Nani aliyemuumba Mungu?

Nani aliyemuumba Mungu?

Unajua why you,

Yani ulivyoandika ni wewe mtupu,maelezo uliyotoa nimeyaconvert to sauti yako....heheheheehhh

Sijui watakuwa wanatumia jina gani ambalo ni tofauti na jina Mungu?🤔
Mungu ni jina tu Joanah. Inategema na mahali fulani tu wameamua kumpa jina gani.

Mfano huku sisi waswahili tunamwita Mungu lakini ana majina mengine kulingana na sehemu. Mfano Allah, God, Dios, YHWH n.k
 
Wafuasi wa Big Bang wote ni wagonjwa wa akili, ile ni dhana tu ambayo inataka ithibati.
Theory zote kuhusu Mwanzo wa Dunia zinamapungufu....sielewi za Dino wala bingbang...hakuna aliyenyoosha maelezo naweza shake credibility ya yeyote hapo.
Nimeamua kuachana na hayo mambo ikija theory mpya ntafuatilia nijue kama imepata ukweli...ili tulizonazo bado sana.
Tuleni maisha tu guys siyo kila kitu lazima tupate majibu kizazi hiki watapata hata kizazi kingine...This is work kwenye progress tusing'ang'anie mavitu hayana majibu...ili tuonekana tumepata majibu....sometimes we need to say I don't know.
 
Wewe mbona huweki ushahidi wa madai unayo dai, zaidi ya kukimbia. Sisi ushahidi tunao,ila itifaki lazima zizingatiwe,maana kama kusema tu kila mtu anaweza kusema,lakini ushahidi ndio unawafunga midomo wasemaji hovyo kama wewe.
Unabwabwaja sana....nikisema kitu hakipo ushahidi wangu ni kutokuwepo kwake...yaani tunasema the absence of evidence is the evidence of absence.
Mtu akija nyumbani kwako akasema hakuna maji basi ujue yeye amayetafuta akakosa hivyo akasema hakuna maji. Ukibisha usimuulizie ushahidi wa kutokuwepo maji(utakuwa ujinga) kama unampinga muoneshe maji case closed

Sasa kama wewe unasema kipo weka ushahidi ila ukija na taarabu zako mimi huo muda sina...usipokuja na ushahidi ila ukaja na taarabu tena sitareply
 
Mtu anahoji iweje aitwe mjinga kwa kuhoji?? Kama asipohoji na anaamini kwamba Mungu kaumbwa aitwe nani??!!

Kuuliza kwake kunamfanya awe mjinga?? muongo, maamuma nk??

Nakwambia mlete hapa huyo ulipokopi hiyo post, hiyo ndiyo shida ya Copy-paste hovyo.
Wewe kidogo una akili..eti kuuliza ni ujinga?
 
The question: "If God is the creator, then who created the creator?" is illegitimate because by definition, the Creator is uncreated. He is eternal, without beginning, without end and all affairs return back to Him: (وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلْمُنتَهَىٰ) "And that to your Lord is the return (of all beings and affairs) (and of all perfections in attributes)." (53:42).

Thus to ask who or what created something that is uncreated is the way of:
a) an ignorant person devoid of intellect,
b) a lying deceiver, a sophist.

Note : Maelezo haya mafupi nime "copy" na ku "paste" toka kwenye tovuti iitwayo "www.aboutatheism.net", mnaweza tembelea huko mpate faida.

Tujadili hili, kwa wale wote ambao huuliza swali hilo, waje watuambie kwanini wanauliza swali hilo.

Ahsante.

Jurjani (Zurri)
Kill your self so that u either go to heaven or Hell to prove your argument.
 
Unabwabwaja sana....nikisema kitu hakipo ushahidi wangu ni kutokuwepo kwake...yaani tunasema the absence of evidence is the evidence of absence.
Nacheka sana huu ni uoga. Ukisema kitu fulani hakipo, unatakiwa uthibitishe kutokuwepo kwake, sio unasema tu. Ukitaka hali iwe unavyotaka,tunakuwa tunatumia akili vibaya. Sasa hapa utaona mimi na wewe nani anabwabwaja tu na kukimbia kujibu hoja.

Hii kauli uliyo itoa nayo inahitaji maelezo na ithibati. Tuambie umejuaje kama hakuna ushahidi.
Mtu akija nyumbani kwako akasema hakuna maji basi ujue yeye amayetafuta akakosa hivyo akasema hakuna maji. Ukibisha usimuulizie ushahidi wa kutokuwepo maji(utakuwa ujinga) kama unampinga muoneshe maji case closed
Ukweli hauko hivyo mpaka athibitishe hili,wapo watu ambao hawatafuti ila kwa uvivu wao na kuokoa muda husema uongo, kwahiyo ithibati lazima iwepo.

Pili, kutokuyaona yeye maji hakumaanishi kwamba kweli maji hamna, ukizingatia yeye ni wakuja tu hapo kwangu. Ndio maana werevu huwa wanauliza kwanza, na naona unatatizo la kutoa mifani timilifu.
Sasa kama wewe unasema kipo weka ushahidi ila ukija na taarabu zako mimi huo muda sina...usipokuja na ushahidi ila ukaja na taarabu tena sitareply
Mpaka najiuliza kwanini hujibu swali nililo kuuliza na kwanini umekuwa muoga kiasi hiki. Umejuaje kama ushahidi haupo ? Thibitisha hilo, usilete "risala kwa ajili ya mgeni rasmi", kuomba huruma ishike hatamu.

Huwa kazi yangu naimaliza hivi, hatuwezi kuendelea hoja bila kujibu swali nililo kuuliza, huu utoto nishaukomesha.

Sisi hatuachi hata nukta, tunahoji, ndio tunaendelea. Utanikuta nipo hapa hapa.
 
Nacheka sana huu ni uoga. Ukisema kitu fulani hakipo, unatakiwa uthibitishe kutokuwepo kwake, sio unasema tu. Ukitaka hali iwe unavyotaka,tunakuwa tunatumia akili vibaya. Sasa hapa utaona mimi na wewe nani anabwabwaja tu na kukimbia kujibu hoja.

Hii kauli uliyo itoa nayo inahitaji maelezo na ithibati. Tuambie umejuaje kama hakuna ushahidi.

Ukweli hauko hivyo mpaka athibitishe hili,wapo watu ambao hawatafuti ila kwa uvivu wao na kuokoa muda husema uongo, kwahiyo ithibati lazima iwepo.

Pili, kutokuyaona yeye maji hakumaanishi kwamba kweli maji hamna, ukizingatia yeye ni wakuja tu hapo kwangu. Ndio maana werevu huwa wanauliza kwanza, na naona unatatizo la kutoa mifani timilifu.

Mpaka najiuliza kwanini hujibu swali nililo kuuliza na kwanini umekuwa muoga kiasi hiki. Umejuaje kama ushahidi haupo ? Thibitisha hilo, usilete "risala kwa ajili ya mgeni rasmi", kuomba huruma ishike hatamu.

Huwa kazi yangu naimaliza hivi, hatuwezi kuendelea hoja bila kujibu swali nililo kuuliza, huu utoto nishaukomesha.

Sisi hatuachi hata nukta, tunahoji, ndio tunaendelea. Utanikuta nipo hapa hapa.
Nshakuzoea wewe toka unajiita mzuri kwahyo sipati shida.
Nimejua hakuwepo kwasababu hakuna ushahidi sasa kama unaniomba tena ushahidi hii mbinu imefeli na kama huna okoa muda wangu na wako hata usiniquote
 
“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.”
— Yohana 1:1 (Biblia Takatifu)
 
Wewe kidogo una akili..eti kuuliza ni ujinga?
Uwe unatuliza akili na kuelewa nini kinacho ongelewa au nani amesema nini ? Sasa nikikuuliza wapi kusemwa kuuliza ni UJINGA ? sijui utanijibu nini ?

Hapa tunajadili uhusiano wa kinachoulizwa na hali yauulizaji.Hivi leo hii ukiulizwa na mtu maswali haya unapata ishara gani kuhusu mtu huyo ?

1. Hivi kiwango cha joto leo ni kilo ngapi ?
2. Hivi kati ya baba na mwana nani mkubwa ?

Sasa mpunguze mihemko na muache utoto kwenye mada za kielimu.

Ahasnte.
 
Nshakuzoea wewe toka unajiita mzuri kwahyo sipati shida.
Nimejua hakuwepo kwasababu hakuna ushahidi sasa kama unaniomba tena ushahidi hii mbinu imefeli na kama huna okoa muda wangu na wako hata usiniquote
Hujajibu hoja kijana, leta ushahidi.

Umejuaje kama hakuna ushahidi ? Hili ndio swali la msingi.
 
Naona hamjaelewa mada.
Ndiyo maana nakwambia masuala ya Mungu yupo ama hayupo ni IMANI na imani haionelani kwa macho...sasa ukitaka kuhakikisha kwamba kweli yupo ama lah ni suala la kujiua ili ukahakikishe mwenyewe kwa macho yako...hakuna njia nyingine !!
 
Back
Top Bottom