Namuheshimu mama yangu lakini simpendi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namuheshimu mama yangu lakini simpendi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by rosemarie, Jul 30, 2011.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  wakuu nina tatizo nimekaa nalo muda mrefu sana moyoni mwangu'
  tumezaliwa wanne kwenye familia yetu'
  sisi ni wachaga na tumekulia na kulelewa na kusoma uchagani'
  lakini kwa kadri tulivyokuwa tunaendelea na maisha niligundua mama yangu mzazi anamthamini mtoto mwenye mali peke yake'
  baada ya kugundua hilo niliamua kunyamaza kimya japo nilikuwa na uchungu moyoni'
  lakini hicho kitendo kilijidhiirisha hata kwa watu wanaotufahamu kijijini kwetu na ilileta matatizo makubwa'
  kwa kweli kutoka moyoni mwangu nimejikuta simpendi kabisa mama yangu lakini bado namweshimu kama mzazi wangu'
  nikienda nyumbani mara moja kwa mwaka sijisikii kabisa hata kukaa naye hata kwa dakika 10 inakuwa ngumu sana,
  niliumia sana kwa kuwa mimi ndiye maskini kabisa na ndiye ambaye sipewi heshima kabisa
  naombeni kujua kama kuna mtu mwenye matatizo kama haya na naombeni kujua kama kunaweza kutokea matatizo yoyote katika maisha yangu kwa hilo

  nawakilisha.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Wewe jinsia ipi?
  Wa ngapi kuzaliwa?

  So far this is very serious........
   
 3. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Huyo mama ni wa hajabu. SIsi mama yetu anampendelea zaidi asiye na uwezo na sisi hatusikii vibaya kwani tunaona ni huruma ya mama kwa mtoto. Yani tulikuwa na kaka yetu mama alikuwa anampendelea sana kwa kuwa alikuwa hana mbele wala nyuma; aliamua kwenda shule kwa sasa ana kazi yake na yuko mbali; ila those days alipokuwa arosto ndio alikuwa kipenzi na ukimsema vibaya kwa mama tegemea kununiwa.
   
 4. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  hiyo tabia ya mama yako imekuwa kawaida tu siku hizi kwa wazazi wengi. nakushauri msamehe huyo mama kwani naye ni binadamu kama wengine. endelea kumheshimu hivyohivyo na ikibidi uongeze heshima lakini pia uwe na bidii kutafuta kujitegemea kwanza na kisha kama ni mapenzi ya Mungu uwe na mali ya ziada na hata uwezo wa kuwasaidia wengine akiwemo mama yako huyo.

  kumbuka kuwa kama hujajitegemea, hilo ndo kikwazo cha kwanza cha wewe kuheshimiwa na watu. jitahidi ujitegemee kwanza. kama tayari unajitegemea, ni vyema lakini usiwe unaomba kusaidiwa na ndugu zako au kupeleka mashitaka nyumbani kwenu kuwa ndugu zako hawakusaidii. jitahidi kupigana peke yako na ikiwezekana shirikiana kwa karibu na marafiki wema ili kuangalia namna ya kunyanyuka kimaisha kwani siku utakaponyanyuka, utaheshimiwa na wote.

  mwisho usipuuze haja ya kujiendeleza kwa kutafuta elimu kubwa zaidi. wengi walishindwa kupata maisha mazuri kwa kuyatafuta mitaani, wakayapata kirahisi kupitia darasani. kuna mtu namfahamu ana zaidi ya miaka kumi (10) hajafika kwao kwa sababu kama hizi zako, heri wewe unakwenda kila mwaka! ila yeye alijikita katika elimu na hata sasa yuko nje akipasua kitabu na hiyo imemletea tena heshima katika familia kwani kila mtu anakubali kuwa his future is brighter!

  Mungu hawezi kukunyima vyote, Yeye ni mwaminifu kwao wamchao na hakika siku moja atasikia sala yako atakuinua kwa wakati wake

  Jina la Bwana lihimidiwe
   
 5. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu mimi ni mwanaume na ni wa kwanza kuzaliwa,wadogo zangu wana uwezo lakini mimi sina uwezo sana ila mungu amenisaidia kuridhika na hali niliyo nayo
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Na isimlaumu sana mama yako.....
  Huwezi jua maisha yame mfunza kitu gani...
  Inawezekana life haikuwa kind kwake.....
  Life was so cruel......so na yeye anatoa kile ambacho life imempa....
  Hakuheshimika labda na society kwa umasikini...
  So na yeye kwa kuuchukia umasikini,anawachukia mpaka watoto masikini..
   
 7. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  judith umenipa ushauri mzuri sana
  lakini mimi ni mtu mzima tayari na natamani nigeweza kumsamehe na kusahau lakini kila nikifika nyumbani nakumbuka na kulia machozi,namkumbuka baba yangu ambaye ni marehemu alivyokuwa mtu mwema na mpole
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  kwa kuwa wewe ni first born na wamama wanataka first born ndio aongoze
  mapambano ya familia.....
  Na kwa kuwa wewe unasema umeridhika na hali uliyonayo...

  Its natural kwa mama yako kuwa dissapointed na wewe...
  Yeye anaona umemuangusha kwa kukubali hali hiyo
  na wewe unaona hakutendei haki....
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mkuu inawezekana wewe na mama yako mna
  tofauti kubwa ya personality....wanaita personality clash....
  Sasa wewe mwanaume unalia machozi kwa kukumbuka ya zamani????
  Mimi naona hapo unakuwa weak na pengine mama
  yupo more strong na anataka wewe uwe strong na ku fight...
  Mama yako ana drive na ambitions ambazo wewe huna naona..
  So mnazidi kutengana...
   
 10. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu nafikiri mimi ni mtu mwenye moyo laini sana
  mtu akishaniudhi inakuwa tabu sana kusahau,lakini nafikiri uwezo nilio nao ni mungu peke yake anaweza kuniongezea
  namtegemea muumba wangu najua siku moja nitakuwa na mali kama wanavyotaka lakini kamwe sitaweza kulazimisha hilo
   
 11. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  pole kaka kaka,

  nakuombea amani ya Bwana ipitayo akili zote,
  tulihimidi Jina la Bwana kila wakati!
   
 12. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  siamini kama wewe ni masikini kiasi hicho,kwani masikini hana ata access ya jamiiforum!shukuru mungu kisha pambana ktk maisha!unataka mama akuthamini huku huna uwezo wa kumtimizia shida zake?akija dar anafikia kwa mtoto aliyempokea na gari ubungo,ataenda kwa mtoto ambaye chakula anachotaka anapikiwa,alale chumba chenye kiyoyozi,akatibiwe trauma centre au agha khan si wewe una mpeleka mwananyamala hosp etc
   
 13. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Ushauri na mtazamo wa The Boss una mantiki, jaribu kujichunguza huenda mama yako naye hakupendi kutokana na jinsi mnavyoyachukulia maisha kwa mitazamo inayokinzana, kwa ufupi mnaishi kwenye dunia mbili tofauti...
   
 14. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu kama huo ndio uwezo nitafanyeje?
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Halafu kuna vitu vingine vinaanzia mbali sana

  je baba yako alikuwa tajiri?
  Kama alikuwa masikini,mama yako alimchukuliaje??

  Kama alikuwa anakasirishwa na baba yako kushindwa
  kutumia nafasi alizopata kuondokana na umasikini

  si ajabu na wewe umerithi tabia za baba yako
  so chuki ya mama yako kwa baba yako imehamia kwako.......
   
 16. Nemo

  Nemo JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 80
  episodes
  Pole sana,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,ila to me it sounds like you are projecting your own feelings of inadequacy as lack of love on your mothers part. Nothing like sucessful sibilings to make ones low self esteem even more......................Kwani ni heshima gani hiyo ambayo wengine wanapewa that you find missing on your side? Na kuhusu wanakijiji, seing the same how sure are you that sio wazushi , out to cause trouble to your family? It's possible that wanakijiji hao hao may have observed the inferior feelings you have towards your siblings and are just using them to fuel the matter!!!!
   
 17. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Inawezekana kabisa jamaa ana infiriority sababu hana pesa kama wadogo zake, ikimtoka hiyo atafurahia maisha kama kawaida tu
  &lt;br /&gt;<br />
  &lt;br /&gt;
   
 18. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280

  mkuu baba yangu hakuwa tajiri,tuliishi maisha ya kawaida kabisa,lakini waliweza kutulea
  kwa kweli jambo la kusema tulazimishe kupata mali mimi nipo kinyume kabisa
  naishi maisha ya kawaida nina nyumba,kazi na kausafiri,na nina watoto wangu wazuri sana
  jamani nifanye nini mimi ili niheshimike?
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Gaga sijaona ulichoandika hapo
  na wewe nemo huoni ungeandika kwa kiswahili ungefanya la maana?????????
   
 20. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Maskini, pole sana. omba mungu nawewe utafanikiwa. wazazi wengi wana huo mchezo, hata sijui kwanini
   
Loading...