DRC: Mama Janeth Magufuli atunukiwa tuzo ya heshima ya M.T. Kasalu

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Mama Janeth Magufuli ametunukiwa tuzo DRC, tuzo ambayo hutolewa kwa wake wa viongozi wakuu na watu maarufu duniani.

Tuzo hiyo ijulikanayo kama M. T. Kasalu aliyotunukiwa ni katika kutambua mchango wake kwa Taifa la Tanzania.

Tuzo ya M.T. Kasalu hutolewa na taasisi ya Martha Tshisekedi Kasalu.

======

Mama Janeth Magufuli, Mjane wa aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Hayati John Pombe Magufuli ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Kimataifa toleo la tatu, inayotolewa na taasisi ya Martha Tshisekedi Kasalu maarufu M. T. Kasalu, kutambua mchango wake kwa Taifa la Tanzania na kwa Hayati Rais Magufuli akiwa Rais wa Awamu ya Tano wakati akitekeleza majukumu yake Kitaifa na Kimataifa.

Aidha, Tuzo hii hutolewa kwa Wenza "spouses' wa Viongozi Wakuu wa Nchi na watu Maarufu duniani kwa kutambua michango yao kwa Wenza wao, jamii na Taifa husika.

Tuzo hii ifahamikayo zaidi kama M. T. Kasalu, Femme D'Honneur Trophee, ilitolewa jana Ijumaa tarehe 24 Machi, 2023 katika hoteli ya Pullman jijini Kinshasa.

Waandaaji wa Tuzo hii ni Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Urithi ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakishirikiana na Taasisi ya Lizadeel.

Kwa mwaka huu waliopokea tuzo hii ya M. T. Kasalu, toleo la 3 ni;

1. Mama Janeth MAGUFULI - Tanzania - mchango wake kwa Rais wa Awamu ya Tano unafahamika Afrika na duniani kote.

2. Mama Suzanne MUKAY - Congo Mke wa Daktari maarufu nchini DRC, wa magonjwa ya kina Mama na kansa, mumewe ameisaidia jamii kwenye nyanja hizo.

3. Mama Vivianne DALO - Mke wa Mchungaji Maarufu na anayeheshimika nchini DRC, Pastor Roland Dalo. Amesaidia jamii hasa wajane, yatima na vijana katika kujitegemea.

4. Mama Colette SENGHOR mke wa Rais wa kwanza wa Senegal, Mhe. Leopold Sedar Senghor , aliisaidia Senegal kupata Uhuru.

5. Mama Coretta KING mke wa Martin Luther King, USA. Mumewe alisaidia mengi ikiwemo kupinga ubaguzi wa rangi USA.

IMG_20230325_131023_909.jpg
IMG_20230325_131023_922.jpg

IMG_20230325_131023_662.jpg
 
Mama Janeth Magufuli, Mjane wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania Hayati John Magufuli ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Kimataifa toleo la 3, inayotolewa na Taasisi ya Martha Tshisekedi Kasalu kwa kutambua mchango wake kwa Taifa la Tanzania na kwa Hayati Magufuli akiwa Rais wakati akitekeleza majukumu yake Kitaifa na Kimataifa.

Tuzo hizi za M. T. Kasalu ambazo hutolewa kwa Wenza wa Viongozi Wakuu wa Nchi na Watu Maarufu Duniani kwa kutambua michango yao kwa Wenza wao, Jamii na Taifa husika, zimetolewa jana Ijumaa March 24, 2023 katika Hoteli ya Pullman Jijini Kinshasa ambapo Waandaaji wa Tuzo ni Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Urithi ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wakishirikiana na Taasisi ya Lizadeel.

Kwa mwaka huu waliopokea Tuzo hizo ni Mama Janeth Magufuli, Mama Suzanne Mukay, Mke wa Daktari maarufu nchini DRC, wa magonjwa ya kina Mama na kansa, Mama Vivianne Dalo, Mke wa Mchungaji Maarufu na anayeheshimika DRC, Pastor Roland Dalo.

Wengne ni Mama Colette SENGHOR, Mke wa Rais wa kwanza wa Senegal, Leopold Senghor ambaye aliisaidia Senegal kupata Uhuru. A Mama Coretta KING Mke wa Martin Luther King ambaye Mumewe alisaidia mengi ikiwemo kupinga ubaguzi wa rangi USA.
#MillardAyoUPDATES
Tutamkumbuka daima Rais JPM kwa kazi zake nzuri alizofanya hapa duniani.
 
Angepewa mume wa mama yetu kipenzi aliyeleta amani,utulivu na utengamano baada ya vita mbaya yachinichini ambapo watu walifungwa,waliporwa pesa na biashara,walitekwa,walipigwa risasi walitoroka nchi,walikandamizwa kuongea,walilalamika vyuma vimekaza,walibaguliwa kimiradi yamaendeleo, walitishwa wasipomchagua yeye na awatakae atawanyima maendeleo nk. nk.
 
Mama Janeth Magufuli, Mjane wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania Hayati John Magufuli ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Kimataifa toleo la 3, inayotolewa na Taasisi ya Martha Tshisekedi Kasalu kwa kutambua mchango wake kwa Taifa la Tanzania na kwa Hayati Magufuli akiwa Rais wakati akitekeleza majukumu yake Kitaifa na Kimataifa.

Tuzo hizi za M. T. Kasalu ambazo hutolewa kwa Wenza wa Viongozi Wakuu wa Nchi na Watu Maarufu Duniani kwa kutambua michango yao kwa Wenza wao, Jamii na Taifa husika, zimetolewa jana Ijumaa March 24, 2023 katika Hoteli ya Pullman Jijini Kinshasa ambapo Waandaaji wa Tuzo ni Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Urithi ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wakishirikiana na Taasisi ya Lizadeel.

Kwa mwaka huu waliopokea Tuzo hizo ni Mama Janeth Magufuli, Mama Suzanne Mukay, Mke wa Daktari maarufu nchini DRC, wa magonjwa ya kina Mama na kansa, Mama Vivianne Dalo, Mke wa Mchungaji Maarufu na anayeheshimika DRC, Pastor Roland Dalo.

Wengne ni Mama Colette SENGHOR, Mke wa Rais wa kwanza wa Senegal, Leopold Senghor ambaye aliisaidia Senegal kupata Uhuru. A Mama Coretta KING Mke wa Martin Luther King ambaye Mumewe alisaidia mengi ikiwemo kupinga ubaguzi wa rangi USA.
#MillardAyoUPDATES
FB_IMG_1679759089526.jpg
 
Back
Top Bottom