Nani amemdanganya Mkuu wa Kaya?

Nani amemdanganya Mkuu wa Kaya?

Am much better, ndiyo maana nimeweka na link hapo ili udukue zaidi.
Hujui chochote bwana. Eti ''im much better''. Unapendekeza boeng triple 7 iwe inafanya safari za Dar Songea halafu unasema ''im much better! You are not! You are STILL sick sir/madam!
 
Mkuu umefanya analysis nzuri lakini hukumalizia ndio maana utapata critism nyingi. ungefanya kitu kimoja ungekata mzizi wa fitna

moja ungeafanya cost analysis kwa abiria mmoja ndege ikiwa imejaa (fully capacity), ikiwa na abiria (50% capacity) na ikiwa na abiria 25% inakuaje. hii itamaliza kabisa fitna yeyote
''Analysis nzuri'' for only mentally sick people! Ukiwa na sound mind huwezi hata kufikiria sembuse kupendekeza Boeing triple 7 ifanye safari za Songea - Dar!
 
Taratibu tutanunua na ndege kubwa pia, dege kubwa unalipeleka Songea hao abiria utawapata wapi? Kwahesabu za kibiashara hizi ndege kwasasa ni good idéal...
 
Hujui chochote bwana. Eti ''im much better''. Unapendekeza boeng triple 7 iwe inafanya safari za Dar Songea halafu unasema ''im much better! You are not! You are STILL sick sir/madam!
Thank you Sir / Madam

NAONGEZEA FACT NYINGINE NADHANI UKIISOMA UTANIELEWA.
 
Hao abiria 400+ wanaokwenda Songea ni kina nani? Tumia akili hii nyepesi: Why send a nearly empty Boeing to Songea when a Bombardier could fit the purpose? Tatizo lenu sio ndege, ingekuwa kubwa mngeponda, sasa ni ndogo mnaponda. Mbona hamzungumzii mabehewa mapya ya kuifufua Reli ya Kati? Acheni siasa za chuki
Yaani hujamuelewa kabisaa jamaa... the guy has point....
 
Mkuu....
Hivi unayo hiyo milioni 7?
Yaani ukisoma hoja ya swali la mleta uzi ni kwamba.. NANI ANAMDANGANYA MKUU WA KAYA?
Alafu wewe ulipo weka picha ya Waziri mkuu na Mkuu wa kaya, maana yake ni kwamba huyo ndie anae mdanganya...
Ebu ngoja niishie hapa kwanza
wewe ndiye unatakiwa kushtakiwa kwasababu ya uchochezi.mimi sijasema hayo uliyosema je unajua sheria?

swissme
 
Wewe mdau mleta mada kias flan hauko sawa.kama trip moja ya Bomberdier ni abiria 75, kwenda na kurudi si abiria 150? Na ili upate hao 450 itahitaj trip 3. Au mwenzetu ulichukulia inarud na ruban tu bila abiria wala chochote? Au hiyo 1 million sio return trip?
Kwani hao 450 ni wa kwenda na kurudi..??
 
Awali ya yote nichukue fursa hii kumpongeza Mkuu wa Kaya yetu kwa moyo wake wa kizalendo wa kutuletea ndege mbili mpya ili kufufua shirika letu ambalo wenzie walilitafuna na kulifilisi. Japo haohao ndio wanaomshangilia kama vile waliofilisi shirika hilo siyo wao.

Mkuu wa Kaya umedanganywa kuhusu gharama za usafiri wa ndege Dar to Songea. Amesema kuwa ndege za kawaida zinaweza kutumia mafuta ya milioni 28 kutoka Dar to Songea lakini ndege mpya za Bombadier Q400 zitatumia mafuta ya milioni 1 tu. Mimi sio mtaalamu wa ndege lakini taarifa imenifanya kufanya utafiti kidogo

Katika kajiutafiti kangu nimegundua kiwango cha mafuta ya ndege kwa safari hakipo constant. Kinatofautiana kutokana na sababu anuai, kama vile aina ya ndege, umbali wa safari, uzito wa mzigo wa kwenye cabin, kimo kutoka usawa wa bahari, namna ya kupaa. Vyote hivi huchangia utofauti wa utumiaji wa mafuta ktk ndege.

Katika hayo tuchukue moja la aina ya ndege na hayo mengi yawe constant (under ceteris peribus). Mkuu wa Kaya amesema "ndege nyingine" zitatumia mafuta ya mil.28 kutoka Dar kwenda Songea, lakini Bombadier zetu zitatumia mafuta ya milioni 1 tu. Tuchukulie mfano wa ndege aina ya Boeing 777 yenye uwezo wa kubeba abiria hadi 450 (mara 6 zaidi ya Bombadier zetu).
Umbali wa Dar to Songea kwa barabara ni maili 655 sawa na kilomita 1,054. Lakini kwa anga ni maili 364 sawa na kilomita 585. Boeing 777 inauwezo wa kukimbia kwa speed ya maili 590 kwa saa, sawa na kilomita 949 kwa saa. Kwahiyo ikisafiri kutoka Dar to Songea (kilomita 585) itatumia mwendo wa dakika 36 tu.
www.distancecalculator.net

Mafuta ya ndege hupimwa kwa galoni (US Liquid gallon) ambapo galoni moja ni sawa na lita 3.7 za ujazo. Boeing 777 inatumia galoni 14.4 za mafuta kwa injini moja kwa dakika (1 lg/engine/minute). Boeing 777 ina injini mbili za "Rolls Royce trent 892" zinazotumia galoni 28.8 za mafuta kwa dakika moja (ingia hapa ). Hivyo basi kwa dakika 36 itakazotumia kutoka Dar to Songea itatumia galoni 1,036.
www.askcaptainlim.com

Galoni moja ya mafuta (US liquid gallon) ina lita 3.7 za ujazo. Kwahiyo galoni 1,036 ni sawa na lita 3,836. Bei ya mafuta ya ndege (jet fuel) katika soko la Marekani ni dola 1.38 kwa galoni moja kwa bei ya September 1 mwaka huu. Kwa Tanzania sijui bei ni kiasi gani, lakini tukadirie ni mara mbili ya bei ya Marekani, yani dola 2.76 kwa galoni moja ya lita 3.7.
www.flightdeckfriend.com

Kwahiyo tukitaka kujua gharama za mafuta ya Boeing 777 kutoka Dar kwenda Songea tunachukua galoni 1,036 mara dola 2.76, mara bei ya dola kwa leo ambayo ni TZS 2,182/=. Utapata Shilingi 6,239,123/=. Hii ndio gharama halisi ya mafuta ambayo Boeing 777 itatumia kutoka Dar to Songea.

Maana yake ni kwamba Boeing 777 itatumia mafuta ya milioni 6.2 kupeleka abiria 450 Songea kutokea Dar.

Sasa twende kwenye Bombadier zetu ambazo Mkuu wa Kaya amesema zinatumia mafuta ya milioni 1 tu kwa safari ya Dar - Songea. Bombadier Q400 inatumia mafuta ya milioni 1 kusafirisha abiria 75 tu kutoka Dar to Songea.
Kwahiyo kama kuna abiria 450 wa kwenda Songea, ndege ya Boeing 777 itawabeba wote na itakwenda mara moja tu kwa mafuta ya milioni 6. Lakini Bombadier itabidi iende trip 6 ndipo iweze kuwamaliza. Yani iende kwa mafuta ya milioni 1, irudi kwa mafuta ya milioni 1 (round ya kwanza), iende tena kwa mafuta ya milioni 1 na kurudi kwa mafuta ya milioni moja (round ya pili). Hadi round zote 6 ziishe Bombadier yetu itakua imetumia mafuta ya milioni 12.
Maana yake ni kwamba Bombadier itaenda round 6 na itatumia mafuta ya milioni 12, kubeba abiria walewale ambao wangebebwa na Boeing 777 mara moja tu na kwa gharama ya mafuta ya milioni 6 tu.

Inaonekana hata waliompa taarifa Mkuu wa kaya hawakufanya utafiti wa kutosha kuhusu gharama, aliposikia mafuta ya milioni 1 Dar to Songea akaona ni gharama ndogo kumbe ndege pia inabeba abiria wachache.
Calculation ya gharama za mafuta lazima ziende sambamba na idadi ya abiria. .

ALIYEMDANGANYA MKUU WA KAYA AADHIBIWE....

NAIPENDA TANZANIA NAWACHUKIA WAPIGA DILI.
Mbona kama umejijibu mwenyewe sasa. Hapo kwenye aya ya 3, sababu ulizozitaja, utofauti huo nadhani ndio unafanya ndege zetu zitumie mafuta ya 1m.
Pia ndege zetu, kwenda abiria75 na ikirudi 75 jumla inakua ni abiria 150. Kwahiyo nenda rudi 3 ni abiria 450.
 
Hivi zile ndege za EAA kama vile VC10...DC9....DAKOTA ziko wapi...????
 
Hapa nazungumzia abiria 450 waliopo Dar na wanaenda Songea
Sasa zungumzia kwenda tu, sababu hata Boeing lazima nayo itarudi tu.
Au hakunaga abiria wa kutoka Songea kurudi Dar es Salaam??
 
Hao abiria 400+ wanaokwenda Songea ni kina nani? Tumia akili hii nyepesi: Why send a nearly empty Boeing to Songea when a Bombardier could fit the purpose? Tatizo lenu sio ndege, ingekuwa kubwa mngeponda, sasa ni ndogo mnaponda. Mbona hamzungumzii mabehewa mapya ya kuifufua Reli ya Kati? Acheni siasa za chuki
Note:Mtoa mada,amahakiki tu kimahesabu kuwa boing 777 hutumia mil 6 na si 28 kama walivyomueleza mkuu wa kaya na amechanganua zaidi kama kuna idadi kubwa ya watu Boeing ina gharama nafuu ya uendeshaji si chuki bali ni maelekezo
 
Kuna fact nimeongezea zisome ili unielewe.
 
Kwahiyo wewe ulitaka tununue Boeing 777 kwa safari ya Songea?

Unachekesha sana. Hao abiria 450 wa kwenda Songea wapo wapi? Halafu huo uwanja wa Songea unaweza kupokea Boeing 777?

Umeandika ngonjera nyingi kweli lakini hayo maswali mawili hujayajibu! Labda uandike tena..
 
Mbona kama umejijibu mwenyewe sasa. Hapo kwenye aya ya 3, sababu ulizozitaja, utofauti huo nadhani ndio unafanya ndege zetu zitumie mafuta ya 1m.
Pia ndege zetu, kwenda abiria75 na ikirudi 75 jumla inakua ni abiria 150. Kwahiyo nenda rudi 3 ni abiria 450.

Kuna fact nimeongezea, ukisoma utanielewa
 
Sasa zungumzia kwenda tu, sababu hata Boeing lazima nayo itarudi tu.
Au hakunaga abiria wa kutoka Songea kurudi Dar es Salaam??

Kuna fact nimeongezea, ukisoma utanielewa
 
Note:Mtoa mada,amahakiki tu kimahesabu kuwa boing 777 hutumia mil 6 na si 28 kama walivyomueleza mkuu wa kaya na amechanganua zaidi kama kuna idadi kubwa ya watu Boeing ina gharama nafuu ya uendeshaji si chuki bali ni maelekezo
Asante kwa kunielewa Mkuu

Kuna fact nimeongezea, ukisoma utanielewa zaidi
 
Mkuu umefanya analysis nzuri lakini hukumalizia ndio maana utapata critism nyingi. ungefanya kitu kimoja ungekata mzizi wa fitna

moja ungeafanya cost analysis kwa abiria mmoja ndege ikiwa imejaa (fully capacity), ikiwa na abiria (50% capacity) na ikiwa na abiria 25% inakuaje. hii itamaliza kabisa fitna yeyote
Mkuu kuna kitu nimeongezea pale pitia kwenye uzi utanielewa.
 
Back
Top Bottom