudi leo sijui itakuwaje.
 
Baada ya Amin kunyakua madaraka nchini Uganda mwaka 1971, kulikuwa kukitokea "frequent border incursions" kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda zikifanywa na majeshi ya Obote yaliyokimbilia Tanzania mara tu baada ya Obote kupinduliwa na Amin, majeshi hayo ya Obote yalikuwa pale Tabora.

Hili lilikuwa likifanyika kwa siri sana na hata mwaka 1978 kabla ya vita pia hayo majeshi ya Obote yalifanya tena uvamizi nchini Uganda na kisha kukimbia na kurejea tena Tanzania. Kimsingi, Amin alikuwa sahihi kwani yeye alichokuwa anafanya ilikuwa ni kujaribu kukomesha uvamizi wa mara kwa mara ktk ardhi yake.

Huu ndio ukweli ambao umekuwa ukifichwa sana na tawala mbalimbali za Tanzania japo ndio chimbuko la vita vyenyewe
Duh! hii mpya kabisa!

Najaribu kutafuta connection kuona inakaaje kwa kutumia case study ya Afrika Kusini ambapo Mandela na Desmond Tutu walipewa tuzo hii licha ya kikundi cha Mandela na Tutu kuwa na makambi ya kujifunza vita vya ukombozi Tanzania (kambi 3), Zambia (Kambi 1) ambapo wapiganaji walipewa mafunzo na kurejea Afrika Kusini kwa siri kufanya incursions ambapo vita hii ilishindwa kuleta ukombozi hadi tu pale Rais Frederik Willem de Klerk (Kaburu) alipoamua kuwatoa akina Mandela jela na kuruhusu kuanza mchakato wa kumaliza ubaguzi wa rangi. Sasa connection inanigomea hivi:-

1. Mwl. Nyerere ali-play central role kwa 90% katika ukombozi kuliko Askofu Tutu na Mandela aliyekuwa jela. Mwl. Nyerere ndiye aliyeiondoa serikali ya Makaburu kwenye Jumuiya ya Madola. Lakini tuzo wakaja kupewa Tutu na Mandela Mwl. Nyerere asiipewe hata baada ya kutoa ground kwa uMkhonto we Sizwe (MK) huku APLA cha akina Letlapa Mphahle ikiendesha vita nyumbani Afrika Kusini Transvaal.

2. Rais Frederik Willem de Klerk ambaye baada ya jitihada za ANC ya akina Oliva Tambo na Yusuf Dadoo, SAUF, SACP, SASO, AAM, SACTU, ARM ya akina John Lange, Monty Berman na Myrtle Berman, PAC ya akina Nana Mahomo na Peter Molotsi (kutaja lakini kwa uchache) kushindwa kuleta ukombozi akaamua kufungua ukurasa mpya wa ukombozi na kuiponya Afrika Kusini hakupewa tuzo hiyo wakapewa akina Chief Albert Luthuli, Bishop Desmond Tutu na Nelson Rhohlilala Madiba Mandela. Tanzania tumelogwa na nani? Mwl. Nyerere na Rais Frederik Willem de Klerk walikosea wapi?

Baghosha! Nobel Prize.
 
Unadhani wanapewapewa tu, ninyi endeleeni kula tozo za wananchi zinawatosha. Mambo ya Nobel Prize msahau.. 😋😋😋😋😋😋😋hayo waachieni wasomi wanaojielewa.
 
Kikwete alikosa ya MO atapata ya NOBEL?? Magufuli angeendela kuishi hadi kumaliza kipindi chake, alikuwa na nafasi kubwa sana kwenye tuzo ya MO.
Duh....? Nikuite jina gani wewe Boya? Tuzo ya MO hupewa ma Dikteta? muuaji Magufuli apewe Tuzo ya MO kwa sababu ya kujenga AIRPORT Chato?kwa sababu ya kununua ndege?kwa sababu ya kuagiza Tundu Lissu auawe na kumpoteza Ben Saanane? Kwa sababu ya kukandamiza Demokrasia Tanzania? mpumbavu sana wewe jamaa....
 
Duh....? Nikuite jina gani wewe Boya? Tuzo ya MO hupewa ma Dikteta? muuaji Magufuli apewe Tuzo ya MO kwa sababu ya kujenga AIRPORT Chato?kwa sababu ya kununua ndege?kwa sababu ya kuagiza Tundu Lissu auawe na kumpoteza Ben Saanane? Kwa sababu ya kukandamiza Demokrasia Tanzania? mpumbavu sana wewe jamaa....
Wewe ni pimbi tu asiyejua mambo ya dunia ndiyo maana unakimbilia kusema Magufuli diktetea ilihali dunia yote inajua kuwa alichaguliwa na wanachi kwa mujibu wa katiba kama wewe pimbi hukukubali matokeo hayo. Unaonekana huna busara kabisa ndiyo maana huwezi kukaa kwenye panel kama ya MO foundation. Tuzo ile hupewa rais aliyestaafu kwa mujibu wa katiba na katika kipindi cha utawala wake alikuwa na impact katika kuendeleza ustawi wa maisha ya watu wa nchi yake kwa kuimarisha fursa za maendeleo kiuchumi kwa watu wake, pamoja na kupunguza rushwa na matumizi mabaya ya raslimali za nchi. Magufuli aliyaweza sana hayo. Piga kelele, rukia darini (kama nyumba unayolala ina dari) au kimbilia chooni, ukweli huo huwezi kuufuta. Ni kweli upinzani wote haukufurahia utawala wake kwa vile aliwanyima talking points, na wale wote waliokuwa wakiishia kwa kufuja mali za umma aliwabana sana lakini sasa hivi tuongee tangible things siyo hadithi za alinacha zitokanazo na hasira binafsi.

Kama alikunyima mwanya wa rushwa au mwanya wa kufuja mali ya umma, usimlaumu kuwa ni dikteta, huo ndio ulikuwa wajibu wake. Kama alikunyima talking points za kisiasa, usimlaumu kwa ni dikteta, ulitakiwa utafute points mpya za kupambana naye kisiasa. Wengi wa wanaomlaumu Magufuli, kama wewe ni kwa sababu mliishi kwa mazowewa mabaya sana. MO foundation haingalii masalhi yenu bali inaangalia masalahi ya taifa.
 
Nobel hutolewa kwa mtu aliye hai tu. Leo hii Nyerere ana vigezo vya kuipata lakini anakosa sifa kwa vile hayuko hai. Mawazo ya Nyerere ya wakati huo yalikuwa hayakubaili nchi za Magharabi; lakini leo hii yanakubalika wakati yeye mwenyewe hayupo kuyazungumzia. Hasa hili swala la uhuru na kujitegemea!
Kuna kiumbe mmoja alijifanya kuiga kichwa kichwa akaishia kuwa kama story ya chura ile ya zamani. In fact don't hunt something you can't kill.
 
Kikwete alikosa ya MO atapata ya NOBEL?? Magufuli angeendela kuishi hadi kumaliza kipindi chake, alikuwa na nafasi kubwa sana kwenye tuzo ya MO.
Umenikera, jiwe mtu asiye na maarifa na muuaji/mtesi /katili/Sadist apewe hizo tuzo?
 
Umenikera, jiwe mtu asiye na maarifa na muuaji/mtesi /katili/Sadist apewe hizo tuzo?
Vigezo unavyotumia wewe na jinsi unavyovitafsisri siyo ambavyo MO inavyotumia. Magufuli asingewza kuwemo kwenye Nobel kwa vile hakuwa na impact pana zaidi ya nyumbani ingawa aliongelewa sana kimataifa. Impact ya Nyerere ilisikika Afrika yote; Kikwete yeye alikuwa mla nchi tu, hakuwa na impact yoyote popote pale. Hakuna nchi yoyote duniani utakakokuta watu wanamuongelea Kikwete au kitu chochote cha kumbukumbu ya Kikwete. Nyerere anakumbukuwa sehemu nyingi sana Afrika, hata sehemu usizoaomini kama Mali wana mtaa unaitwa Nyerere, na Magufuli anajulikana dunia nzima.
 
Tuzo ya kimataifa ya Nobel iliyoanzishwa na Bw Alfred Bernhard Nobel, Mswidi mbobezi wa kemia, uhandisi, mvumbuzi, mjasiriamali na mdiakonia (matendo ya huruma (philanthropist)) imetoa tuzo hiyo kwa Wanafizikia watatu kwa mpigo.

Swali:
Katika safu ya marais 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unadhani nani kati yao angeweza kustahili tuzo hiyo maarufu?

Kwa sababu zipi?

Kwanini imeshindikana?

Afrika Kusini wana Laureate 3, Liberia 2, DR Congo 1, Ethiopia 1, Kenya 1, Tanzania tumekwama wapi na juhudi zote nzuri za #AMANI YA NCHI, #ULINZI WA AMANI YA DUNIA, #UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA, #MIUNDOMBINU BORA, #MUUNGANO WA PEKEE DUNIANI, #OAU, #KUANZISHWA KWA NON ALIGNED MOVEMENT, #SOUTH SOUTH COMMISSION, #SADC, #EAC, na mengine mengi mazuri kimataifa. Ni Mwl. Nyerere ndiye aliingiza China kwenye kundi la mataifa yenye kura ya turufu katika Umoja wa Mataifa. Aidha alikuwa mmoja wa washauri wa Malkia wa Uingereza lakini hata tuzo ya heshima ya juu Uingereza ya "Sir" hakuwahi kuipewa. Naomba nikope maneno ya Paulo Mtume aliyeuliza hivi "Enyi Wagalatia mmerogwa na nani? Wagalatia.3:1"

Yote hayo na mengine mengi mazuri ya Tz bado Kamati ya Nobel haizioni tu?

Angalizo:
Changia mawazo yako kwa kutuonyesha hekima na busara zako ili tufaidike na maarifa yako, usichangie jazba za kuonyesha kejeli, dharau na matusi, utakuwa umetunyima maarifa yako.
Hakuni
 
Back
Top Bottom