Nani anasema nyumba za shirika la nyumba ni za watu wa kima cha chini?

Nahisi kuna wizi hapo, hii serikali haiaminiki ndo maana hata walipogawa neti watu tulifikiria mara mbili je ni kweli serikali inatupenda watanzania au kuna kitu,

Toka lini serikali ya kitanzania ikapenda wananchi yake iwakopeshe nyumba kwa bei nafuu, hilo ni Bomu linakuja kulipuka,,,,

UKIONA MANYOYA UJUE KALIWA NA UKIJIONA UMEKULA UJUWE UMELIWA, this is Danganyika na presdaa ni John Mtembezi aka mzee wa Trip
 
Pamoja na interest kuwa juu kiasi hicho bado naamini kuna unafuu na faida kubwa kununua nyumba kwa kutumia hii mikopo ingawaje mabenki na NHC hawajaweza kuwaelewesha wateja wake;
  • Je hii nyumba ambayo mteja atainunua kwa mil 25 itakuwa na dhamani gani baada ya kumaliza mkopo i.e kama equity > interest rate basi ni uwekezaji mzuri kwenye ununuzi wa hizi nyumba
  • Fikiria kwa mtu ambaye anapanga na analipa kodi ya nyumba kati ya 300,000/= to 500,000/=...hiii kodi inamnufaisha land lord na kwa mpangaji ni pesa inayopotea, lakini kwenye mkopo wa nyumba marejesho unayofanya inakua ni pesa yako mwenyewe maana baada ya kumaliza mkopo nyumba inakuwa ni mali yako na imepanda thamani yaani kutoka 25mil na kuwa hata zaidi ya 65mil ulizorejesha.
  • Faida nyingine ya ununuzi wa nyumba kwa mkopo ni njia mbadala ya kuweka akiba ya uzeeni..Mifuko ya penseni imeshindwa kukidhi mahitaji ya wastaafu wengi na ununuzi wa nyumba kwa mkopo ni ukombozi kwani wakati wa uzeeni baada ya kumaliza mkopo unaweza kupangisha hii nyumba na kulamba kodi ya kuendesha maisha ya uzeeni vinginevyo unauza na kupata cash ya matanuzi.

Splendid!
 
Mkifanya mchango ukoo wenu mka-raise hiyo ela cash NHC watatoa apartment?

Nadhani kama nyumba zitawadodea, labda watapokea huo "mchango" wako, lakini kwa shingo upande. Mahesabu yanayoambatana na huo mkopo kama kwenye origino uzi inaonyesha interest pekee karibia mara tatu ya mkopo, kwa hiyo mchango wako hautakuwa na faida yoyote kwao, watasubiri mwenye kuingia mkenge...
 
Benki ndio inakula interest siyo NHC.
 
Benki ndio inakula interest siyo NHC.

Nimekuelewa, provided tu, kama unazo, unaweza kununua moja kwa moja from NHC. Kwa bei ya mil 25 basi sio mbaya sana kwani kama mahesabu ya kukodi nyumba elsewhere ni laki 3 hadi 5, basi, ni bonge la offer.... yaani, ni cheap...
 
Nadhani kama nyumba zitawadodea, labda watapokea huo "mchango" wako, lakini kwa shingo upande. Mahesabu yanayoambatana na huo mkopo kama kwenye origino uzi inaonyesha interest pekee karibia mara tatu ya mkopo, kwa hiyo mchango wako hautakuwa na faida yoyote kwao, watasubiri mwenye kuingia mkenge...
Kama benki ndio waliweka hela zao kwene basket ya ujenzi wa hizo nyumba, nadhani cash is not an option. Kama ni NHC wamejenga kwa pesa yao nadhani ni haki yetu watz kulipa hata kwa cash na kuchukua hizo apartments.
 
itabidi waweke vigezo vya kuzuia wale matajiri wa kutupa kutoweza nunua hizi nyumba alafu waje kutuuzia milioni miamoja kama wafanyavyo sasa baada ya miaka mitatu
 
Ni investment nzuri hasa kama utaitumia wakati unaendelea kulipa mkopo aidha kukodisha au mwenyewe ikiwezekana ijilipe yenyewe kwa Not less than 40% of installment, vinginevyo riba ni kubwa sana ni kwa vile watanzania waliowengi hatuna financial discipline kama utaangalia opportunity cost ya longterm investment/project kwa 19% continually kwa hiyo installment unaweza kukuta hiyo nyumba umeinunua ghali sana.
-Aidha ni bora kununua cash,
Kwani kwa inflation ya 10-13% leo ni sh25 mln baada ya miaka 15 yaweza kuwa shs 130 mln hadi 180 mln
---na Present Value of cash flow ya sh 400,000 kila mwezi x180 ni shs 36 mln hadi 40 mln same inflation.
KWA MAONI YANGU DECISION FACTOR MUHIMU NI DEMAND YA MATUMIZI YA HIYO NYUMBA KWA KIPINDI HICHO NA FINACIAL POSITION YAKO
 
kama unaweza kununua kiwanja chako,USINUNUE nyumba za NHC.
watanzani tumeshazoea kuhamia nyumba semi finished,unamalizia nyumba ukiwa unaishi humo humo after 5 years nyumba imeshakamilika ,kuna bustani na vikuku.nchi za ulaya e.g UK hawaruhusu mtu kujijengea nyumba na kuna sheria nyingi za kukuzuia.lakini kwa bongo 80% ya Ardhi haijawa surveyed so ni uwezo wako tu kujenga then unaanza kufanya survey na taratibu za kuhalalisha umiliki.
nyumba za NHC zenye thamani ni zile za mjini TU,upanga, na city centers mikoani,unachukua halafu unatafuta mpangaji atakayelipa pesa ya kutosha mkopo na visent vya kubakia kwa ajili ya ada za watoto etc.
ukichukua nyumba ya mkopo alafu ukaishi humo humo inakula kwako.
 
Nimeipenda sentensi yako ya mwisho ni kweli ukikopa nyumba hizi it makes sense upangishe na ijilipie yenyewe huo mkopo.

Mkifanya mchango ukoo wenu mka-raise hiyo ela cash NHC watatoa apartment?
Kama kweli wana nia ya kusaidia watu kuwe na options kadhaa:
1.kwa wanaoweza walipe cash 25m kwisha kazi,
2.kuna wanaoweza kulipa kwa muda mfupi chini ya mika 5 nao wapunguziwe riba,
3.wanaobaki ndio wawe na option hii ya miaka 15.
 
itabidi waweke vigezo vya kuzuia wale matajiri wa kutupa kutoweza nunua hizi nyumba alafu waje kutuuzia milioni miamoja kama wafanyavyo sasa baada ya miaka mitatu

Mkuu ndiyo ubepari huo unless kama kuna special favors za serikali ndani katika ujenzi wa nyumba hizo itawapa uhalali kuwawekea hizo protections.
 
Nimeipenda sentensi yako ya mwisho ni kweli ukikopa nyumba hizi it makes sense upangishe na ijilipie yenyewe huo mkopo.

Kama kweli wana nia ya kusaidia watu kuwe na options kadhaa:
1.kwa wanaoweza walipe cash 25m kwisha kazi,
2.kuna wanaoweza kulipa kwa muda mfupi chini ya mika 5 nao wapunguziwe riba,
3.wanaobaki ndio wawe na option hii ya miaka 15.

Mkuu that is how it works, ukilipa taslim hakuna hiyo riba. Ukilipa say in 2 years unaweza kukuta unalipa say 30mln. All in all kwa mikopo ya nyumba ilitakiwa iwe in a tune of less than 10%, sasa sema hiyo hela yetu nayo haiko stable kabisa. Lakini pia kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu it's far much better kuliko kulipa the same amount au 70% ya kulipa pango. Lakini pia ni opportunity kwani unaanza kuitumia nyumba hiyo immediately tofauti na nyumba nyingi unakuta mtu anaijenga taratibu for more than 20 years, umaliziaji baada ya mafao ya kustaafu.

Kuna Basic mortgage calculator hapa (Bonyeza Hapa) ingiza hizo figures mkopo, interest na muda wa malipo utapata picha pana ukizibadilisha badiliisha say miaka au interest rate.
 
Jee, wameeleza ikiwa mtu baada ya miaka fulani, tuseme 10, ameshindwa kabisa kulipa watachukua hatua gani?
 
Hizo nyumba za NHC kwa milioni 25 ziko wapi? Navyojua kwa sasa NHC wana kampeni ya kuuza apartments Arusha (so-called Meru Residential Apartments) kwa $100,000 - ambapo kuna 10% downpayment, halafu 90% iliyobaki zilipwe baada ya miezi 3.
 
Ukishindwa kulipa wanachukua nyumba na unakuwa umepoteza equity yako yote, hupati hata senti.
Kwa upande mmoja bado ni nafuu, uchukulie kama hizo ulizolipa kwa mwezi kodi yako ya mwezi. Hapo kinachouma ni hiyo interest. Huko Ulaya ambako interest ni ndogo, baadhi ya nchi unapoteza na bado unalazimishwa kulipa deni lililobakia.
 
itabidi waweke vigezo vya kuzuia wale matajiri wa kutupa kutoweza nunua hizi nyumba alafu waje kutuuzia milioni miamoja kama wafanyavyo sasa baada ya miaka mitatu
wasipofanya hivyo itakuwa balaa!!! kuna watu wanaweza kununua flat yote hiyo kwa mkupuo mmoja na ma-interest yao humohumo.
 
Hizo nyumba za NHC kwa milioni 25 ziko wapi? Navyojua kwa sasa NHC wana kampeni ya kuuza apartments Arusha (so-called Meru Residential Apartments) kwa $100,000 - ambapo kuna 10% downpayment, halafu 90% iliyobaki zilipwe baada ya miezi 3.

Ukweli mkuu mie naona watu washabikia hapa wakati kitu chenyewe hakipo. ha hiyo $100,000 si afadhali nichukue mkopo wa shs 50k nijenge nyumba kwenye kiwanja ntakacho kuwa nacho na nyumba itakuwa na private playing area for my kids na big area ya kuweka hata bustani ya mboga au banda la kuku jamani.
 
Du NHC wamekubuhu! alafu sasa kwa watanznia wepi hao wakununua hizo nyumba? Jamani JK si watetee wapiga kura wake vp tena hapa?
 
Back
Top Bottom