Nani amemdanganya Mkuu wa Kaya?

Nani amemdanganya Mkuu wa Kaya?

Tatizo lenu mmechagua kuwa wakali tu kwa wanaotoa maoni msiyoyapenda-kumbe mkulu alipozungumzia ndege nyingine zinatumia mafuta ya gharama ya milioni zaidi ya 30 alikusudia nini? Mnamdanganya mnapoumbuliwa macho yanawatoka!

Katika hizo ndege nyingine alitaja Boeing 777 ya watu 450?
 
Awali ya yote nichukue fursa hii kumpongeza Mkuu wa Kaya yetu kwa moyo wake wa kizalendo wa kutuletea ndege mbili mpya ili kufufua shirika letu ambalo wenzie walilitafuna na kulifilisi. Japo haohao ndio wanaomshangilia kama vile waliofilisi shirika hilo siyo wao.

Mkuu wa Kaya umedanganywa kuhusu gharama za usafiri wa ndege Dar to Songea. Amesema kuwa ndege za kawaida zinaweza kutumia mafuta ya milioni 28 kutoka Dar to Songea lakini ndege mpya za Bombadier Q400 zitatumia mafuta ya milioni 1 tu. Mimi sio mtaalamu wa ndege lakini taarifa imenifanya kufanya utafiti kidogo

Katika kajiutafiti kangu nimegundua kiwango cha mafuta ya ndege kwa safari hakipo constant. Kinatofautiana kutokana na sababu anuai, kama vile aina ya ndege, umbali wa safari, uzito wa mzigo wa kwenye cabin, kimo kutoka usawa wa bahari, namna ya kupaa. Vyote hivi huchangia utofauti wa utumiaji wa mafuta ktk ndege.

Katika hayo tuchukue moja la aina ya ndege na hayo mengi yawe constant (under ceteris peribus). Mkuu wa Kaya amesema "ndege nyingine" zitatumia mafuta ya mil.28 kutoka Dar kwenda Songea, lakini Bombadier zetu zitatumia mafuta ya milioni 1 tu. Tuchukulie mfano wa ndege aina ya Boeing 777 yenye uwezo wa kubeba abiria hadi 450 (mara 6 zaidi ya Bombadier zetu).
Umbali wa Dar to Songea kwa barabara ni maili 655 sawa na kilomita 1,054. Lakini kwa anga ni maili 364 sawa na kilomita 585. Boeing 777 inauwezo wa kukimbia kwa speed ya maili 590 kwa saa, sawa na kilomita 949 kwa saa. Kwahiyo ikisafiri kutoka Dar to Songea (kilomita 585) itatumia mwendo wa dakika 36 tu.
www.distancecalculator.net

Mafuta ya ndege hupimwa kwa galoni (US Liquid gallon) ambapo galoni moja ni sawa na lita 3.7 za ujazo. Boeing 777 inatumia galoni 14.4 za mafuta kwa injini moja kwa dakika (1 lg/engine/minute). Boeing 777 ina injini mbili za "Rolls Royce trent 892" zinazotumia galoni 28.8 za mafuta kwa dakika moja (ingia hapa ). Hivyo basi kwa dakika 36 itakazotumia kutoka Dar to Songea itatumia galoni 1,036.
www.askcaptainlim.com

Galoni moja ya mafuta (US liquid gallon) ina lita 3.7 za ujazo. Kwahiyo galoni 1,036 ni sawa na lita 3,836. Bei ya mafuta ya ndege (jet fuel) katika soko la Marekani ni dola 1.38 kwa galoni moja kwa bei ya September 1 mwaka huu. Kwa Tanzania sijui bei ni kiasi gani, lakini tukadirie ni mara mbili ya bei ya Marekani, yani dola 2.76 kwa galoni moja ya lita 3.7.
www.flightdeckfriend.com

Kwahiyo tukitaka kujua gharama za mafuta ya Boeing 777 kutoka Dar kwenda Songea tunachukua galoni 1,036 mara dola 2.76, mara bei ya dola kwa leo ambayo ni TZS 2,182/=. Utapata Shilingi 6,239,123/=. Hii ndio gharama halisi ya mafuta ambayo Boeing 777 itatumia kutoka Dar to Songea.

Maana yake ni kwamba Boeing 777 itatumia mafuta ya milioni 6.2 kupeleka abiria 450 Songea kutokea Dar.

Sasa twende kwenye Bombadier zetu ambazo Mkuu wa Kaya amesema zinatumia mafuta ya milioni 1 tu kwa safari ya Dar - Songea. Bombadier Q400 inatumia mafuta ya milioni 1 kusafirisha abiria 75 tu kutoka Dar to Songea.
Kwahiyo kama kuna abiria 450 wa kwenda Songea, ndege ya Boeing 777 itawabeba wote na itakwenda mara moja tu kwa mafuta ya milioni 6. Lakini Bombadier itabidi iende trip 6 ndipo iweze kuwamaliza. Yani iende kwa mafuta ya milioni 1, irudi kwa mafuta ya milioni 1 (round ya kwanza), iende tena kwa mafuta ya milioni 1 na kurudi kwa mafuta ya milioni moja (round ya pili). Hadi round zote 6 ziishe Bombadier yetu itakua imetumia mafuta ya milioni 12.
Maana yake ni kwamba Bombadier itaenda round 6 na itatumia mafuta ya milioni 12, kubeba abiria walewale ambao wangebebwa na Boeing 777 mara moja tu na kwa gharama ya mafuta ya milioni 6 tu.

Inaonekana hata waliompa taarifa Mkuu wa kaya hawakufanya utafiti wa kutosha kuhusu gharama, aliposikia mafuta ya milioni 1 Dar to Songea akaona ni gharama ndogo kumbe ndege pia inabeba abiria wachache.
Calculation ya gharama za mafuta lazima ziende sambamba na idadi ya abiria. .


NAOMBA NIONGEZEE FACT NYINGINE KUONYESHA KUWA MKUU WA KAYA ALIDANGANYWA.

Kwa kutumia yale makadirio
1 US Gallon = 3.7 Lita

Dhamani ya Dola ni Tshs 2,182

Kwahiyo,
Kama 3.7 Lita = 2.76 US Dolla
1 Lita = 0.8 US Dolla

Kumbuka Bombadier Q400 inatumia Lita 7 @ Maili

Dar to Songea ni 364 Maili

Angalia hapa:

LITA 7 × 364 MAILI × 0.8 DOLA @ LITA × 2182 TSH (Thamani ya Shilingi @ Dola) = 4,447,788.8 TSHS

KWAHIYO;
GHARAMA YA NDEGE TULIYONUNUA KUSAFIRISHA ABIRIA 75 KUTOKA DAR - SONGEA KWA SAFARI MOJA TU NI 4,447,788.8 TSHS.

Nani alimuambia Mkuu wa Kaya ni 1,000,000 TSHS?


ALIYEMDANGANYA MKUU WA KAYA AADHIBIWE....

NAIPENDA TANZANIA NAWACHUKIA WAPIGA DILI.
Takwimu zake nyingi huwa ni utata mtupu lakini baadhi yetu huzifuatilia na tukibaini ukweli hubaki vinywa wazi.

Thank u for this!
 
Ukiona watu wanauliza ujue pamoja na kuongeza hizo facts bado hujaeleweka, kuna haya mawili:
1. Je kiwanja cha ndege cha Songea kinaweza kutumiwa na Boeing 777?na je kuna viwanja vingapi nchini sasa vitaweza kutumiwa na ndege hiyo?hii ni hoja ya msingi sana kufikia uamuzi.
2. Je tuna abiria 450 kwa safari moja watakaosafiri kati ya Dar na Songea, Dar na Mbeya, Dar na Tabora, na Dar na Dodoma kwa uchache? Kwa kuongezea tu kwa sasa usafiri wa ndege Songea na Dar unakuwepo kama mara mbili au tatu kwa wiki, na uwezo wa ndege hizo ni abiria 12 tu kwa safari.Maana yake Songea kwa wiki kuna watu wanaopanda ndege wasiozidi 36 kwa route moja, sasa unawaletea ghafla ndege ya abiria 450?

Ukijibu hayo maswali ndipo utakuwa na haki ya kuelekea kwenye calculations hizo, bila vigezo hivyo viwili Boeing 777 haiwezi kuwa na maana.
Mkuu wa kaya angesema hatununui Boeing kwa sababu hatuna viwanja, hatuna abiria wengi kwa mkupuo wanaotumia ndege, huu uzi ungekosa maana, lakini kwa sababu alikimbilia kwenye mafuta kwa umbali wa dar-songea!, ndio maana mleta uzi kafanya uchochezi kwa kigezo hicho hicho!.
 
Kwa hiyo alidanganywa kwenye 28Mil lakini 1Million ya bombardier iko sawa?
 
Ngoja tukupe ufahamu. Na lazima mwelewe tu, maana hakuna jinsi:

• Dar - Songea abiria 75 = trip 1 mafuta ya TZS 1,000,000

• Songea - Dar abiria 75 = trip 2 mafuta ya TZS 1,000,000

• Dar - Songea abiria 75 = trip 3 mafuta ya TZS 1,000,000

• Songea - Dar abiria 75 = trip 4 mafuta ya TZS 1,000,000

• Dar - Songea abiria 75 = trip 5 mafuta ya TZS 1,000,000

• Songea - Dar abiria 75 = trip 6 mafuta ya TZS 1,000,000

Kwa hiyo;

Trip ni 6

TRIP abiria 75

Maana yake 75 × 6 = 450 passengers!!

Gharama ya mafuta kwa mujibu wa "Mtukufu" ni;

TZS 1,000,000 kwa safari moja

Safari (trip) ni 6

Kwa hiyo gharama ya mafuta ni;

TZS 1,000,000 × 6 = 6,000,000!!!

Hiyo ni Bombadia Mapanga shaa yenye capacity ya kubeba abiria 75 kwa safari moja!!

Je, Boeing 777 yenye uwezo wa kubeba abiria 450 kwa mpigo au safari moja?

At least LumumbaB7Bombadia wenzako wameshaelewa na wanakuja na ubishi ktk engo tofauti

Ingalau wenzako wanabisha kuwa, tatizo ni kuwa hakuna uwanja wa kutua Boeing 777 huko Songea lakini kwa ishu ya gharama maana yake wanakubali kuwa "Mtukufu" amedanganywa mchana kweupe!!

NB: Rudia tena kusoma uzi wa mleta mada utaelewa. Naamini hukusoma na kuelewa ndiyo maana umekuja na ubishi usio na kichwa wala miguu!!
Kwa hiyo hapo ndio tuseme punda kashurutishwa kufika mtoni Na kushutishwa kunywa maji pia.
 
Kama sababu ya msingi Ni economies of scale, basi mkuu wa kaya ndio alitakiwa aseme hivyo wakati anazipigia upatu bombardier, yeye kaenda kwenye mfano wa mafuta+umbali wa Dar-Songea pekee, Na b191 katembelea nyayo hizo hizo kuleta uzi. Kimsingi kosa limeanzia kwenye maelezo ya mkuu wa kaya.
Tatizo ni la mtoa mada kufanya hesabu za kawaida (kutoa na kujumlisha) kumkosoa Mkuu wa Kaya pasipo kujua uamuzi wa kuwekeza kimaendeleo ni suala la kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiteknolojia
 
Very nice facts and good calculation kaka, tatizo watu wa humu ndani sijui vichwa vyao ni vigumu kuelewa au wamerogwaa nini? mdau ametolea kama assumption ya Bombardier na Boeing Airbus on Landing to Songea, as just an example, ndo mana akafanya hizo hesabu, it might be yes ikawa Mwanza Airport to Zanzibar or JKIA, route zenye watu wengi , but ujumbe ukiusoma vzr mbn unajielezaa? sasa kuna manyumbu fulani humu ndani yanaponda tu habari za Songea na abiria wake eti hawafiki idadi hiyo, Ebu elimu zetu zitusaidie jamani, so shame of u nyumbuz!
Afadhali umenisaidia maana kila nikitaka ku comment najikuta jazba inapanda kwasababu hao nyumbu basi naacha. Tatizo ni ELIMU, ELIMU, ELIMU
Hii post inataka u fikirie nje ya box.
Dhana ya great thinker naona haina nguvu nowdays
 
Tatizo ni la mtoa mada kufanya hesabu za kawaida (kutoa na kujumlisha) kumkosoa Mkuu wa Kaya pasipo kujua uamuzi wa kuwekeza kimaendeleo ni suala la kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiteknolojia
Mtoa mada kafanya comparative of economic fuel consumption kwa mujibu wa mkuu wa kaya, mengine tunayaongeza sisi mwisho tunajikuta tuko nje ya mada husika
 
Kwa kiasi kikubwa hesabu zako zaweza kuwa sawa... Ila je ni wangapi wapanda ndege kutoka Dar to Songea?

Viwanja vina accomodate hizo boeing 777??

Hiyo bombadier yenyewe yaweza kwenda mswaki na ndo ndege ndogo ya abiria 75 tu.... Alafu wewe unataka ziletwe boeing 777

Subiri kwanza itengenezwe miundombinu ndo zitakuja hizo 777....
 
Mtoa mada kafanya comparative of economic fuel consumption kwa mujibu wa mkuu wa kaya, mengine tunayaongeza sisi mwisho tunajikuta tuko nje ya mada husika
Si kweli unavyotetea. Mtoa mada amefanta kosa la maingi kwa kuzungumzia "investment decision" kwa "simple comperative of economic fuel consumption". Hata hesabu yake hiyo ya mlinganisho kaifanya isivyo sahihi. Sihitaji kwenda kwa undani kuhusu hili, kwa kuwa limekwisha changiwa vya kutosha, humu jamvini.

Rejea tena hotuba ya Mkuu wa Kaya kuhusu faida ya hizo ndege mpya kulinganisha na zingine, alizoziainisha. Suala la gharama la mafuta lilikuwa moja katika faida nyingi. Iweje kukosoa maamuzi ya kununua hizo ndege (au kudanganyika kwa Mkuu wa Kaya) kwa hesabu ya shule za msingi.

TUWE MAKINI TUNAPOKOSOA KANA KWAMBA WANAOFANYA MAAMUZI NI MBUMBUMBU
 
Am much better, ndiyo maana nimeweka na link hapo ili udukue zaidi.
Wewe ni Malisa? Kama sio basi umekopi post ya Malisa huko Facebook ukaileta hapa na kibaya zaid unashindwa hata kuitetea zaid ya ''Am much better''edit post yako uonyeshe heshima kwa muandishi mbona naona watu wanakuuliza maswali yasiyolingana na akili yako
 
Mkuu wewe shughulika na imani ya UKUTA. Haya ya ndege hamtayaweza. Sasa hivi Bombardiers ziko tayari kwa kazi tuna subiri Boeing.

Tunachotaka leo tarehe moja Oktoba ni kwanini hakuna UKUTA?
Mimi siyo mwanasiasa na sina chama ila napenda facts hasa mahali ambapo panahitaji seriousness.
 
Hoja yako inaweza kuwa na substance. Lakini jee tunao abiria 450 wa kupanda Boeing 777 kwenda Songea Kwa wakati mmoja? Nadhani walimshauri Mkuu wa Kaya waliangalia vigezo kadhaa ikiwemo ulichokijengea hoja.
Hoja hapa ni uwiano wa matumizi ya mafuta, million 28 kwa million moja, inawezekana wapi hii??
Na aliyejaribu ku-compare hayo matumizi na kuja na hoja ya 28m kwa 1m, ilizingatia safari za kwenda wapi?
 
Kama sababu ya msingi Ni economies of scale, basi mkuu wa kaya ndio alitakiwa aseme hivyo wakati anazipigia upatu bombardier, yeye kaenda kwenye mfano wa mafuta+umbali wa Dar-Songea pekee, Na b191 katembelea nyayo hizo hizo kuleta uzi. Kimsingi kosa limeanzia kwenye maelezo ya mkuu wa kaya.
ASANTE SANA KWA KUNIELEWA VIZURI.
 
Hoja hapa ni uwiano wa matumizi ya mafuta, million 28 kwa million moja, inawezekana wapi hii??
Na aliyejaribu ku-compare hayo matumizi na kuja na hoja ya 28m kwa 1m, ilizingatia safari za kwenda wapi?
Unapolinganisha ndege hizi mbili, zote uzijengee mazingira sawa, umbali, uwezo wa kubeba (full capacity), mwelekeo, hali ya hewa, and what have you! ...swala la kwenda songea, au wapi ni mfano tu. Kwani ni nani asiyejua Boeing haiendi Songea! Ni nani asiyejua kuwa si rahisi kupata abiria wa kuijaza Boeing kwenda Songea, n.k.

Na je, hizo ndege zetu zitamudu ushindani wa kwenda nje ya nchi, au zote mbili ni kwa ajili ya kuzunguka Tanzania tu, na mchina jirani?
 
Back
Top Bottom