King Elly
JF-Expert Member
- Sep 19, 2013
- 1,206
- 1,308
No.3 nimekuelewaUshauri no 1:
Kuna jamaa alikuwa na ng'ombe wake alikuwa anampeleka mnadani, akiwa njiani alitokea mteja akataka kumnunua kwa laki tatu jamaa akagoma, akatokea wa pili akataka kumnunua kwa laki mbili na 80 jamaa akagoma, lengo lake ni kumuuza kwa laki tano. Alipofika mnadani akajikuta hata kumpata mteja wa laki mbili ikashindikana na akamuuza ng'ombe kwa laki moja na 70.
Ushauri no 2
Oa mwanamke anayekupenda na si unayempenda, kwa kuwa ukioa mwanamke unayempenda ni ngumu kutambua reflection ya upendo wake kwako, kwani +ve na +ve unajua kinachotokea.
Like charges repel each other - kiswahili chake sijui.
Ushauri no 3.
Oa mwanamke mwenye akili na ni vema mwanamke akaolewa na mwanaume mwenye akili kwa kuwa upendo ukizidi hupunguza kiwango cha kufikiri.
NB: love is not static. Pia hiyo ni hali ya kawaida sana kwa wanaune waliooa nafikiri wameshakutana na kipindi kigumu kama hicho, just inatokea tu unaona kama hakuwa chaguo lako na ikitokea ukakosa msimamo unajikuta unafanya maamuzi ya ajabu ambayo matokeo yake unakuja kuyaona baadaye.