Kwani Magufuli Alikuwa Nani?

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,032
3,911
Habari za wakati huu?

Kwanza nianze kwa kusema kwamba mimi binafsi nilikuwa muumini mkubwa kabisa wa sera za Magufuli lakini nilikuwa mkosoaji mkubwa sana wa Mtindo wake wa uongozi.Kama mdau wa elimu ya siasa huwa sipendi kutenganisha Sera za Kiongozi na Mtindo wa kiongozi lakini huwa najua kabisa kwa imethibitishwa kwamba Sera nzuri bila uongozi mzuri ni matatizo na Uongozi mzuri bila sera nzuri nayo pia ni matatizo.

Tangu tupate uhuru,Tanzania na Afrika kwa ujumla na hata maeneo mengi duniani yamekuwa na ukosefu wa muendano wa Sera nzuri na Uongozi mzuri.

Lengo la mjadala huu ni kuchokozi swala lenye lengo la kuandika kitabu cha kutaka kuwajibu waandishi nguli ambao wameandika kitabu cha kukosoa baadhi ya maamuzi ya Hayati Magufuli hasa yanayohusu ujenzi na maono yako dhidi ya Mji wa Chato. Ninavoandika makala hii niko safarini kuelekea katika mji wa Chato kwa lengo la kwenda kujionea hayo makosa ya Magufuli ambayo yalifanyika lakini zaidi ni kuandika Kitabu ambacho kitayaeleza katika Mwanga Chanya yale ambayo Magufuli aliyafanya katika Mji wa Chato.Ninatamani sana kupata Nakala ya Kitabu hicho cha "I am the State" ili ninapoandika cha kuyapinga yale yaliyomo basi niweze kuwajiba katika mtiririko sahihi.

Je, Magufuli alikuwa Ni nani?

Magufuli alikuwa ni Mtanzania, kiongozi wa kitanzania ambaye aliingia katika uongozi na kulelewa katika siasa za Tanzania.Magufuli hakutoka nje ya Tanzania na wala hakutoka nje ya Mfumo wa Tanzania.Kama ambavyo Nyerere,Mwinyi,Mkapa na Kikwete ambavyo walitawala nchi hii kwa awamo zao na kufanya yale waliyoweza kuyafanya kwa kadiri ya uwezo wao Ndivyo hivyo Magufuli alivyoingi Madarakani na kuongoza kwa kipindi chake?

Lakin Je Magufuli ni Nani?au alikuwa ni Nani?Je ni kweli Magufuli alikuwa mtu ambaye tumeelezwa katika vyomba vya havari baada ya kuondoka kwake.Hasa wale ambao wanalengo la kumuweka Magufuli kama Mwovu,Mbinafsi,Mlafi na Mchoyo?Au kama ambavyo waandishi wa kitabu cha I am State walivyoamua kutuambia kwamba yeye alikuwa Juu ya Wote?

Nachelea kusema kwamba binafsi sikubaliani Na waandishi hawa wa hichi kitabu,pamoja na kwamba sijabahatika kukisoma kitabu hicho lakini swala la wao kujaribu kuiandika historia ya Magufuli bila kutambua kwamba tulikuwepo, tuliona na tulisikia yale yote ambayo alisema na kutenda katika kipindi chake cha uongozi ni jambo la kushangaza sana. Waandishi hawa walipaswa kutambua kwamba wanachoandika sio Matokeo ya historia ambayo walioiona wamekufa hapana,Tupo HAI tuliona Makosa ya Magufuli lakini pia tuliona Uzuri wake.Waswahili husema "Uzuri wa mkakasi ndani yake Mti" na wengine pia husema Baniani Mbaya kiatu chake dawa' ama Mnyonge Mnyongeni ila haki yake Mpeni"

Sidhani kama waandishi wa kitabu hiki walizingatia weledi katika kuweka historia hii sawa ndio maana Mimi binafsi nimeamua kuchukua hatua ya kwenda Chato nikauone huo ubaya wa Magufuli kwa kujenga lami na kutaka kuiendeleza Chato kiasi cha kutaka kutuaminisha kwamba kilikuwa ni kitendao cha kishetani zaidi kuwahi kutokea hapa duniani.

Sitaki kusema mengi leo ila nitarejea hapa jukwaani Muswada wa kitabu ukikamilika na huenda Nikakitoa kwa Nakala Laini(Softy Copy ila kila mtu asome na kuelewa Ukweli kwamba Magufuli Hakuwa Mkamilifu lakini katika udhaifu wake alijitahidi kutenda kadiri ya Uwezo wake.
 
Back
Top Bottom