Namshauri Dkt. Tulia amsamehe kiongozi mkubwa aliyetaka ashindwe Urais wa IPU

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu Watanzania,

Nikiri wazi kuwa mimi ni mtu niliye jipambambanua waziwazi bila kificho kumuunga mkono kwa moyo wangu wote Dr Tulia kutokana na utendaji kazi wake mzuri, uchapa kazi wake, moyo wake wa huruma, upendo, unyenyekevu, ukarimu na usikivu mkubwa sana kwa wananchi mbalimbali bila kujali itikadi za kisiasa, hali ya mtu pamoja na uwezo wake mkubwa wa kiuongozi na upeo mkubwa alio nao.

Nitaendelea kumuunga mkono na kumuombea kila la heri bila kuchoka wala kukata Tamaa wala kuona aibu kwa kuwa maisha yake ya kibunge yameleta nuru, matumaini na Tabasamu kwa watu wengi sana nyanda za juu kusini.

Ndugu zangu sote tumeisikia hotuba fupi ya Dr Tulia punde tu aliporejea nyumbani kutoka nchini Angola. Ni hotuba fupi lakini yenye kubeba hisia kali sana, upendo kwa Taifa lake na shukurani kwa Taifa lake zima kwa maombi makubwa aliyokuwa akiombewa kutoka kila kona.

Maombi na ushirikiano ulioongozwa na Amiri jeshi mkuu wetu mama Samia Suluhu Hasssan aliyempigania kwa kutumia ushawishi wake kuwaomba serikali zingine ziwaombe na kuwasihi wabunge wake wampigie kura mwanae Dr. Tulia Acksoni mwansasu katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya Urais wa IPU.

Katikati ya hotuba hiyo ya kihistoria na yenye kugusa mioyo ya watu dada yetu Dr. Tulia kwa hisia kali, uchungu, masikitiko, akaeleza juu ya Watanzania wenzetu waliokosa uzalendo kwa Taifa letu waliweza kuandika mitandaoni ujumbe kwenda kwa wajumbe ili asichaguliwe.

Tulia alienda mbali kuwa yupo mmoja kiongozi mkubwa naye aliingia katika mchezo huo mchafu na wenye kukosa uzalendo kwa Taifa letu wa kutaka kumkwamisha, na kusema kuwa ameagiza wasaidizi wake wamtafute huyo mmoja tu ili pengine ajifunze au ajuwe wapi anakosea ajirekebishe au kosa lake nini.

Sasa ningependa kumshauri Dada yangu Dr. Tulia kwa moyo wa unyenyekevu, upendo na dhamira njema kabisa kutoka katika sakafu ya moyo wangu kuwa sisi wakristo tunasema kuwa sisi binadamu au wanadamu siyo wakamilifu, siyo malaika na siyo miungu watu.

Sisi ni binadamu tunakosea na kukosewa, hatuwezi kupendwa na kila mtu wala kukubalika na kila mtu wala kuungwa mkono na kila mtu hata kama tupo tunapeperusha bendera ya Taifa. Kutofautiana ni jambo la kawaida katika masuala ya kisiasa.

Kumbuka hata marehemu Benard Membe amewahi kulalamika kuwa alinyimwa ushirikiano kutoka mamlaka ya juu pale alipotaka kuwainia nafasi ya juu katika jumuiya ya madola, lakini alisamehe na kusonga mbele na maisha yakaendelea.

Dada yangu Dr. Tulia uongozi unatoka kwa Mungu mwenyewe na siyo mwanadamu, imeandikwa amelaaniwa yule amtumainiye na kumtegemea mwanadamu kuwa kinga yake.

Ushindi wako haujatoka kwa wanadamu bali kwa Mungu ambaye ndiye aliyekutengenezea njia na kukuchorea Ramani ya ushindi wako.

Yeye ndiye amekufikisha hapo, huo ndio ulikuwa wakati wako uliopangwa na Mungu. Kama Mungu hayupo upande wako mwanadamu afanya kazi bure hata angekesha anakuombea kura.

Nani alijuwa hayati Dr. John Pombe Joseph Magufuli angepenya mbele ya Mh Edward Ngoyai Lowassa katika kura za maoni ndani ya CCM? Nani alikuwa anakubalika na wajumbe wa CCM kama Lowassa?

Nani angempita lowasa 2015 kama jina lake lingetua mkutano mkuu wa CCM kupigiwa kura? Nani angemzui? Kwa kutumia kalamu ipi? Ya wino wa rangi ipi? Unajifunza nini hapa dada yangu? Jibu ni kuwa kama Mungu ameufanya wakati uwe upande wako basi hakuna mwanadamu awezaye kukuzui, hivyo unapaswa kumsamehe kila mtu na kusherehekea ukuu wa Mungu juu yako.

Samehe dada yangu,fungua moyo dada yangu, achilia wote moyoni mwako waliokuumiza, kukutesa, kukupa maumivu.

Hawajakukomesha bali wamekuimarisha, wamekufanya kuwa bora zaidi ya awali, wamekukomaza, wamekufanya uwajuwe nani wapo upande wako, nani wanakuunga mkono, nani wanakupenda.

Wamekufanya ujuwe na utambue thamani yako kwa watu ipoje, wamekufanya utambue Mungu hashindwi hata kama mwanadamu akikuombea mabaya lakini pia wamekufunulia mioyo yao kuweza kuwajuwa zaidi, wamekufanya ufahamu nani unaweza kumuamini na kumuachia glasi ya maji na ukarejea kuinywa tena baada ya kurejea.

Samehe saba mara sabini dada yangu, uongozi ni Jalala, uongozi unahitaji ngozi ngumu,uongozi unahitaji stamini ya kifua, uvumilivu, subira, busara, hekima, upendo, unyenyekevu na utayari wa kupokea yote bila kuyumbishwa.

Huna sababu ya kumtafuta ili kujifunza kitu kutoka kwake huna cha kukifuata kutoka kwake aliye kupinga, muache maana ushindi wako umemmaliza na kuangamiza nafsi yake angali yu hai.

Wewe jifunze kutoka kwa washindi, jifunze kutokana na mitihani unayopitia ikiwepo huu wa kupingwa na huyo kiongozi, jifunze kutoka katika kila hatua upitiayo. Wewe ni mshindi kwa Taifa letu, wewe ni mshindi wa wasichana wote, wewe ni mfano wa kuigwa kwa mabinti waliopo pale loleza na zanaki sekondari, wewe ni kioo cha kuigwa kwa mabinti wa pale Ivumwe sekondari au shule ya wasichana mpanda mkoani katavi. Wewe ni Nembo ya mabinti na wasichana wote wenye kupigania ndoto zao.

Muache Mungu akupiganie vita yako, vita ni ya Bwana, vita ni ya Mungu mpe nafasi Mungu akupiganie na utashinda katika kila pambano dada yangu. Siyo lazima upigane kila vita, zipo vita nyingine ushindi wako unategemea uvumilivu wako wa kukaa kimya na kuchunga tu ulimi wako na kinywa chako. Usiwape nafasi maadui zako za kukufahamu zaidi ya Mungu wako.

Samehe Dada yangu, hakuna aliye mkamilfu. Zuia na wakataze wasaidizi wako kuendelea na kazi ya kumtafuta huyo kiongozi mkubwa uliyesema unamhitaji, ushindi wako ni maumivu kwake. Wewe chapa kazi, songa mbele, endelea kuwa mnyenyekevu, safari bado ni ndefu inakuhitaji kazi yakuifaya katika kuitembea, unahitaji maombi yetu juu yako.

Nisamehe nitakapokuwa nimekukosea au kukukwaza kupitia andiko langu.nakuheshimu sana na naendelea kukuunga mkono na nitaendelea kukuombea kwa mwenyezi Mungu Akusaidie, kukupigania, kukutetea na kukulinda katika kila hatua upigayo. Mshike sana na mtumainie sana Mungu wako kuliko Mwanadamu. Maana mwanadamu hugeuka lakini Mungu hageuki ni yeye yule wa juzi, jana, leo na hata milele. Asante.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na Sauti.


Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Hivi nyie akina mama wajane kwanini mnakuwa wapuuzi hivi? fanya kazi fuga hata kuku uwe busy. Shame on you
Kwa hiyo hizo kazi unataka nije nifanyie kibarazani kwako hapo ndio ijulikane kuwa nafanya kazi ?😄😄😄😄 Mbona wewe upo hapa muda wote ukitukana matusi muda wote kama mwendawazimu? Hizo kazi unafanya muda gani?
 
Ila mwanangu hua unaandika mada ndefu halafu point ni nusu sentensi
Wala usijali ndugu yangu.unaweza kuishia unapoona pana hoja kulingana na upeo wako.vipi unaweza ukasoma mkataba wa kurasa hata mbili tu? Unaweza kusoma mwenendo wa hukumu ya aina yoyote ile iliyotolewa mahakamani kujuwa na kupata ukweli? Unaweza ukasoma kitabu nyaraka ya aina yoyote ile kama rejea kwa jambo muhimu kwa Taifa letu.
 
Back
Top Bottom