Kunahitajika mabadiliko ya fikra kwa Mawaziri na wasaidizi wote kumsaidia Rais Samia kuwatumikia Watanzania

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,161
1,493
Ili Taifa liweze kusonga mbele tunahitaji mabadiliko ya fikra kwa Watu walioaminiwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumsaidia kuwaletea Maendeleo Watanzania. Ni Muhimu sana Mawaziri, Wakurugenzi na Wasaidizi Wengine Waiwaze Tanzania ya mwaka 2040.

Ni sahihi kuendele kutumia Bahari yetu ya Hindi kwa kusafirisha mizigo, watu na Utalii? au ni muda sahihi wa kuanza kufikiria kuhakikisha Bahari yetu inatumika kwa kilimo kule Sumbawanga, Ruvuma, Mbeya n.k.

Pengine urithi tunaoweza kuwaachia Kizazi kijacho ni kuhakikisha kuwa Bahari yetu itatumika zaidi ya inavyotumika sasa. Tukiwa tunasema Kilimo ni Utii wa Mgongo, Je ni sahihi kuendelea kutegemea mvua hizi ambazo zimekuwa hazina uhakika? Mabadiliko ya Fikra yaanze sasa kwa ajili ya kizazi kijacho. Kilimo kinaaminika baada ya miaka si mingi ijayo ndio kitatoa mabilionea wengi.

Ni hatua kubwa tumepiga katika Sekta ya Umeme- Bwawa la Nyerere ambalo mwaka huu litaanza kufanya kazi, bila shaka ni kazi kubwa imefanyika.

Pongezi kwa Wizara, Watendaji na Mh Rais kwa kuhakikisha mradi umekamilika. Ni muhimu Watendaji wetu wakafikiria namna ya kupata chanzo kingine cha uhakika kisichokuwa cha maji. Wote tunajua namna mabadiliko ya hali ya hewa duniani yanavyoongezeka kwa kasi, sina hakika kama Mabwawa yetu ambayo ni chanzo cha Umeme baada ya miaka 25 ijayo kama yatapata maji ya kutosha. Ukame na kupungua kwa mvua katika mikoa ya Iringa , Morogoro, Mbeya , Singida etc ni tishio kubwa .

Ni muda wa kuanza kuwekeza kwenye nishati ya Jua, Upepo wa pale Singida, Iringa na gesi.

Kama Taifa ni Muda sahihi wa kuwekeza kwenye Sayansi, Dunia inaenda kasi saana. Vitu vingi vinahitaji Mapinduzi ya Fikra. Pengine Kizaji kijacho kitahoji kama kuna ulazima wa Wizara ya Kilimo na Watendaji wake Wakuu kuwa Dodoma na Sio Njombe/Songea etc au Wizara ya Utalii kuwa Dodoma na sio Arusha etc ..

Watanzania, tumuombee Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluh Hassan kwa kazi kubwa anayofanya. Leo Tanzania ni moja ya Nchi zenye Health Facilities nzuri na bora Afrika Mashariki, Mfumo wa Elimu umeendelea kuimarishwa zaidi kuanzia Mifumo, Majengo na Vifaa etc.

Mh Rais ndiye Chief Comforter wa Taifa, lakini haiwezekani kila kitu kikafanywa na Mh. Rais, yaani Mtu amezulumiwa Ardhi kijijini kwetu jambo hili tunataka Rais alisemee wakati kuna VEO, WEO, etc.

Watanzania tumuombee Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwenyezi Mungu Mbariki na umpe Afya njema Mh. Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwenyezi Mungu Ibariki Tanzania.
 
In short hatuna watendaji serikalini tuna takataka tu rais anahitaji ushauri wa kijasiri na aukubali
 
Back
Top Bottom