Nani aliyesema mafisadi wanaweza kutaka kiongozi mwenye kuwadhibiti? Kati yao, nani atake tena kiongozi kama Magufuli?

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
1,939
4,119
Siku zote fisadi ni kama mtu kipofu asiyeelewa wala kujua kama naye ni mtu wa kufa kama ilivyo kwa wengine

Kazi kubwa kwao ni kuiba na kukusanya mali pasipo kujua uhalali wa makusanyo hayo, kwa bahati mbaya kabisa, hata wakiwa navyo vyote, bado watataka na kingine kutoka mahali popote na kwa gharama zozote

Mtu kama huyo, aweza vipi kutaka kutawaliwa na mtu mwenye kumzuia asifanye hicho?

Mtu kama huyo, atakubaliana vipi na kiongozi mwenye huluka ya kina Magufuli ambaye hatakubali uchotwaji wa kodi za Watanzania na kujimilkisha mali pasipo uhalali?

Hata ukiniamsha usiku wa manane ukaniuliza, ni kina nani walikuwa kwenye vita kali na JPM ya ama yeye ama wao ni mafisadi including na wanufaika wa watumishi hewa, vyeti feki pia, hawa ndio walioongoza kumchukia Magufuli na mpaka leo hawana hamu na jina lake

Ni ujinga kuamishwa na watu hawa eti Magufuli alikuwa kiongozi mbaya, mtu ambaye alifanya mambo mengi na makubwa na ya kushangaza kwenye nchi hii na kwa muda mfupi? Wataendelea kuwa wale wale na bahati mbaya hawajaweza na hawataweza kuwashawishi na wengine waamini huo msimamo na uwongo wao, kwa bahati mbaya kabisa, kila mwananchi hakuambiwa tazama, waliona, na waliyaishi mazuri yake na mpaka sasa bado wanajivunia!

Mambo aliyofanya Magufuli yanafahamika vema na kila mtanzania

Mafisadi kila leo wamekuwa wakijaribu kuwaaminisha wananchi kwamba, Magufulì hakuwa lolote, wakati huo huo kwa sasa ndio wanapiga pesa na kutapika maneno yao hayo mbofu mbofu

Kama Mungu aishivyo, Bado Watanzania wenye nia njema na nchi hii, Mungu atawapatia tena kiongozi mwenye kuchukia dhuluma na kuwadhibiti majangili ya nchi hii
 
"...amefanta mambo mengi, makubwa na ya kushangaza katika nchi hii na kwa muda mfupi mno.."

Huu 👆👆 msemo huwa unanikera sana.

Kwa sababu hata mkiulizwa hayo mambo ni yapi mtaishia kusema barabara na madaraja.

Lakini mnasahau ule msemo wa vyuma kukaza cement kupanda bei, watu kupotea, fedha kuadimika, biashara kufungwa n.k.

Hivi barabara ina faida gani iwapo huna hela ya kununulia gari?

Daraja linakufaidisha nini iwapo huna nauli ya kupita?

Acheni kumtukuza mtu kama Mungu. Mwacheni apumzike.

Mnasifia mtu kama vile tuliobaki ni wajinga tusiojielewa.
 
Huu msemo huwa unanikera sana.

Wewe ni mbwa fisadi au cheti fake!
Naomba bila kupepesa Macho nikupe za USO!
 
"...amefanta mambo mengi, makubwa na ya kushangaza katika nchi hii na kwa muda mfupi mno.."

Huu 👆👆 msemo huwa unanikera sana.

Kwa sababu hata mkiulizwa hayo mambo ni yapi mtaishia kusema barabara na madaraja.

Lakini mnasahau ule msemo wa vyuma kukaza cement kupanda bei, watu kupotea, fedha kuadimika, biashara kufungwa n.k.

Hivi barabara ina faida gani iwapo huna hela ya kununulia gari?

Daraja linakufaidisha nini iwapo huna nauli ya kupita?

Acheni kumtukuza mtu kama Mungu. Mwacheni apumzike.

Mnasifia mtu kama vile tuliobaki ni wajinga tusiojielewa.
Nani aliacha kusafiri? Gari la nani alipaki

Bei ya petrol iliyopo sasa unaweza kuilinganisha na kipindi hicho?

Uko wapi wewe ambako umeme hakuna mgao?

Wewe ni fisadi? Wewe ni wale vilaza wanunua vyeti? Wewe ni wanufaikaji wa watumishi hewa?
 
Nani aliacha kusafiri? Gari la nani alipaki

Bei ya petrol iliyopo sasa unaweza kuilinganisha na kipindi hicho?

Uko wapi wewe ambako umeme hakina mgao?

Wewe ni fisadi? Wewe ni wale vilaza wanunua vyeti? Wewe ni wanufaikaji wa watumishi hewa?
None of the above.

Niliteseka since 2015 hadi 2021.

Mungu anisamehe kwa kweli niliumia sana. Mungu ni shahidi wa haya.

Wala wewe sikulazimishi kuamini.
 
Mlipe kodi bila kusukumwa, acheni kulimbikiza kodi, lipa kwa hiari, ipende nchi yako, toa risti ukiuza, acha ujanja ujanja

Na hata sasa akija kiongozi mwenye kufuatilia mambo ya dhulumati, bado utateseka kwa sababu hutaki kuishi kwa haki
 
Ivi una mradi wa SGR, Bwawa la mwalimu Nyerere, Nyumba za magereza, Madaraja, hostel za vyuo n.k unategemea kwa uzalishaji wa Cement Nchini na matumizi yaliyo ongezeka ya Cement katika miradi Bado bei ingebaki vilevile!!
Jpm inawezekana alikua na shida zake upande flani ila Mwamba alipambana kwa akili na nguvu zake zote.

Kwasasa amepumzika na wengine wafanye kwa akili na uwezo wao kadri Mungu atakavyo wajaalia.
 
Jamaa hana ajualo, ufisadi ni upofu mkubwa huwezi kuona chema kwa anayekufanya uishi kwa haki
 
Mlipe kodi bila kusukumwa, acheni kulimbikiza kodi, lipa kwa hiari, ipende nchi yako, toa risti ukiuza, acha ujanja ujanja

Na hata sasa akija kiongozi mwenye kufuatilia mambo ya dhulumati, bado utateseka kwa sababu hutaki kuishi kwa haki
Wewe una utoto mwingi na kwa kuwa upo nyuma ya keyboard huwezi kuelewa
 
..Mafisadi pia hawapendi KATIBA BORA inayodhibiti madaraka yao.

..Pia hawapendi BUNGE na MAHAKAMA zinazofanya maamuzi bila kuingiliwa.

..Zaidi hawapendi TUME HURU ya uchaguzi.
 
"...amefanta mambo mengi, makubwa na ya kushangaza katika nchi hii na kwa muda mfupi mno.."

Huu 👆👆 msemo huwa unanikera sana.

Kwa sababu hata mkiulizwa hayo mambo ni yapi mtaishia kusema barabara na madaraja.

Lakini mnasahau ule msemo wa vyuma kukaza cement kupanda bei, watu kupotea, fedha kuadimika, biashara kufungwa n.k.

Hivi barabara ina faida gani iwapo huna hela ya kununulia gari?

Daraja linakufaidisha nini iwapo huna nauli ya kupita?

Acheni kumtukuza mtu kama Mungu. Mwacheni apumzike.

Mnasifia mtu kama vile tuliobaki ni wajinga tusiojielewa.
Isitoshe, hata wakitaja hivyo, mbkna vimejengwa sana tu na kikwete?!!!!
 
None of the above.

Niliteseka since 2015 hadi 2021.

Mungu anisamehe kwa kweli niliumia sana. Mungu ni shahidi wa haya.

Wala wewe sikulazimishi kuamini.
kindeena kya mburu au ichoondi? Ila mtu asikulazimishe ukubali kila kitu. Hata mimi jiwe naona alizingua vingi.
 
Back
Top Bottom