Namuomba Rais Samia amsaidie huyu dada aliyekuwa muigizaji

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,069
40,732
Sina hakika kama imeshaletwa huku au laa, ila mimi ndio nimeiona leo. Nikaona niilete hapa ili mwenye kuweza kusaidia matubabu ya mwigizaji Carina asaidie. Pengine hata tukimega pesa kidogo toka kwenye yale magoli ya Mama si mbaya sana, asaidiwe apelekwe hata India tu. Maelezo kamili yapo chini kwenye video

====
Caroline Hussein, maarufu kama Carina, ni muigizaji mashuhuri wa filamu nchini Tanzania. Hata hivyo, maisha yake yamejaa mateso makubwa kutokana na tatizo la tumbo lake kuwa wazi na kuvuja uchafu wa haja kubwa kama bomba. Hali hii imesababishwa na upasuaji ambao ulifanyika na kufanya tumbo lake liwe wazi wakati wote.

Globaltvonline imefanya mahojiano naye mara nyingine tena na kueleza changamoto na magumu anayopitia. Moja ya changamoto hizo ni kufanyiwa mavazi (dressing) mara kumi kwa siku. Hii ni hali isiyokuwa ya kawaida na inaleta gharama kubwa kwa familia yake. Wanahitajika kutumia pesa nyingi kila siku ili kupata vifaa vya kufanyia mavazi hayo. Gharama hizi zimechukua kila kitu walichokuwa nacho na wamekumbwa na hali ya uhitaji mkubwa.

Caroline anahitaji msaada wetu. Kwa sasa, wanahitaji kufanya operesheni ya 18 ili kurekebisha tatizo hili. Kupitia namba zilizotolewa hapo chini, tunaweza kuchangia kiasi chochote cha fedha ili kusaidia kugharamia operesheni hiyo na kumpatia Caroline matumaini na afueni.

Namba za kuchangia:
  • Tigo Pesa: 0712595858
  • M-Pesa: 0769990045
  • Airtel Money: 0789095858

Kila mchango una thamani kubwa na unaweza kuleta mabadiliko katika maisha ya Caroline. Tuchukue hatua na tuonyeshe mshikamano wetu kwa kumchangia na kumsaidia kupitia kipindi hiki kigumu.
 
Sina hakika kama imeshaletwa huku au laa, ila mimi ndio nimeiona leo. Nikaona niilete hapa ili mwenye kuweza kusaidia matubabu ya mwigizaji Carina asaidie. Pengine hata tukimega pesa kidogo toka kwenye yale magoli ya Mama si mbaya sana, asaidiwe apelekwe hata India tu. Maelezo kamili yapo chini kwenye video

Mateso makali sana loh.

Mungu afanye wepesi
 
Jamani tumsaidie mwenzetu mimi tayari
Umetuma TSh 5,000 kwenda kwa 255712595858 - CAROLINHAWA EBRAHIMBOUNIN. Jumla ya Makato TSh 184. (Ada TSh 130, Tozo TSh 54), VAT TSh 20. Kumbukumbu no.: XXXXXX. 11/05/23 19:32. Salio lako jipya ni TSh 133. Furahia punguzo la Tozo unapofanya miamala kwa Tigo Pesa.
 
Sawa, na mimi natuma nitaweka muamala hapa
 
Back
Top Bottom