Namshukuru Mungu silalii tena mabox

Namshukuru Mungu silalii tena mabox

Unatuonaje jamani? Wee si umetoka kutudanganya kuwa ulikuwa unalala Msasani beach unajifunika na mchanga?
 
Dah sitosahau siku ya kwanza nilipoamua kupanga hakuna siku nilitetemeka kama siku hiyo haipo siku nimewai kua katika mtetemeko wa woga kama siku hiyo nilisahau hata njia ya nyumba niliyopanga kutokana na wenge .

Sitosahau nilivyoenda kuuza ukwaju wa bakhresa na kufanya vibarua sabasaba ili nikamikishe kodi na pesa ya dalali ili nihamie kwangu.

Sisahau nilivyolalia box la tv nililopewa pale msimbazi centre asee ulikua msimu wa baridi mwezi wa saba nyumba ilitoka kusakafikwa na walikuwa wameweka maji ili cement ishike vizuri nilioadeki jioni natandika kulala box lililowana asee sisahau kamwe.

Sisahu nilimkaribisha mwanagu akaona gheto zuri ila mi ndo maskini akanizunguka kwa mwenye nyumba apamiliki yeye namshukuru Mungu kabla ya mda wa kodi kuisha nilipata kazi mkoani morogoro japo nako kazi ilinipitisha mapito mazito hatujakaaa sawa corona ikaingia kazi ikasimama sina hata 100 mbovu aseee niliona maisha hayafai asee nikajitoa akili akiba niliyokua nayo nihonge mshikaji anifanyie mpango nipate kazi yapi merkezi asee yule jamaa alinitapeli kistaarabu aseee mambo ni mengi sana.

Mpaka hapa nilipo namshukuru Mungu ngozi yangu haina makovu ila nimepigika sana ila niliibuka mshindi.

Ukimpata mwenza sahihi ni rahisi sana kufanikiwa hata kama hana kitu ilo nina ushuhuda nalo.
Wanaume tuishi vizuri na wenza wetu kama wanakua wema kwetu wamebeba baraka zetu nyingi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom