Nani amemdanganya Mkuu wa Kaya?

Nani amemdanganya Mkuu wa Kaya?

Hao abiria 400+ wanaokwenda Songea ni kina nani? Tumia akili hii nyepesi: Why send a nearly empty Boeing to Songea when a Bombardier could fit the purpose? Tatizo lenu sio ndege, ingekuwa kubwa mngeponda, sasa ni ndogo mnaponda. Mbona hamzungumzii mabehewa mapya ya kuifufua Reli ya Kati? Acheni siasa za chuki
Sasa vp siku wakiwepo abiria 450 wa kwenda Songea? msaidieni Juma apunguze kuzomoka anatuaibisha!
 
hii picha ina inazungumza mengi mambo si mambo umejifunza nini hapa.
View attachment 410241
swissme
"Mh majaliwa nenda dodoma hata kama nyumba yako haijakamilika.. Ili akina mbowe na vichaa wenzake kina lissu wasipate cha kuongea.. Na kama kuna watu wanataka kuleta michango ya tetemeko waambie wakuletee dodoma... "
Mh Majaliwa "mkuu kwani siwezi kuondoka na bombadia? Natamani niizindue .. Wanadodoma nao wakaione"
JPM.. " Bombadia hazina mafuta .. Zitaanza kutumika mwaka wa bajeti ujao.. We tangulia dodoma ili tuwaoneshe sisi ni watu wa kazi tu"
 
Awali ya yote nichukue fursa hii kumpongeza Mkuu wa Kaya yetu kwa moyo wake wa kizalendo wa kutuletea ndege mbili mpya ili kufufua shirika letu ambalo wenzie walilitafuna na kulifilisi. Japo haohao ndio wanaomshangilia kama vile waliofilisi shirika hilo siyo wao.

Mkuu wa Kaya umedanganywa kuhusu gharama za usafiri wa ndege Dar to Songea. Amesema kuwa ndege za kawaida zinaweza kutumia mafuta ya milioni 28 kutoka Dar to Songea lakini ndege mpya za Bombadier Q400 zitatumia mafuta ya milioni 1 tu. Mimi sio mtaalamu wa ndege lakini taarifa imenifanya kufanya utafiti kidogo

Katika kajiutafiti kangu nimegundua kiwango cha mafuta ya ndege kwa safari hakipo constant. Kinatofautiana kutokana na sababu anuai, kama vile aina ya ndege, umbali wa safari, uzito wa mzigo wa kwenye cabin, kimo kutoka usawa wa bahari, namna ya kupaa. Vyote hivi huchangia utofauti wa utumiaji wa mafuta ktk ndege.

Katika hayo tuchukue moja la aina ya ndege na hayo mengi yawe constant (under ceteris peribus). Mkuu wa Kaya amesema "ndege nyingine" zitatumia mafuta ya mil.28 kutoka Dar kwenda Songea, lakini Bombadier zetu zitatumia mafuta ya milioni 1 tu. Tuchukulie mfano wa ndege aina ya Boeing 777 yenye uwezo wa kubeba abiria hadi 450 (mara 6 zaidi ya Bombadier zetu).
Umbali wa Dar to Songea kwa barabara ni maili 655 sawa na kilomita 1,054. Lakini kwa anga ni maili 364 sawa na kilomita 585. Boeing 777 inauwezo wa kukimbia kwa speed ya maili 590 kwa saa, sawa na kilomita 949 kwa saa. Kwahiyo ikisafiri kutoka Dar to Songea (kilomita 585) itatumia mwendo wa dakika 36 tu.
www.distancecalculator.net

Mafuta ya ndege hupimwa kwa galoni (US Liquid gallon) ambapo galoni moja ni sawa na lita 3.7 za ujazo. Boeing 777 inatumia galoni 14.4 za mafuta kwa injini moja kwa dakika (1 lg/engine/minute). Boeing 777 ina injini mbili za "Rolls Royce trent 892" zinazotumia galoni 28.8 za mafuta kwa dakika moja (ingia hapa ). Hivyo basi kwa dakika 36 itakazotumia kutoka Dar to Songea itatumia galoni 1,036.
www.askcaptainlim.com

Galoni moja ya mafuta (US liquid gallon) ina lita 3.7 za ujazo. Kwahiyo galoni 1,036 ni sawa na lita 3,836. Bei ya mafuta ya ndege (jet fuel) katika soko la Marekani ni dola 1.38 kwa galoni moja kwa bei ya September 1 mwaka huu. Kwa Tanzania sijui bei ni kiasi gani, lakini tukadirie ni mara mbili ya bei ya Marekani, yani dola 2.76 kwa galoni moja ya lita 3.7.
www.flightdeckfriend.com

Kwahiyo tukitaka kujua gharama za mafuta ya Boeing 777 kutoka Dar kwenda Songea tunachukua galoni 1,036 mara dola 2.76, mara bei ya dola kwa leo ambayo ni TZS 2,182/=. Utapata Shilingi 6,239,123/=. Hii ndio gharama halisi ya mafuta ambayo Boeing 777 itatumia kutoka Dar to Songea.

Maana yake ni kwamba Boeing 777 itatumia mafuta ya milioni 6.2 kupeleka abiria 450 Songea kutokea Dar.

Sasa twende kwenye Bombadier zetu ambazo Mkuu wa Kaya amesema zinatumia mafuta ya milioni 1 tu kwa safari ya Dar - Songea. Bombadier Q400 inatumia mafuta ya milioni 1 kusafirisha abiria 75 tu kutoka Dar to Songea.
Kwahiyo kama kuna abiria 450 wa kwenda Songea, ndege ya Boeing 777 itawabeba wote na itakwenda mara moja tu kwa mafuta ya milioni 6. Lakini Bombadier itabidi iende trip 6 ndipo iweze kuwamaliza. Yani iende kwa mafuta ya milioni 1, irudi kwa mafuta ya milioni 1 (round ya kwanza), iende tena kwa mafuta ya milioni 1 na kurudi kwa mafuta ya milioni moja (round ya pili). Hadi round zote 6 ziishe Bombadier yetu itakua imetumia mafuta ya milioni 12.
Maana yake ni kwamba Bombadier itaenda round 6 na itatumia mafuta ya milioni 12, kubeba abiria walewale ambao wangebebwa na Boeing 777 mara moja tu na kwa gharama ya mafuta ya milioni 6 tu.

Inaonekana hata waliompa taarifa Mkuu wa kaya hawakufanya utafiti wa kutosha kuhusu gharama, aliposikia mafuta ya milioni 1 Dar to Songea akaona ni gharama ndogo kumbe ndege pia inabeba abiria wachache.
Calculation ya gharama za mafuta lazima ziende sambamba na idadi ya abiria. .

[emoji116]
NAOMBA NIONGEZEE FACT NYINGINE KUONYESHA KUWA MKUU WA KAYA ALIDANGANYWA.

Kwa kutumia yale makadirio
1 US Gallon = 3.7 Lita

Dhamani ya Dola ni Tshs 2,182

Kwahiyo,
Kama 3.7 Lita = 2.76 US Dolla
1 Lita = 0.8 US Dolla

Kumbuka Bombadier Q400 inatumia Lita 7 @ Maili

Dar to Songea ni 364 Maili

Angalia hapa:

LITA 7 × 364 MAILI × 0.8 DOLA @ LITA × 2182 TSH (Thamani ya Shilingi @ Dola) = 4,447,788.8 TSHS

KWAHIYO;
GHARAMA YA NDEGE TULIYONUNUA KUSAFIRISHA ABIRIA 75 KUTOKA DAR - SONGEA KWA SAFARI MOJA TU NI 4,447,788.8 TSHS.

Nani alimuambia Mkuu wa Kaya ni 1,000,000 TSHS?

ALIYEMDANGANYA MKUU WA KAYA AADHIBIWE....

NAIPENDA TANZANIA NAWACHUKIA WAPIGA DILI.

Labda nijaribu kwanza kukuelewa kabla ya kuanza kujibu, hoja yako hasa ni nini? Kwamba tulipaswa tununue Boeing badla ya Bombadier, au tulipaswa tununue Ndege ya kubeba watu wengi kwanza kabla ya za wachace? Au ni nini? Naomba unisaidie hapo kuelewa pole pole ilie niweze kuchangia kikamilifu!
 
Mkuu wa kaya angesema hatununui Boeing kwa sababu hatuna viwanja, hatuna abiria wengi kwa mkupuo wanaotumia ndege, huu uzi ungekosa maana, lakini kwa sababu alikimbilia kwenye mafuta kwa umbali wa dar-songea!, ndio maana mleta uzi kafanya uchochezi kwa kigezo hicho hicho!.
Samahani Mkuu sijachochea ila nimeweka facts.
 
Kwa hiyo alidanganywa kwenye 28Mil lakini 1Million ya bombardier iko sawa?
Kwenye Million 28 alidanganywa pia 1 Million alidanganywa.

Nenda kwenye mada na usome hadi mwisho.
 
Hao abiria 400+ wanaokwenda Songea ni kina nani? Tumia akili hii nyepesi: Why send a nearly empty Boeing to Songea when a Bombardier could fit the purpose? Tatizo lenu sio ndege, ingekuwa kubwa mngeponda, sasa ni ndogo mnaponda. Mbona hamzungumzii mabehewa mapya ya kuifufua Reli ya Kati? Acheni siasa za chuki

Shida yake kubwa ni jina, anataka ndege yetu iitwe Boeng au Airbus hata kama ingekuwa ni kubeba abiria 5 na ingeitwa Boieng au Airbus asingekuwa na shida ni kama vile mtu anataka nembo ya kiatu kama hakiitwi adidas basi siyo kiatu, hao ndiyo Waafrika!
 
Tatizo ni la mtoa mada kufanya hesabu za kawaida (kutoa na kujumlisha) kumkosoa Mkuu wa Kaya pasipo kujua uamuzi wa kuwekeza kimaendeleo ni suala la kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiteknolojia
Soma vizuri mada yangu, sijamkosoa Mkuu wa Kaya bali nimewakosoa wale waliompa taarifa za uongo ili waadhibiwe.
 
Kwa kiasi kikubwa hesabu zako zaweza kuwa sawa... Ila je ni wangapi wapanda ndege kutoka Dar to Songea?

Viwanja vina accomodate hizo boeing 777??

Hiyo bombadier yenyewe yaweza kwenda mswaki na ndo ndege ndogo ya abiria 75 tu.... Alafu wewe unataka ziletwe boeing 777

Subiri kwanza itengenezwe miundombinu ndo zitakuja hizo 777....
Target yangu ni kuonyesha kudanganywa kwa 20 milion na 1 milion
 
Awali ya yote nichukue fursa hii kumpongeza Mkuu wa Kaya yetu kwa moyo wake wa kizalendo wa kutuletea ndege mbili mpya ili kufufua shirika letu ambalo wenzie walilitafuna na kulifilisi. Japo haohao ndio wanaomshangilia kama vile waliofilisi shirika hilo siyo wao.

Mkuu wa Kaya umedanganywa kuhusu gharama za usafiri wa ndege Dar to Songea. Amesema kuwa ndege za kawaida zinaweza kutumia mafuta ya milioni 28 kutoka Dar to Songea lakini ndege mpya za Bombadier Q400 zitatumia mafuta ya milioni 1 tu. Mimi sio mtaalamu wa ndege lakini taarifa imenifanya kufanya utafiti kidogo

Katika kajiutafiti kangu nimegundua kiwango cha mafuta ya ndege kwa safari hakipo constant. Kinatofautiana kutokana na sababu anuai, kama vile aina ya ndege, umbali wa safari, uzito wa mzigo wa kwenye cabin, kimo kutoka usawa wa bahari, namna ya kupaa. Vyote hivi huchangia utofauti wa utumiaji wa mafuta ktk ndege.

Katika hayo tuchukue moja la aina ya ndege na hayo mengi yawe constant (under ceteris peribus). Mkuu wa Kaya amesema "ndege nyingine" zitatumia mafuta ya mil.28 kutoka Dar kwenda Songea, lakini Bombadier zetu zitatumia mafuta ya milioni 1 tu. Tuchukulie mfano wa ndege aina ya Boeing 777 yenye uwezo wa kubeba abiria hadi 450 (mara 6 zaidi ya Bombadier zetu).
Umbali wa Dar to Songea kwa barabara ni maili 655 sawa na kilomita 1,054. Lakini kwa anga ni maili 364 sawa na kilomita 585. Boeing 777 inauwezo wa kukimbia kwa speed ya maili 590 kwa saa, sawa na kilomita 949 kwa saa. Kwahiyo ikisafiri kutoka Dar to Songea (kilomita 585) itatumia mwendo wa dakika 36 tu.
www.distancecalculator.net

Mafuta ya ndege hupimwa kwa galoni (US Liquid gallon) ambapo galoni moja ni sawa na lita 3.7 za ujazo. Boeing 777 inatumia galoni 14.4 za mafuta kwa injini moja kwa dakika (1 lg/engine/minute). Boeing 777 ina injini mbili za "Rolls Royce trent 892" zinazotumia galoni 28.8 za mafuta kwa dakika moja (ingia hapa ). Hivyo basi kwa dakika 36 itakazotumia kutoka Dar to Songea itatumia galoni 1,036.
www.askcaptainlim.com

Galoni moja ya mafuta (US liquid gallon) ina lita 3.7 za ujazo. Kwahiyo galoni 1,036 ni sawa na lita 3,836. Bei ya mafuta ya ndege (jet fuel) katika soko la Marekani ni dola 1.38 kwa galoni moja kwa bei ya September 1 mwaka huu. Kwa Tanzania sijui bei ni kiasi gani, lakini tukadirie ni mara mbili ya bei ya Marekani, yani dola 2.76 kwa galoni moja ya lita 3.7.
www.flightdeckfriend.com

Kwahiyo tukitaka kujua gharama za mafuta ya Boeing 777 kutoka Dar kwenda Songea tunachukua galoni 1,036 mara dola 2.76, mara bei ya dola kwa leo ambayo ni TZS 2,182/=. Utapata Shilingi 6,239,123/=. Hii ndio gharama halisi ya mafuta ambayo Boeing 777 itatumia kutoka Dar to Songea.

Maana yake ni kwamba Boeing 777 itatumia mafuta ya milioni 6.2 kupeleka abiria 450 Songea kutokea Dar.

Sasa twende kwenye Bombadier zetu ambazo Mkuu wa Kaya amesema zinatumia mafuta ya milioni 1 tu kwa safari ya Dar - Songea. Bombadier Q400 inatumia mafuta ya milioni 1 kusafirisha abiria 75 tu kutoka Dar to Songea.
Kwahiyo kama kuna abiria 450 wa kwenda Songea, ndege ya Boeing 777 itawabeba wote na itakwenda mara moja tu kwa mafuta ya milioni 6. Lakini Bombadier itabidi iende trip 6 ndipo iweze kuwamaliza. Yani iende kwa mafuta ya milioni 1, irudi kwa mafuta ya milioni 1 (round ya kwanza), iende tena kwa mafuta ya milioni 1 na kurudi kwa mafuta ya milioni moja (round ya pili). Hadi round zote 6 ziishe Bombadier yetu itakua imetumia mafuta ya milioni 12.
Maana yake ni kwamba Bombadier itaenda round 6 na itatumia mafuta ya milioni 12, kubeba abiria walewale ambao wangebebwa na Boeing 777 mara moja tu na kwa gharama ya mafuta ya milioni 6 tu.

Inaonekana hata waliompa taarifa Mkuu wa kaya hawakufanya utafiti wa kutosha kuhusu gharama, aliposikia mafuta ya milioni 1 Dar to Songea akaona ni gharama ndogo kumbe ndege pia inabeba abiria wachache.
Calculation ya gharama za mafuta lazima ziende sambamba na idadi ya abiria. .

[emoji116]
NAOMBA NIONGEZEE FACT NYINGINE KUONYESHA KUWA MKUU WA KAYA ALIDANGANYWA.

Kwa kutumia yale makadirio
1 US Gallon = 3.7 Lita

Dhamani ya Dola ni Tshs 2,182

Kwahiyo,
Kama 3.7 Lita = 2.76 US Dolla
1 Lita = 0.8 US Dolla

Kumbuka Bombadier Q400 inatumia Lita 7 @ Maili

Dar to Songea ni 364 Maili

Angalia hapa:

LITA 7 × 364 MAILI × 0.8 DOLA @ LITA × 2182 TSH (Thamani ya Shilingi @ Dola) = 4,447,788.8 TSHS

KWAHIYO;
GHARAMA YA NDEGE TULIYONUNUA KUSAFIRISHA ABIRIA 75 KUTOKA DAR - SONGEA KWA SAFARI MOJA TU NI 4,447,788.8 TSHS.

Nani alimuambia Mkuu wa Kaya ni 1,000,000 TSHS?

ALIYEMDANGANYA MKUU WA KAYA AADHIBIWE....

NAIPENDA TANZANIA NAWACHUKIA WAPIGA DILI.
Umejtahidi kuweka analysis nzuri. ila ni too a
 
Wewe ni Malisa? Kama sio basi umekopi post ya Malisa huko Facebook ukaileta hapa na kibaya zaid unashindwa hata kuitetea zaid ya ''Am much better''edit post yako uonyeshe heshima kwa muandishi mbona naona watu wanakuuliza maswali yasiyolingana na akili yako
Punguza jazba nenda kwenye Original topic utaona.
 
Hoja yako inaweza kuwa na substance. Lakini jee tunao abiria 450 wa kupanda Boeing 777 kwenda Songea Kwa wakati mmoja? Nadhani walimshauri Mkuu wa Kaya waliangalia vigezo kadhaa ikiwemo ulichokijengea hoja.

Kama route ya songea siyo viable kwa nini kupeleka ndege kule wakati maeneo mengi yana uwezo wa kufanya vizuri kwa biashara ya usafiri wa anga? Kuna nini huko Songea cha kulazimisha ndege mtoto kwenda kule?
 
Labda nijaribu kwanza kukuelewa kabla ya kuanza kujibu, hoja yako hasa ni nini? Kwamba tulipaswa tununue Boeing badla ya Bombadier, au tulipaswa tununue Ndege ya kubeba watu wengi kwanza kabla ya za wachace? Au ni nini? Naomba unisaidie hapo kuelewa pole pole ilie niweze kuchangia kikamilifu!
Hoja yangu siyo ndege ipi tungenunua bali ni nani aliyempa Mkuu wa Kaya takwimu za uongo?
 
Mafuta ya ndege hupimwa kwa galoni (US Liquid gallon) ambapo galoni moja ni sawa na lita 3.7 za ujazo. Boeing 777 inatumia galoni 14.4 za mafuta kwa injini moja kwa dakika (1 lg/engine/minute). Boeing 777 ina injini mbili za "Rolls Royce trent 892" zinazotumia galoni 28.8 za mafuta kwa dakika moja (ingia hapa ). Hivyo basi kwa dakika 36 itakazotumia kutoka Dar to Songea itatumia galoni 1,036.

mkuu unajua consumption ya mafuta kwa engine ya boeing au umekurupuka, hizo galoni 14.4 ulizoandika hazitoshi hata nusu dakika
 
Soma vizuri mada yangu, sijamkosoa Mkuu wa Kaya bali nimewakosoa wale waliompa taarifa za uongo ili waadhibiwe.
Nadhani hujapitia bandiko zangu kuhusu mada yangu. Tatizo ni hesabu yako.
 
Hoja yangu siyo ndege ipi tungenunua bali ni nani aliyempa Mkuu wa Kaya takwimu za uongo?

Basi kama hiyo ndiyo hoja yako na nimerudia tena kukusoma nafikiri una matatizo ya uelewa, labda nikuulize mfano wa Dar -Songea kuna demand gani ya kubeba abiria zaidi ya 400 kwa mara moja? Kama mashirika makubwa ya ndege yana struggle kujaza Airbus ya watu 200-300 ktk Ulaya mpka Afrika iweje upate abiria 400 wa raundi moja ktk Dar-Songea, au Mkoa wowote ule wa TZ?
 
Punguza jazba nenda kwenye Original topic utaona.
Jazba gani? Wakati post yenyewe ina title la mtu mwingine na ndio maana kile ulichoongeza ungesema ni wewe na post ni ya mtu mwingine kuonyesha heshima kwani yule muandishi anayo official page yake kule na maandiko yake lazima yatumike kwa kuonyesha heshima yake
 
Hoja yako inaweza kuwa na substance. Lakini jee tunao abiria 450 wa kupanda Boeing 777 kwenda Songea Kwa wakati mmoja? Nadhani walimshauri Mkuu wa Kaya waliangalia vigezo kadhaa ikiwemo ulichokijengea hoja.
Kama hakuna Abiria basi ndege hizo Ni mapambo Tuu..na hazina umuhimu wowote..
 
Back
Top Bottom