Namshauri Ben Saanane, Siasa sio Uaduai.
Zamani kidogo, niliwahi kuwa na rafiki, rafiki ambaye nilimuamini, nikafanya nae kazi kwa ukaribu na kumshirikisha katika mambo yangu mengi. Wakati mwingine Urafiki unazidi Undugu, ndivyo ilivyokuwa kwangu na rafiki yangu huyu, alikuwa kama ndugu au zaidi ya ndugu Kwangu.
Nilipokutana nae, nilitambulishwa kwake kuwa huyu ni "mwenzetu" nami nikamchukulia kuwa ni "mwenzangu" kwani sikuwahi kuishi kwa mitego mitego na ulaghai katika maisha yangu ya siasa, niliishi kwa misimamo na kuabudu nilichokiamini, nilikuwa hivyo na nipo hivyo.
Namzunguzia Ben Saanane, kama mwanaharakati, rafiki na ndugu yangu. Namjua kwa kiasi kikubwa, naijua hulka na tabia zake, nasikitika kukiri mbele ya jukwaa hili kuwa ndugu yangu huyu SI MTU WA KUAMINIKA, mwenye Kinyongo, anayependa UADUI na PURUKUSHANI.
Nimesikia anataka UBUNGE kwao ROMBO - TARAKEA, na ameenda katika sura yake ile ile ya UADUI, sura ya Purukushani na Kinyongo, lakini baya zaidi nililosikia na kunisikitisha ameanza kuchonganisha wenzake, kama ilivyo kawaida yake.
Naomba nikushauri kupitia jukwaa hili, maana simu yangu siku hizi haupokei (UADUI), SIASA haifanywi namna unavyotaka kufanya wakati mwingine siasa ni Upepo, fuata unavyovuma, Usishindane nao...hauwezi kushindana na Upepo ukaushinda...na SIASA sio UADUI.