Namshukuru Mungu silalii tena mabox

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,706
Ashukuriwe Mungu aliye juu na muweza wa yote,

Siku ya kwanza natoka kijijini nafikia kwenye chumba nilichokitafuta nikiwa kijijini,

Nilifika nikiwa na kabegi changu cha mgongoni na computer redio, na vifaa vingine kwa ajili ya ufundi, wa simu na radio,

Nilitafuta mabox nikatandika chini na kulala huku nikiomba ndoo ndogo kwa ajili ya kuchotea maji na kuoga,
huku nikiendelea kutafuta sehemu ya kufungua ofisi, na nikimsubiri make wangu ambaye angekuja baada ya wiki mbili na begi langu dogo nililolisahau lenye mouse,extarno,na hadidisk za computer

Basi bhana wife alivokuja, bahati nzuri aliuza kuku wake huko kijijini, na kununua Yale magodoro yanauzwa 30000, ya kutengenezea masofa, hivo Yale mabox nikayapeleka ofisina na kuanza kulalia huko maana of is I iliko usalama ni 0

Tukaanza maisha lakini mpaka sasa namshukuru mungu nalipa kodi sehemu zote ambazo jumla ni kama 90 ukijumlisha na umeme,

Jambo kubwa namshukuru Mungu, nimeweza kununua godoro japo limetumika ila lipo tu katika halina nzuri,

Veto limechangamka, mziki tv kochi la mtu mmoja, napikia gesi mm pia naweza badili hata suruali sasa, tulikuwa tuna tumia simu moja na make wangu, ila sasa kila mtu ana smart yake,

Namshukuru Mungu kwani hayo yote ni ndani ya miezi 6 tu,

Wakati watu wengene wakifurahia kupiga hata 10, Mimi pia nafurahia kwa kupiga nusu hata hii,
 

Unatuonaje jamani? Wee si umetoka kutudanganya kuwa ulikuwa unalala Msasani beach unajifunika na mchanga?
jaribu kuanzia hapa labda utaelewa ila kama una kichwa chepesi

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom