Nani anasema nyumba za shirika la nyumba ni za watu wa kima cha chini?

Hizi labda ni kwa ajili ya mawaziri wa JK wanaozitafuna kodi zetu.
 
ni kwa wenye fedha taslim.... ukichukua mkopo wa sh mil 200 benki, baada ya miaka mitano utakuwa umekuwa na kufikia milioni 500, kwa riba ya asilimia 20
 
Wanatangaza kama formality lakini simesha uzwa siku nyingi hizo na wajanja wamesha nyaka

Wacha kudanganya watu. Uongo utakusaidia nini? ulikwenda ukakuta zimekwisha uzwa? sema huna fedha za arbuni.
 
[h=3]Mmeigeuza Tanzania nchi ya majambazi?[/h]

Mkurugenzi wa Uendeshaji Biashara wa NHC, Shambwe na Meneja Uhusiano wa NHC Sanguya wakizindua utapeli wa nyumba kuuza nyumba za Ubungo mwaka 2011..
Hakuna kitu kimetutisha na kutushangaza kama tangazo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) la kuuza nyumba maeneo ya Ilala. Ukiangalia tangazo mwanzoni ni zuri tu. Lakini ukifikia kwenye kipengee cha bei ya nyumba zinazoitwa za watu wa kawaida, unapata kichefuchefu. Bila aibu wanasema eti nyumba moja ni shilingi 168,239,748.62 tena bila VAT! Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uendeshaji Biashara, David Shambwe, hiyo ndiyo eti bei wanayoona inamfaa mwananchi wa kawaida! Ukifanya hesabu ya haraka ni kwamba ili mfanyakazi au mkulima kununua nyumba moja anapaswa kufanya kazi kwa miaka 35 akiwa anapokea mshahara wa shilingi 400,578.83 kwa mwezi. Na kama anapata kiwango hicho cha mshahara ahakikishe hatumii hata senti tano ndipo aweze kuwa na kiwango kinachotakiwa. Je ni watanzania wangapi wa kawaida wanapata mshahara kiasi hicho? Shame on you! Hivi kweli watu wa kawaida ambao karibu kwa maisha yao wengi wao walikuwa wajamaa haya mamilioni ya shilingi wayatoe wapi kama siyo kufanya ujambazi na ufisadi? Je hii ni biashara au ni aina nyingine ya wakubwa kutumia cha biashara kuhalalisha pesa yao chafu? Haiwezekani mtu wa kawaida mkulima na mfanyakazi akapata hiyo pesa bila kuwapo jinai nyuma yake. Je namna hii siyo kuigeuza Tanzania nchi ya majambazi na wauza unga? Ajabu hata serikali nayo inachekelea wakati hii ni taarifa kuwa asiyeliibia taifa au kujihusisha na biashara haramu alie tu hatapata kuwa na nyumba kwenye maeneo yaliyopimwa na yanaoyoeleweka.
 
ndo maana nasema nchi hii inahitaji ukombozi kwenye kila sector wakuu....huo ni wizi wa waziwazi kama walivyoiba tembo na twiga wetu KIA...
 
Sijui kwanini hizi nyumba wanamzungumzia watu wa kipato cha chini,sijui tabaka gani la chini lenye uwezo wa kulipa mil 168 au kazi gani wanazofanya kwa mishahara ambayo itawawezesha kulipa hiyo mikopo ya nyumba,sidhani kama wanamzungumzia mtanzania wa kawaida mimi nnaye mfahamu.Nimekosa imani na hili shirika kwa kuegemea sana watu wa kipato cha juu ambao ni wachache mno na kutoa idadi kubwa ya nyumba kwao.ooh god help us,no hope in this nation.
 
Shirika mufilisi linatapatapa, wanadhani wataokoka kwa kujiingiza kichwakichwa kwenye biashara.
Kilichonichefua kwa mpango wa maendeleo wa miaka 5 ya NHC wanalenga kujenga nyumba makaazi elfu 5 (hii ni kwa nchi nzima), cheka mwenyewe huko!
Mbaya zaidi sikumsikia Mchechu akizungumzia utafiti katika miradi ya "NYUMBA NAFUU"....
Wameshindwa hata kujifunza kutoka South Afrika na Brazil...!?

Tumepotea hii nchi.
 
Nimesoma kwenye Mwananchi ya leo ikimnukuu mkurugenzi wa maendeleo ya biashara wa NHC (Bw. David Shambwe) akisema nyumba za Mchikichini Ilala zitauzwa kila moja kwa Tsh 168.2 MIL bila Vat! I WAS SHOCKED!! No wonder kila mtu anafikiria kuiba tu!

Sote tunatambua kuwa maisha ni nyumba. Nilipo sikia na kuona NHC wanajenga nyumba za kuuza nikafurahi. Sasa furaha yangu imepotea baada ya kupata tetesi kuwa wanauza 99M VAT EXCLUSIVE!
 
Watanzania bwana! wakati mwingine huwa nashindwa kabisa kujua tuna matatizo gani, hivi kweli huwazi kujenga nyumba nyumba nzuri ya kawaida ukaishi confortable kwa 40M? Ukitaka kiwanja cha bei mbaya (beach plot and others) lazima vitakugharimu lakini vya bei ya kawaida kulingana na uwezo wako pia vipo vingi tuu.


Nyumba gani hizo miln 40?
Inflation inazidi kuongezeka..cost of living inakuwa juu..40m ni bei ya kiwanja..
 
Fani yangu ni ujenzi..najenga sana na nawajengea watu nyumba zao..
Nyumba haijengwi tu kwa mabati na matofali.. Kupandisha nyumba tu siyo kazi kubwa sana..complications zipo kwenye finishing

Rejao!

Kila biashara , siasa, ubishi, na mengine mengi ni fani yako. Wewe ni mtu wa namna gani?

Au ndiyo ile kitu ya malipo kadri unavyo bisha?

Pole.
 
Wacha kudanganya watu. Uongo utakusaidia nini? ulikwenda ukakuta zimekwisha uzwa? sema huna fedha za arbuni.

Ni kweli nyumba za Arusha walinunua matajiri wa jumla! I.e mtu mmoja ananunua the entire flat.bottom line is - NHC wamechemsha katika hili! Hii ni kampuni la Serikali so nilakwetu-wananchi.
Hivyo basi pamoja na kuwa make Pesa another objetive is to lift us from peverty!

Kwa hili la Arusha sijui kama mtu atasema both objectives were met! Na kama hakukuwa na another best alternative
 
wewe unaonesha hujawahi kujenga kumbe..

mwenzio leo nimenunua mabati 70 na bati moja nimenunua 13,000=
piga mahesabu hapi

tofali moja sh 800 na nyumba ya vyumba vitatu wastani matofali 1500

piga mahesabu hapo...hata milioni kumi hap hatufiki...

mwenzio najenga as we speak....wait and see

Maneno mengi si mali, jenga na kama ni kweli basi biashara umeipata ili mradi iwe nyumba ya kuonekana.
 
Back
Top Bottom