Namshauri Ben Saanane, Siasa sio Uadui

Namshauri Ben Saanane, Siasa sio Uadui

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,609
Namshauri Ben Saanane, Siasa sio Uaduai.

Zamani kidogo, niliwahi kuwa na rafiki, rafiki ambaye nilimuamini, nikafanya nae kazi kwa ukaribu na kumshirikisha katika mambo yangu mengi. Wakati mwingine Urafiki unazidi Undugu, ndivyo ilivyokuwa kwangu na rafiki yangu huyu, alikuwa kama ndugu au zaidi ya ndugu Kwangu.

Nilipokutana nae, nilitambulishwa kwake kuwa huyu ni "mwenzetu" nami nikamchukulia kuwa ni "mwenzangu" kwani sikuwahi kuishi kwa mitego mitego na ulaghai katika maisha yangu ya siasa, niliishi kwa misimamo na kuabudu nilichokiamini, nilikuwa hivyo na nipo hivyo.

Namzunguzia Ben Saanane, kama mwanaharakati, rafiki na ndugu yangu. Namjua kwa kiasi kikubwa, naijua hulka na tabia zake, nasikitika kukiri mbele ya jukwaa hili kuwa ndugu yangu huyu SI MTU WA KUAMINIKA, mwenye Kinyongo, anayependa UADUI na PURUKUSHANI.

Nimesikia anataka UBUNGE kwao ROMBO - TARAKEA, na ameenda katika sura yake ile ile ya UADUI, sura ya Purukushani na Kinyongo, lakini baya zaidi nililosikia na kunisikitisha ameanza kuchonganisha wenzake, kama ilivyo kawaida yake.

Naomba nikushauri kupitia jukwaa hili, maana simu yangu siku hizi haupokei (UADUI), SIASA haifanywi namna unavyotaka kufanya wakati mwingine siasa ni Upepo, fuata unavyovuma, Usishindane nao...hauwezi kushindana na Upepo ukaushinda...na SIASA sio UADUI.
 
hahahahaha....LENGO UNATAKA KUTUAMBIA KUWA UNAMJUA BEN...YAANI AMEKUJUA....NA MKAJUANA...kwa HIO UNAMPIGIA SIMU KWA MINAJILI YA "KUJUANA"

Sasa ushauri wangu kwenye siasa usiendekeze mapenzi
 
Juliana Shonza

Acha kujipendekeza.Kwani Ben baba yako umeacha kuwaandika ndugu zako wanaosota kwa umaskini kijijini kwenu unakuja kumuandika Ben.Waandike kwanza wajomba zako,bibi zako babu kaka zako mama zako wadogo na wale wengine wote walio tegemezi kwako mpaka unashindwa kutoka kimaisha ndo uje umuandike Ben
 
Last edited by a moderator:
Siasa ni uadui....kama vibaya utamalizwa.....wewe unacheza na siasa...ouko aliuwawa na moi kwasb ya siasa...wewe unakuja kutuletea ujinga hapa eti siasa ni utani,upendo....siasa ni uadui ndio maana hata lipumba alipigwa na mapolisi waliotumwa...
 
Ha ha haa...yaani nimecheka vibaya sana leo!! Hizi siasa hizii...!! Pole sana Juliana umeingilia mlango mbovu, nakushauri siku nyingine ukitaka kumshauri X wako ingia MMU kule utapata support kubwa!!

Ila Ben namna hii sio bhanaaa hata simu jamani!!?? Aombaye msamaha husamehewa japo si lazima ku-resume!! Ha ha ha....

I feel sorry for her Husband,sijui akisoma hii thread ya Wife atajisikiaje? Yani Bi dada kashindwa kabisa kuzuia hisia zake kwa Ben!
 
....

.....goli la wazi hilo hata kwa mkono unafunga hakuna refa
 
Bibie Julie,

Hivi hili nalo linakupa credit gani ktk kuupata Ubunge wa "vitu maalum" hapa Mlowo?

BACK TANGANYIKA
 
Wakulaumiwa ni Mbowe kwani yeye ndiye aliyemfundisha kuwa siasa ni uadui pale alipompa sumu awadhuru wapinzani wake wa uenyekiti ndani ya chama.
 
Back
Top Bottom