Rais Samia ni kiongozi Mwenye misimamo na Utulivu wa Kiuongozi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,327
9,748
Ndugu zangu watanzania,

Hii ni bahati ya kipekee Nchi na Taifa letu limebahatika kuipata kutoka katika uumbaji wa mwenyezi Mungu kwa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Dkt mama samia Suluhu Hasssan,kiongozi wa watu ,mpenda maendeleo,mwenye moyo wa huruma, unyenyekevu na upendo usiopimika katika mizani ya aina yoyote ile. Kiongozi anayefahamu kuwa licha ya mamlaka yake na madaraka yake makubwa kikatiba na kisheria lakini bado anaishi katika hali ya ubinadamu,bado amebakiwa na ubinadamu wake na katu na kamwe hajawahi kujifananisha na Mungu wala kujivika Umungu Mtu, katu na kamwe mama huyu na Rais huyu wa kipekee kabisa kuwahi kutokea katika Bara la Afrika hajawahi kuhitaji kuabudiwa wala kupewa utukufu apewao Mwenyezi Mungu.

Rais Samia Ni kiongozi mwenye misimamo ya hali ya juu sana kiuongozi,ni kiongozi mwenye utulivu wa kiwango cha juu sana,Ni kiongozi asiye yumba wala kuyumbishwa katika kutimiza maono yake na ndoto zake katika Taifa letu,Ni kiongozi mwenye kifua na moyo ambao ingekuwa mataifa yaliyo endelea kwa hakika lingekuwa ni somo Tosha katika madarasa ya wanafunzi wanaosomea uongozi,siasa utawala wa umma na mahusiano ya kimataifa. Rais samia ni Maktaba itembeayo ,Ni dhahabu katika uso wa Dunia ,Ni lulu Kwa Taifa,Ni almasi kwa vijana Na rejea kwa vizazi vijavyo na Ni hadhina ya Taifa.

Ndugu zangu watanzania,Tumefika hapa kama Taifa mahali tunaposifiwa hadi na mashirika ya kimataifa kutokana na ukuaji na maendeleo ya uchumi kutokana na misimamo mizuri ya kisera ya uchumi aliyo nayo Jemedari wetu Dr Samia.Utulivu wake Ndio umekuwa chachu katika maendeleo ya Taifa letu katika kila sekta.

Rais samia huwa hatishwi wala kuyumbishwa na makelele yasiyo na hoja wala mashiko,Rais samia siku zote anatazama mbele kwa mipango na mikakati maridadi na kabambe katika kulivusha na kulipaisha Taifa kiuchumi,.ndio maana amekuwa mshindi katika mioyo ya watanzania na kwa kila sekta amefanikiwa kwa kiwango cha juu.

Watanzania wenzangu mtambue yakuwa kama kiongozi usipokuwa na misimamo na kanuni unazosimamia zinazozingatia maslahi mapana ya Taifa na kuzingatia misingi ya kisheria na katiba ya nchi lazima uyumbe,lazima uyumbishwe,lazima ucheleweshwe ,lazima upoteze we muda,lazima ujazwe hasira,lazima upotezwe Dira na muelekeo wako kwa kuwa unapokuwa unaongoza Taifa kuna kuwa na watu wamekaa pembeni wanasubiri ukosee ,udondoke,ujikwae ,uvuruge na hata wakati mwingine wanaweza wakafanya hata hila ya kuchomelea mambo ili tu kutaka kukupoteza ,wapo wengine wanakuwa hata pembeni wakitamani hata kesho washike na kukalia kiti chako,wapo wengine wanakuwa wanahisi wao ndio walistahili kukalia kiti chako na siyo wewe.

Ndio maana viongozi wenye upeo mkubwa na maarifa makubwa na akili kubwa kama aliyo nayo Rais samia na misimamo yake ya kiuongozi na utulivu mkubwa wa kiuongozi pamoja na kupewa kibali na kuinuliwa na mwenyezi Mungu katu na kamwe huwezi kuwayumbisha, huwezi kuwadanganya huwezi kuwapotosha wala kuwachezea, wala kuwalaghai wala kufanya hila na usitambulikane maana ni kawaida viongozi aina ya Rais samia kuwa na Taarifa zote kiganjani pao hata kabla ya kufika eneo fulani au kusikiliza maelezo ya mtu fulani.

Viongozi aina ya Rais samia ni nadra sana kuwapata Duniani, ndio maana unaona watanzania wakiendelea kumuunga mkono Rais samia, maana wanajuwa ni lulu ,Ni zawadi ambayo huwa haipatikani kila siku na ndio maana watanzania wana itunza kwa wivu mkubwa sana na kwa heshima ya kipekee kabisa. Rais samia ni kama chemchemi katikati ya jangwa,Ni nuru katikati ya Giza ,Ni Njia katikati ya pori,Ni tumaini la vijana na nuru ya wanyonge.

Asante sana Rais samia, kwa hakika maisha yako na utumishi wako ni zawadi tosha kwa watanzania,Ni Tabasamu tosha kwa wenye uchungu na ni faraja tosha kwa wenye kukata Tamaa. Umeunda na kuongoza serikali ambayo imewatua mizigo mamilioni ya watanzania.imewatua mizigo wanafunzi ambao sasa wanasoma bure, imewatua na kuwainua migongo wakulima, imewatua mizigo wafanyabishara ambao sasa wanafungua biashara kila kona ya nchi. Asante Rais samia mama wa Taifa, mlezi wa watanzania na mboni Ya Taifa.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Wananchi hawana imani na Serikali anayoiongoza.

20141018_MAP004_0.jpg
 
Nani anataka undugu na wewe
Ndugu zako wako Kyela huko
Watanzania wote ni ndugu ndio maana unaweza kutoka katika mkoa wako na kwenda kuishi na kufanyia shughuli zako na wala usiulizwe habari za kabla lako wala Dini yako wala ukoo wako, unaweza hata kupewa chumba cha kulala ikiwa usiku utakukutia njiani na kesho yake ukapewa na kuku mkononi. Watanzania wote ni ndugu na tunaendelea kuishi kindugu.
 
Wananchi hawana imani na Serikali anayoiongoza.
Mamilioni ya watanzania wana imani kubwa sana na uongozi wa Rais samia na ndio maana wana endelea kumuunga mkono kwa nguvu zote kwa kuwa amegusa maisha yao na kuleta mabadiliko chanya katika maisha yao.
 
Fafanua Kidogo ndg..! Misimamo gani..?

Misimamo ya Kukomaza Shingo kutosikiliza Kilio cha Wananchi?

Tumemkosea nini sisi mpaka Aiuze Bandari yetu..!

Katiba imempa mamlaka Kamili juu ya Ardhi yetu..ailinde ipo chini yake kwa manufaa ya mTz ,yeye mamlaka hayo kawapa Wawekezaji wa Dubai.

Wawekezaji wakisema hapa tunapataka hata kama ni pale Magogoni yeye anakuwa hana Kauli, kweli? Tukubali tu..! Mfano tu
 
Upo Tanzania ipi ndugu Lucas mwashambwa? Hii hii ambayo DPw wamechukua ukanda wote wa Pwani wa Tanganyika kutoka Tanga hadi Mtwara pamoja na bandari zote ktk maziwa makuu ya Tanganyika ikiwemo bandari Kavu ya Isaka?

You must be kidding.

Wacha upumbavu. Jitafakari kuleta ujingaujinga hapa JF. We are tired.
 
CCM wenzako wanakushangaa, ni aina gani ya chawa wewe maana wenzio kusifu na kuabudu walishaacha siku nyingi. Watu radhi kuchagua andazi kuliko CCM ya huyu bibi.
 
Mamilioni ya watanzania wana imani kubwa sana na uongozi wa Rais samia na ndio maana wana endelea kumuunga mkono kwa nguvu zote,kwa kuwa amegusa maisha yao na kuleta mabadiliko chanya katika maisha yao.
Niliposoma huu uzi nikambuka wimbo wa Nay wa Mitego - Amkeni
 
Mahakama imeshatoa uamuzi na Taifa linasonga mbele kwa kishindoo
Hata wakati Nyerere anadai huru wa Tanganyika, mahakama hizohizo japo zilikuwa chini ya mkoloni zilitumika kuhalalisha kuwa Nyerere ni mchochezi. Lakini Nyerere hakukoma. Kwa hiyo watanganyika hawatakoma simply because mahakama za watawala zimetoa uamuzi. Siyo kirahisi namna hiyo. Site tunaoenda nchi hii, Ni yetu site lakini rusiende kihuni namna hii.
 
Ndugu zangu watanzania,

Hii ni bahati ya kipekee Nchi na Taifa letu limebahatika kuipata kutoka katika uumbaji wa mwenyezi Mungu kwa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Dkt mama samia Suluhu Hasssan,kiongozi wa watu ,mpenda maendeleo,mwenye moyo wa huruma ,unyenyekevu na upendo usiopimika katika mizani ya aina yoyote ile. Kiongozi anayefahamu kuwa licha ya mamlaka yake na madaraka yake makubwa kikatiba na kisheria lakini bado anaishi katika hali ya ubinadamu,bado amebakiwa na ubinadamu wake na katu na kamwe hajawahi kujifananisha na Mungu wala kujivika Umungu Mtu, katu na kamwe mama huyu na Rais huyu wa kipekee kabisa kuwahi kutokea katika Bara la Afrika hajawahi kuhitaji kuabudiwa wala kupewa utukufu apewao Mwenyezi Mungu.

Rais Samia Ni kiongozi mwenye misimamo ya hali ya juu sana kiuongozi,ni kiongozi mwenye utulivu wa kiwango cha juu sana,Ni kiongozi asiye yumba wala kuyumbishwa katika kutimiza maono yake na ndoto zake katika Taifa letu,Ni kiongozi mwenye kifua na moyo ambao ingekuwa mataifa yaliyo endelea kwa hakika lingekuwa ni somo Tosha katika madarasa ya wanafunzi wanaosomea uongozi,siasa utawala wa umma na mahusiano ya kimataifa. Rais samia ni Maktaba itembeayo ,Ni dhahabu katika uso wa Dunia ,Ni lulu Kwa Taifa,Ni almasi kwa vijana Na rejea kwa vizazi vijavyo na Ni hadhina ya Taifa.

Ndugu zangu watanzania,Tumefika hapa kama Taifa mahali tunaposifiwa hadi na mashirika ya kimataifa kutokana na ukuaji na maendeleo ya uchumi kutokana na misimamo mizuri ya kisera ya uchumi aliyo nayo Jemedari wetu Dr Samia.Utulivu wake Ndio umekuwa chachu katika maendeleo ya Taifa letu katika kila sekta.

Rais samia huwa hatishwi wala kuyumbishwa na makelele yasiyo na hoja wala mashiko,Rais samia siku zote anatazama mbele kwa mipango na mikakati maridadi na kabambe katika kulivusha na kulipaisha Taifa kiuchumi,.ndio maana amekuwa mshindi katika mioyo ya watanzania na kwa kila sekta amefanikiwa kwa kiwango cha juu.

Watanzania wenzangu mtambue yakuwa kama kiongozi usipokuwa na misimamo na kanuni unazosimamia zinazozingatia maslahi mapana ya Taifa na kuzingatia misingi ya kisheria na katiba ya nchi lazima uyumbe,lazima uyumbishwe,lazima ucheleweshwe ,lazima upoteze we muda,lazima ujazwe hasira,lazima upotezwe Dira na muelekeo wako kwa kuwa unapokuwa unaongoza Taifa kuna kuwa na watu wamekaa pembeni wanasubiri ukosee ,udondoke,ujikwae ,uvuruge na hata wakati mwingine wanaweza wakafanya hata hila ya kuchomelea mambo ili tu kutaka kukupoteza ,wapo wengine wanakuwa hata pembeni wakitamani hata kesho washike na kukalia kiti chako,wapo wengine wanakuwa wanahisi wao ndio walistahili kukalia kiti chako na siyo wewe.

Ndio maana viongozi wenye upeo mkubwa na maarifa makubwa na akili kubwa kama aliyo nayo Rais samia na misimamo yake ya kiuongozi na utulivu mkubwa wa kiuongozi pamoja na kupewa kibali na kuinuliwa na mwenyezi Mungu katu na kamwe huwezi kuwayumbisha ,huwezi kuwadanganya huwezi kuwapotosha wala kuwachezea ,wala kuwalaghai wala kufanya hila na usitambulikane maana ni kawaida viongozi aina ya Rais samia kuwa na Taarifa zote kiganjani pao hata kabla ya kufika eneo fulani au kusikiliza maelezo ya mtu fulani.

Viongozi aina ya Rais samia ni nadra sana kuwapata Duniani,ndio maana unaona watanzania wakiendelea kumuunga mkono Rais samia,maana wanajuwa ni lulu ,Ni zawadi ambayo huwa haipatikani kila siku na ndio maana watanzania wana itunza kwa wivu mkubwa sana na kwa heshima ya kipekee kabisa. Rais samia ni kama chemchemi katikati ya jangwa,Ni nuru katikati ya Giza ,Ni Njia katikati ya pori,Ni tumaini la vijana na nuru ya wanyonge.

Asante sana Rais samia,kwa hakika maisha yako na utumishi wako ni zawadi tosha kwa watanzania,Ni Tabasamu tosha kwa wenye uchungu na ni faraja tosha kwa wenye kukata Tamaa. Umeunda na kuongoza serikali ambayo imewatua mizigo mamilioni ya watanzania.imewatua mizigo wanafunzi ambao sasa wanasoma bure,imewatua na kuwainua migongo wakulima, imewatua mizigo wafanyabishara ambao sasa wanafungua biashara kila kona ya nchi. Asante Rais samia mama wa Taifa ,mlezi wa watanzania na mboni Ya Taifa.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Utaandika hivyo hivyo hadi 2025 ila uteuzi hupati

Sent from my Infinix X6516 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom