VICTOR BASHINGWA
Member
- Sep 24, 2016
- 16
- 8
kwenye boing umetoa hesabu ya mafuta ya kwenda tu na hauja toa ya kuludi.Lkn pia je hiyo Songea yaweza kuwa na abilia 450 kwa kila safari?nahisi nawe umesahau ni watu wa aina gani wanapanda ndege tz.
Kuna kitu nimeongeza kwenye uzi wangu pitia tena nadhani utakuwa umenielewa vizuriKwa hiyo wewe unashauri boeing triple 7 itumike kwenye usafiri wa Dar Songea? Makubwa tena makubwa kabisa. Will you please refrain from giving advanced technical advise for something you dont know? Ningeshauri sana wewe na watanzania wengi wanaofungua thread za kijinga kila siku hapa kusemea technical issues za air aviation ambazo hawajui hata abc zake wakae kumya.
Ni kweli ila hebu soma nilichoongezea halafu uniambie hapo tumeokoa nini?Kwa nyingeza kuna gharama ambazo ni lazima (fixed costs) ndege imepaa au la! Ndege imejaza abiria na mizigo au la!
Ati unanua roli na mtoto wake (tani 40) kubeba tani 5 ambazo zingebebwa na canter! Uchumi gani huo! Mtoa mada akajifunze uchumi kwanza "economies of scale"!
Mkuu,Mafuta ya ndege hupimwa kwa galoni (US Liquid gallon) ambapo galoni moja ni sawa na lita 3.7 za ujazo. Boeing 777 inatumia galoni 14.4 za mafuta kwa injini moja kwa dakika (1 lg/engine/minute). Boeing 777 ina injini mbili za "Rolls Royce trent 892" zinazotumia galoni 28.8 za mafuta kwa dakika moja (ingia hapa ). Hivyo basi kwa dakika 36 itakazotumia kutoka Dar to Songea itatumia galoni 1,036.
www.askcaptainlim.com
...
Kumbuka Bombadier Q400 inatumia Lita 7 @ Maili
...
...
Nimefanya uchambuzi kwa mafuta ya ndege tuliyonunua.Mkuu,
1) Ikitokea tuseme kuna demand ya abiria labda 200 tu wa kwenda songea kwa Muda huo uliozungumzia huoni kama hesabu zako zitakinzana??
Manake Bombardier itahitajika kwenda trip mbili labda kwa mafuta ya hiyo 4mil total wakati Boeing mwendo ni uleule wa afuta ya 6mil (kwenda tu)??
2) Kama umeweza kufanya upembuzi ukagundua Si kweli kua Boeing inagharimu Over 26Mil bali only 6mil, mbona hukufanya upebuzi huohuo kwenye mafuta ya Bombardier? Huoni kama inawezekana aliedanganya kwenye mafuta ya Boeing atakua amedanganya pia kwenye mafuta ya Bombardier?? Huoni kama inawezekana hata hiyo 1mil per trip inaweza kua kubwa nayo kama ilivyokuzwa ile ya Boeing??
Algebra inakuona mkuu!!Mkuu,
1) Ikitokea tuseme kuna demand ya abiria labda 200 tu wa kwenda songea kwa Muda huo uliozungumzia huoni kama hesabu zako zitakinzana??
Manake Bombardier itahitajika kwenda trip mbili labda kwa mafuta ya hiyo 4mil total wakati Boeing mwendo ni uleule wa afuta ya 6mil (kwenda tu)??
2) Kama umeweza kufanya upembuzi ukagundua Si kweli kua Boeing inagharimu Over 26Mil bali only 6mil, mbona hukufanya upebuzi huohuo kwenye mafuta ya Bombardier? Huoni kama inawezekana aliedanganya kwenye mafuta ya Boeing atakua amedanganya pia kwenye mafuta ya Bombardier?? Huoni kama inawezekana hata hiyo 1mil per trip inaweza kua kubwa nayo kama ilivyokuzwa ile ya Boeing??
Yes Mkuu, na kwa kuwa hii aliyofanya ni comparative analysis, under ceteris peribus, basi hakutakuwa kutoa conclusion kwa derivative ya comsuption kwa boing against number of trips kwa bombardier, alitakiwa aweke analysis ya consumption ya hayo mapanga boi kwanza ndipo ajenge base ya hitimisho. Kifupi kafanya kazi nusu, kahukumu bila kumpa mshtakiwa wasaa wa kujitetea. Pangu Pakavu.
Mimi nadhani uamuzi wa kununua ndege ndogo kwa matumizi ya ndani, ni uamuzi sahihi kwa wakati huu kwa sababu kwa sasa watumiaji wa usafiri wa ndege ni wachache.
Lakini pia siyo kweli kwamba Dash 8 Q400 ndiyo ndege bora kuliko nyingine zote kwa mazingira ya aina zote. Kusema kuwa Q400 inatumia mafuta kidogo kuliko ndege nyingine zote nao ni uwongo pia. Matumizi ya mafuta kwa ndege hupimwa kwa kuangalia wastani wa matumizi ya mafuta kwa abiria mmoja kwa kilometa 100. Na kwenye kipimo hicho mpaka sasa Q400 is not the best.
Hapo unaongelea matumizi ya mafuta. Na matumizi ya mafuta siyo yanayoweza kulihakikishia shirika kupata faida. Faida hutegemea zaidi efficiency ya shirika.
Ni efficiency pekee ndiyo itakayolifanya ATCL isonge mbele au ianguke, wala siyo kiasi cha mafuta ndege zinachotumia au upya wa ndege tulizo nazo.
Sasa utafanya kazi kama hesabu zenyewe ndo hizo!! Kweli??????fanyeni kazi,kazi kudukua magufuli kaongea nini mpate pa kusemea
by the late BobmaryLabda ni Stiff necked fool. ..![]()
Kuna kipindi JF inakuwa kweli nyumba ya wataalamu na wanaotumia akili na elimu yao. Bandiko hili linawakilisha vyema uwapo wa great thinkers.Awali ya yote nichukue fursa hii kumpongeza Mkuu wa Kaya yetu kwa moyo wake wa kizalendo wa kutuletea ndege mbili mpya ili kufufua shirika letu ambalo wenzie walilitafuna na kulifilisi. Japo haohao ndio wanaomshangilia kama vile waliofilisi shirika hilo siyo wao.
Mkuu wa Kaya umedanganywa kuhusu gharama za usafiri wa ndege Dar to Songea. Amesema kuwa ndege za kawaida zinaweza kutumia mafuta ya milioni 28 kutoka Dar to Songea lakini ndege mpya za Bombadier Q400 zitatumia mafuta ya milioni 1 tu. Mimi sio mtaalamu wa ndege lakini taarifa imenifanya kufanya utafiti kidogo
Katika kajiutafiti kangu nimegundua kiwango cha mafuta ya ndege kwa safari hakipo constant. Kinatofautiana kutokana na sababu anuai, kama vile aina ya ndege, umbali wa safari, uzito wa mzigo wa kwenye cabin, kimo kutoka usawa wa bahari, namna ya kupaa. Vyote hivi huchangia utofauti wa utumiaji wa mafuta ktk ndege.
Katika hayo tuchukue moja la aina ya ndege na hayo mengi yawe constant (under ceteris peribus). Mkuu wa Kaya amesema "ndege nyingine" zitatumia mafuta ya mil.28 kutoka Dar kwenda Songea, lakini Bombadier zetu zitatumia mafuta ya milioni 1 tu. Tuchukulie mfano wa ndege aina ya Boeing 777 yenye uwezo wa kubeba abiria hadi 450 (mara 6 zaidi ya Bombadier zetu).
Umbali wa Dar to Songea kwa barabara ni maili 655 sawa na kilomita 1,054. Lakini kwa anga ni maili 364 sawa na kilomita 585. Boeing 777 inauwezo wa kukimbia kwa speed ya maili 590 kwa saa, sawa na kilomita 949 kwa saa. Kwahiyo ikisafiri kutoka Dar to Songea (kilomita 585) itatumia mwendo wa dakika 36 tu.
www.distancecalculator.net
Mafuta ya ndege hupimwa kwa galoni (US Liquid gallon) ambapo galoni moja ni sawa na lita 3.7 za ujazo. Boeing 777 inatumia galoni 14.4 za mafuta kwa injini moja kwa dakika (1 lg/engine/minute). Boeing 777 ina injini mbili za "Rolls Royce trent 892" zinazotumia galoni 28.8 za mafuta kwa dakika moja (ingia hapa ). Hivyo basi kwa dakika 36 itakazotumia kutoka Dar to Songea itatumia galoni 1,036.
www.askcaptainlim.com
Galoni moja ya mafuta (US liquid gallon) ina lita 3.7 za ujazo. Kwahiyo galoni 1,036 ni sawa na lita 3,836. Bei ya mafuta ya ndege (jet fuel) katika soko la Marekani ni dola 1.38 kwa galoni moja kwa bei ya September 1 mwaka huu. Kwa Tanzania sijui bei ni kiasi gani, lakini tukadirie ni mara mbili ya bei ya Marekani, yani dola 2.76 kwa galoni moja ya lita 3.7.
www.flightdeckfriend.com
Kwahiyo tukitaka kujua gharama za mafuta ya Boeing 777 kutoka Dar kwenda Songea tunachukua galoni 1,036 mara dola 2.76, mara bei ya dola kwa leo ambayo ni TZS 2,182/=. Utapata Shilingi 6,239,123/=. Hii ndio gharama halisi ya mafuta ambayo Boeing 777 itatumia kutoka Dar to Songea.
Maana yake ni kwamba Boeing 777 itatumia mafuta ya milioni 6.2 kupeleka abiria 450 Songea kutokea Dar.
Sasa twende kwenye Bombadier zetu ambazo Mkuu wa Kaya amesema zinatumia mafuta ya milioni 1 tu kwa safari ya Dar - Songea. Bombadier Q400 inatumia mafuta ya milioni 1 kusafirisha abiria 75 tu kutoka Dar to Songea.
Kwahiyo kama kuna abiria 450 wa kwenda Songea, ndege ya Boeing 777 itawabeba wote na itakwenda mara moja tu kwa mafuta ya milioni 6. Lakini Bombadier itabidi iende trip 6 ndipo iweze kuwamaliza. Yani iende kwa mafuta ya milioni 1, irudi kwa mafuta ya milioni 1 (round ya kwanza), iende tena kwa mafuta ya milioni 1 na kurudi kwa mafuta ya milioni moja (round ya pili). Hadi round zote 6 ziishe Bombadier yetu itakua imetumia mafuta ya milioni 12.
Maana yake ni kwamba Bombadier itaenda round 6 na itatumia mafuta ya milioni 12, kubeba abiria walewale ambao wangebebwa na Boeing 777 mara moja tu na kwa gharama ya mafuta ya milioni 6 tu.
Inaonekana hata waliompa taarifa Mkuu wa kaya hawakufanya utafiti wa kutosha kuhusu gharama, aliposikia mafuta ya milioni 1 Dar to Songea akaona ni gharama ndogo kumbe ndege pia inabeba abiria wachache.
Calculation ya gharama za mafuta lazima ziende sambamba na idadi ya abiria. .
NAOMBA NIONGEZEE FACT NYINGINE KUONYESHA KUWA MKUU WA KAYA ALIDANGANYWA.
Kwa kutumia yale makadirio
1 US Gallon = 3.7 Lita
Dhamani ya Dola ni Tshs 2,182
Kwahiyo,
Kama 3.7 Lita = 2.76 US Dolla
1 Lita = 0.8 US Dolla
Kumbuka Bombadier Q400 inatumia Lita 7 @ Maili
Dar to Songea ni 364 Maili
Angalia hapa:
LITA 7 × 364 MAILI × 0.8 DOLA @ LITA × 2182 TSH (Thamani ya Shilingi @ Dola) = 4,447,788.8 TSHS
KWAHIYO;
GHARAMA YA NDEGE TULIYONUNUA KUSAFIRISHA ABIRIA 75 KUTOKA DAR - SONGEA KWA SAFARI MOJA TU NI 4,447,788.8 TSHS.
Nani alimuambia Mkuu wa Kaya ni 1,000,000 TSHS?
ALIYEMDANGANYA MKUU WA KAYA AADHIBIWE....
NAIPENDA TANZANIA NAWACHUKIA WAPIGA DILI.
Hebu hata usimjibu. Maana hawa vijana wanaamini tafiti za kutumia mitandao pasipo kushughulisha akili zao. Haya ni matokeo ya elimu ya vyeti mbadala anayopanbana nayo Ndalichako.Hujui chochote bwana. Eti ''im much better''. Unapendekeza boeng triple 7 iwe inafanya safari za Dar Songea halafu unasema ''im much better! You are not! You are STILL sick sir/madam!
