Nani amemdanganya Mkuu wa Kaya?

Nani amemdanganya Mkuu wa Kaya?

..
Mkuu umefanya analysis nzuri lakini hukumalizia ndio maana utapata critism nyingi. ungefanya kitu kimoja ungekata mzizi wa fitna

moja ungeafanya cost analysis kwa abiria mmoja ndege ikiwa imejaa (fully capacity), ikiwa na abiria (50% capacity) na ikiwa na abiria 25% inakuaje. hii itamaliza kabisa fitna yeyote

..mimi nilifikiri alitakiwa alinganishe ndege zenye ukubwa unaolingana.

..inawezekana na yeye amekosea kwasababu anamjibu mtu aliyefanya utafiti wenye makosa tayari.

..labda nitoe mfano wa magari na wanapotoa viwango vya fuel consumption.

..huwezi kukuta wamelinganisha toyota corolla na bmw 7 series. Corolla inatakiwa ipambanishwe na honda civic, vw jetta au magari mengine ya "class" hiyo.

..kwa hiyo nilitegemea mtoa mada alinganishe ndege ya Magufuli na ndege zingine za "class" hiyo. Washauri wa Raisi nao walipaswa kufanya hivyo.
 
Wewe mdau mleta mada kias flan hauko sawa.kama trip moja ya Bomberdier ni abiria 75, kwenda na kurudi si abiria 150? Na ili upate hao 450 itahitaj trip 3. Au mwenzetu ulichukulia inarud na ruban tu bila abiria wala chochote? Au hiyo 1 million sio return trip?
Ambapo kwa hizo Boeing Si ndio watakuwa 900 kwa kwenda Na kurudi?, swali ulilomaliza nalo ndio jibu!.
 
Awali ya yote nichukue fursa hii kumpongeza Mkuu wa Kaya yetu kwa moyo wake wa kizalendo wa kutuletea ndege mbili mpya ili kufufua shirika letu ambalo wenzie walilitafuna na kulifilisi. Japo haohao ndio wanaomshangilia kama vile waliofilisi shirika hilo siyo wao.

Mkuu wa Kaya umedanganywa kuhusu gharama za usafiri wa ndege Dar to Songea. Amesema kuwa ndege za kawaida zinaweza kutumia mafuta ya milioni 28 kutoka Dar to Songea lakini ndege mpya za Bombadier Q400 zitatumia mafuta ya milioni 1 tu. Mimi sio mtaalamu wa ndege lakini taarifa imenifanya kufanya utafiti kidogo

Katika kajiutafiti kangu nimegundua kiwango cha mafuta ya ndege kwa safari hakipo constant. Kinatofautiana kutokana na sababu anuai, kama vile aina ya ndege, umbali wa safari, uzito wa mzigo wa kwenye cabin, kimo kutoka usawa wa bahari, namna ya kupaa. Vyote hivi huchangia utofauti wa utumiaji wa mafuta ktk ndege.

Katika hayo tuchukue moja la aina ya ndege na hayo mengi yawe constant (under ceteris peribus). Mkuu wa Kaya amesema "ndege nyingine" zitatumia mafuta ya mil.28 kutoka Dar kwenda Songea, lakini Bombadier zetu zitatumia mafuta ya milioni 1 tu. Tuchukulie mfano wa ndege aina ya Boeing 777 yenye uwezo wa kubeba abiria hadi 450 (mara 6 zaidi ya Bombadier zetu).
Umbali wa Dar to Songea kwa barabara ni maili 655 sawa na kilomita 1,054. Lakini kwa anga ni maili 364 sawa na kilomita 585. Boeing 777 inauwezo wa kukimbia kwa speed ya maili 590 kwa saa, sawa na kilomita 949 kwa saa. Kwahiyo ikisafiri kutoka Dar to Songea (kilomita 585) itatumia mwendo wa dakika 36 tu.
www.distancecalculator.net

Mafuta ya ndege hupimwa kwa galoni (US Liquid gallon) ambapo galoni moja ni sawa na lita 3.7 za ujazo. Boeing 777 inatumia galoni 14.4 za mafuta kwa injini moja kwa dakika (1 lg/engine/minute). Boeing 777 ina injini mbili za "Rolls Royce trent 892" zinazotumia galoni 28.8 za mafuta kwa dakika moja (ingia hapa ). Hivyo basi kwa dakika 36 itakazotumia kutoka Dar to Songea itatumia galoni 1,036.
www.askcaptainlim.com

Galoni moja ya mafuta (US liquid gallon) ina lita 3.7 za ujazo. Kwahiyo galoni 1,036 ni sawa na lita 3,836. Bei ya mafuta ya ndege (jet fuel) katika soko la Marekani ni dola 1.38 kwa galoni moja kwa bei ya September 1 mwaka huu. Kwa Tanzania sijui bei ni kiasi gani, lakini tukadirie ni mara mbili ya bei ya Marekani, yani dola 2.76 kwa galoni moja ya lita 3.7.
www.flightdeckfriend.com

Kwahiyo tukitaka kujua gharama za mafuta ya Boeing 777 kutoka Dar kwenda Songea tunachukua galoni 1,036 mara dola 2.76, mara bei ya dola kwa leo ambayo ni TZS 2,182/=. Utapata Shilingi 6,239,123/=. Hii ndio gharama halisi ya mafuta ambayo Boeing 777 itatumia kutoka Dar to Songea.

Maana yake ni kwamba Boeing 777 itatumia mafuta ya milioni 6.2 kupeleka abiria 450 Songea kutokea Dar.

Sasa twende kwenye Bombadier zetu ambazo Mkuu wa Kaya amesema zinatumia mafuta ya milioni 1 tu kwa safari ya Dar - Songea. Bombadier Q400 inatumia mafuta ya milioni 1 kusafirisha abiria 75 tu kutoka Dar to Songea.
Kwahiyo kama kuna abiria 450 wa kwenda Songea, ndege ya Boeing 777 itawabeba wote na itakwenda mara moja tu kwa mafuta ya milioni 6. Lakini Bombadier itabidi iende trip 6 ndipo iweze kuwamaliza. Yani iende kwa mafuta ya milioni 1, irudi kwa mafuta ya milioni 1 (round ya kwanza), iende tena kwa mafuta ya milioni 1 na kurudi kwa mafuta ya milioni moja (round ya pili). Hadi round zote 6 ziishe Bombadier yetu itakua imetumia mafuta ya milioni 12.
Maana yake ni kwamba Bombadier itaenda round 6 na itatumia mafuta ya milioni 12, kubeba abiria walewale ambao wangebebwa na Boeing 777 mara moja tu na kwa gharama ya mafuta ya milioni 6 tu.

Inaonekana hata waliompa taarifa Mkuu wa kaya hawakufanya utafiti wa kutosha kuhusu gharama, aliposikia mafuta ya milioni 1 Dar to Songea akaona ni gharama ndogo kumbe ndege pia inabeba abiria wachache.
Calculation ya gharama za mafuta lazima ziende sambamba na idadi ya abiria. .


NAOMBA NIONGEZEE FACT NYINGINE KUONYESHA KUWA MKUU WA KAYA ALIDANGANYWA.

Kwa kutumia yale makadirio
1 US Gallon = 3.7 Lita

Dhamani ya Dola ni Tshs 2,182

Kwahiyo,
Kama 3.7 Lita = 2.76 US Dolla
1 Lita = 0.8 US Dolla

Kumbuka Bombadier Q400 inatumia Lita 7 @ Maili

Dar to Songea ni 364 Maili

Angalia hapa:

LITA 7 × 364 MAILI × 0.8 DOLA @ LITA × 2182 TSH (Thamani ya Shilingi @ Dola) = 4,447,788.8 TSHS

KWAHIYO;
GHARAMA YA NDEGE TULIYONUNUA KUSAFIRISHA ABIRIA 75 KUTOKA DAR - SONGEA KWA SAFARI MOJA TU NI 4,447,788.8 TSHS.

Nani alimuambia Mkuu wa Kaya ni 1,000,000 TSHS?


ALIYEMDANGANYA MKUU WA KAYA AADHIBIWE....

NAIPENDA TANZANIA NAWACHUKIA WAPIGA DILI.
Very nice facts and good calculation kaka, tatizo watu wa humu ndani sijui vichwa vyao ni vigumu kuelewa au wamerogwaa nini? mdau ametolea kama assumption ya Bombardier na Boeing Airbus on Landing to Songea, as just an example, ndo mana akafanya hizo hesabu, it might be yes ikawa Mwanza Airport to Zanzibar or JKIA, route zenye watu wengi , but ujumbe ukiusoma vzr mbn unajielezaa? sasa kuna manyumbu fulani humu ndani yanaponda tu habari za Songea na abiria wake eti hawafiki idadi hiyo, Ebu elimu zetu zitusaidie jamani, so shame of u nyumbuz!
Hao abiria 400+ wanaokwenda Songea ni kina nani? Tumia akili hii nyepesi: Why send a nearly empty Boeing to Songea when a Bombardier could fit the purpose? Tatizo lenu sio ndege, ingekuwa kubwa mngeponda, sasa ni ndogo mnaponda. Mbona hamzungumzii mabehewa mapya ya kuifufua Reli ya Kati? Acheni siasa za chuki
 
tufafanulie hizo dk 36 za boeing dar to songea, huenda uzi wote ukakosa maana hapo!
 
Hao 75 mnao ? Weka majina yao na account zao JF.
Fikra fikra

Uwezo na matumizi ndivyo vya kufanyia hesabu. Kwa nini wafikiri songea hakuna abiria 400?
 
Kwa nyingeza kuna gharama ambazo ni lazima (fixed costs) ndege imepaa au la! Ndege imejaza abiria na mizigo au la!

Ati unanua roli na mtoto wake (tani 40) kubeba tani 5 ambazo zingebebwa na canter! Uchumi gani huo! Mtoa mada akajifunze uchumi kwanza "economies of scale"!
Kama sababu ya msingi Ni economies of scale, basi mkuu wa kaya ndio alitakiwa aseme hivyo wakati anazipigia upatu bombardier, yeye kaenda kwenye mfano wa mafuta+umbali wa Dar-Songea pekee, Na b191 katembelea nyayo hizo hizo kuleta uzi. Kimsingi kosa limeanzia kwenye maelezo ya mkuu wa kaya.
 
Cha arusha pia imewahi kutua Ethiopian airways hahahahaha
Ile ilipoteza uelekeo bhana na jamaa alitua akijua anatua KIA ndiyo maana iliserereka hadi ikavuka runway na kuingia kwenye majani na siku ya kuja kuirusha alitafutwa rubani mahiri na ndege ikiwa haina mzigo ndo maana akaweza kuipaisha.
 
Yaani hata kama abiria wapo wa kutosha wa kwenda na kurudi songea bado bombardier itakua na faida.
 
Wewe mdau mleta mada kias flan hauko sawa.kama trip moja ya Bomberdier ni abiria 75, kwenda na kurudi si abiria 150? Na ili upate hao 450 itahitaj trip 3. Au mwenzetu ulichukulia inarud na ruban tu bila abiria wala chochote? Au hiyo 1 million sio return trip?
Duh, wewe Kamanda Moshi ndiye mfano halisi ya Mtanzania mdanganyika ninayemfahamu...ndege inabeba abiria 75 na ili iweze kubeba abiria 150 ni lazima ifanye trip mbili. Trip mbili mara tatu ni trip sita...yaani hata mimi ambaye sikuona milango ya shule siwezi kuleta ubishi wa kijinga kama huu.

Na kwa kuongezea tu...hivi hizi bombadier zimeletwa kwa safari local tu za ndani? Nauliza tu kwa nia nzuri...yaani zitawanufaisha tu Watanzania wenye uwezo ambao ama ni wayanya biashara wakubwa au viongozi wa serikali. Mkulima kijijini ananufaikaje na hizi ndege local?
 
''Analysis nzuri'' for only mentally sick people! Ukiwa na sound mind huwezi hata kufikiria sembuse kupendekeza Boeing triple 7 ifanye safari za Songea - Dar!
Samahani mkuu nauliza tuu!, hivi Ni kwa nini kwenye usafiri wa anga huwa kunakuwa Na utaratibu wa kubadili ndege?,
Hivi Ni kwa nini Kuna route zinamilikiwa Na ndege kubwa Na kufaurisha abiria wanaletwa ndege ndogo. Kuna mahali ufahamu wetu umekua fixed kwamba usafiri wa ndege Ni lazima uwe direct route!.
 
Aisee kweli hesabu hazidanganyi, wamemdanganya Rais


Hao waliomshauri Rais wako sahihi kwani unaponunua ndege za abiria unaangalia effective demand ya usafiri husika!! Hivi sasa ndege za aina ya Bombardier [ ambazo ATCL ilikuwa nazo] zimeonekana kuwa ni economical in fuel consumption na ideal kwa condition ya viwanja vyetu vya ndege; nyie mnaoshabikia ndege kubwa za Boeing mjue kwamba watu wanaojua Aviation economics kama Fastjet ambao walikuwa wanarusha BOEING katika safari zao hivi sasa wanafikiria kuanza kutumia ndege ndogo baada ya ujio wa JPM Bombadier aircraft!!!
 
Hiyo 'nondo' ngoja niifanya ni homework niisome baadae
 
Hoja yako inaweza kuwa na substance. Lakini jee tunao abiria 450 wa kupanda Boeing 777 kwenda Songea Kwa wakati mmoja? Nadhani walimshauri Mkuu wa Kaya waliangalia vigezo kadhaa ikiwemo ulichokijengea hoja.
Yeye hajasema inunuliwe boing, anachosema ni kuwa alidanganywa unafuu wa mafuta!..1,000,000 Tsh per trip
 
Hao abiria 400+ wanaokwenda Songea ni kina nani? Tumia akili hii nyepesi: Why send a nearly empty Boeing to Songea when a Bombardier could fit the purpose? Tatizo lenu sio ndege, ingekuwa kubwa mngeponda, sasa ni ndogo mnaponda. Mbona hamzungumzii mabehewa mapya ya kuifufua Reli ya Kati? Acheni siasa za chuki
Tatizo lenu mmechagua kuwa wakali tu kwa wanaotoa maoni msiyoyapenda-kumbe mkulu alipozungumzia ndege nyingine zinatumia mafuta ya gharama ya milioni zaidi ya 30 alikusudia nini? Mnamdanganya mnapoumbuliwa macho yanawatoka!
 
Back
Top Bottom