Namna Watanzania wanavyotapeliwa na Waganga wa Kienyeji nchini Kongo

SEHEMU YA TATU



Baada ya muda kupita bwana Seif alirejea akiwa ameambata na watu kadhaa huku wengine wakiwa na mafurushi ya mizigo.

Kamugisha alimfuata akaanza kuzungumza nae na ndipo alimwambia asubiri kwanza kwakuwa kuna watu alikuwa anawafanyia taratibu za kusafiri;Alipomalizana na watu wake hao takribani yapata saa 8 mchana,alitufuata tulipokuwa tumekaa kisha akawa anahitaji tumpatie maelekezo ni wapi tulikuwa tunaelekea .

Kamugisha " Tunaelekea Congo mkuu"

Seif "Congo sehemu gani?"

Kamugisha "Moba"

Seif "Ok usafiri wa Kuelekea Moba ni hadi kesho kutwa,kuna ile boti pale ndiyo mtakayoondoka nayo!"

Aliendelea "Congo mnaenda kufanyaje ndugu zangu"

Kamugisha "Kwenye mambo ya biashara tu kaka"

Seif "Kuweni wakweli,unajua watanzania sijui tukoje,mara kibao wanapita wanashindwa kusema ukweli ili kama ni msaada wapewe wao wanajifanya wajanja wakifika huko mambo yakiwagomea wanarudi na manung'uniko"

Kamugisha "Hahaha hahaha kaka bhana"

Seif "Nakwambia ukweli ndugu zangu,nyie kama mnaenda kwa waganga semeni niwaambie waganga wazuri msije mkatapeliwa!"

Jamaa alikuwa anaongea kwa ujasiri sana na pia mbele za watu,kitu ambacho mimi na mshikaji hatukukipenda hata kidogo,jamaa alimuomba kama inawezekana tutafute sehemu ambayo tutakuwa sisi watu watatu tuzungumze!.Seif alituchukua hadi maeneo ya nyumbani kwake ambako pembeni kulikuwa na Grosari ya kwake tukakaa hapo.

Sasa tukiwa pale kuna mtu alimpigia simu akamwambia amletee samaki wakubwa 3,haukupita muda bodaboda mmoja alikuja na samaki wakubwa akiwa amewaning'i niza mbele ya taa.

Seif "Ngojeni kwanza wawakaangie samaki hawa mle kisha ndiyo tuongee,mimi hapa kwangu huwa siwezi kuongea na watu bila kula kwanza"


Baada ya muda wale samaki waliletwa wakiwa wamekaangwa,tulianza kuwatafuna huku tukiendelea kupiga stori za hapa na pale.Tulipomaliza kula wale samaki jamaa ndipo akaanzisha stori na alihitaji kufahamu tunaelekea Congo kufanya kitu gani!.

Kamugisha "Yes kaka unajua mficha maradhi kifo umuumbua,sisi tunaelekea Congo kwa ajili ya matibabu"

Seif "Eeeh huo ndiyo uanaume,niambieni sasa mnaenda kwenye matibabu ya aina gani,Je mnaumwa ?"

Aliendelea "Msije mkaona nawauliza sana maswali,nyinyi ni watanzania wenzangu na kule mimi napafahamu vizuri sana na hata waganga wengi wazuri nawajua na ndiyo maana nataka nijue tatizo lenu kisha nitawaambia mtu sahihi atakaye wafaa!"

Seif "Hivyo msione aibu niambieni"

Kamugisha "Kaka sisi tulikuwa tunaelekea kwenye ishu za mali!"

Seif "Kwahiyo mlikuwa mnataka pesa,si ndiyo!"

Kamugisha "Ndiyo,brother!"

Seif "Sasa hayo ndiyo maneno,hapo nitajua sasa namna ya kuwasaidia!"

Aliendelea "Ngoja nimpigie bwana mmoja,aje muongee nae yaani kwa huyu niaminini tatizo lenu limepata tiba sahihi!"


Jamaa alinyanyua simu yake akapiga,ilipopokelewa wakaanza kuongea kwa lugha ya huko(Kiha au Kifipa).

Seif "Kuna jamaa nimemuita anakuja,huyu yeye ni mtaalamu wa maradhi ya kawaida na kuna kipindi mke wangu alikuwa akiumwa alinisaidia sana,huyu yeye ni mkongomani ila ameshazamia Tanzania muda mrefu na kaoa mwanamke wa Kiha,atawasaidia sana!"

Tulikaa tukiendelea kumsubiri huyo jamaa aliyeitwa aje tuzungumze ili tujue wapi pa kuanzia;Seif alikuwa ni muongeaji sana na kiukweli jamaa alibarikiwa kipaji cha kuongea.Haukupita muda huyo jamaa alifika akiwa anavuta tumbaku,baada ya kufika bwana Seif alianza kumueleza kila kitu tulichokuwa tumezungumza nae.Baada ya kuelezwa jambo letu,jamaa alituambia wabongo wengi huwa wanafeli kwasababu ya ujuaji wa kijinga.

Jamaa "Unajua watanzania wengi huwa hawajui chochote,na hata hao mnaowaona wanasimulia huwa ni uongo tu,ukweli wa huku tunaujua sisi"

Aliendelea "Mmeaga?"

Kamugisha "Mimi sijamuaga mtu,sijui kwa upande wako mwanangu!"

Mimi "Mimi pia sijamuaga mtu"

Jamaa "Kuaga simaanishi hivyo mnavyofikiria nyie,kuaga maana yake mmeongea na mizimu ya wazee wenu?"

Baada ya kutuambia hiyo kauli tulibaki tunaangaliana na Kamugisha kwasababu lilikuwa ni jambo jipya ambalo tulilisikia kwa jamaa.

Kamugisha "Sasa hao mizimu tungewaaga vipi?"

Jamaa "Hamuwezi kwenda huko bila kuaga mizimu,au mnadhani mnaweza kufanikisha mambo yenu bila kuaga mizimu?"

Aliendelea "Sasa sijui nyie mnasemaje,muage kwanza kabla ya kuondoka au muondoke bila kuaga!"

Kamugisha "Kwakuwa nia na lengo ni pesa,nadhani kuaga ni bora zaidi!"

Jamaa "Pale Moba Pol kuna jamaa yangu huyu ni mtaalamu sana kwa kazi yenu hiyo mnayoitaka,na yeye huwa hachukui pesa mpaka afanye kazi kwanza,sasa kama mko tayari tuvuke wote niwapeleke kwake kisha nikisha wafikisha mimi nitarudi nitawaacha ila mtanipa ka hela kadogo tu"

Kamugisha "Hayo sasa ndiyo mambo,tunaomba utusaidie!"

Kamugisha "Ujatuambia lakini jina lako kaka"

Jamaa "Mimi naitwa Jentre"

Kamugisha "Ok, sasa tunafanyaje?"

Jentre "Kuaga maana yake ni kuiaga mizimu ya ndugu zenu waliokufa,wawe mababu,mababa,wamama,au watoto;ili mradi wawe wamekufa hao ndiyo tunaita mizimu!"

Aliendelea "Kwakuwa hamkuaga huko mtokako,tutatafuta makaburi hapa jirani mkaage huko,kwanza nipeni hela nikachukue pemba nyeupe na udi kwa ajili ya kuagia!"


Kamugisha alichomoa noti ya shilingi elfu 5 akawa amempatia bwana Jentre ili akanunue mahitaji yaliyokuwa yanahitajika kwa ajili ya kuagia mizimu.

Jentre "Hili zoezi litafanyika usiku siyo muda huu lakini"

Seif "Ok kama ndivyo nadhani hawa mabwana waende wakatafute Guest House waweke mizigo yao kisha watarudi hapa ili ikifika jioni iwe rahisi"


Basi,bwana Seif alituchukua pale kwake akatupeleka kwenye Guest moja ambayo haikuwa mbali sana tukawa tumechukua vyumba kwa ajili ya kuweka mizigo,baada ya hapo tulirudi kwa bwana Seif kupumzika huku tukipiga stori za hapa na pale kupoteza muda.

Ilipofika jioni Seif alimuelekeza jamaa makaburi yaliyokuwa jirani na makazi ya watu,hata hivyo jamaa alimwambia pale itakuwa si pazuri kwasababu ni sehemu ambayo watu walikuwa wanapita masaa 24 na sisi tulipaswa kuvua nguo na kubaki uchi!.

Seif alimuelekeza makaburi ambayo yalikuwa mbali kidogo na mji ule mdogo na yalikuwa makaburi yaliyokuwa yanamilikiwa na kanisa la Roman Katholic,alimuita yule bodaboda aliyeleta wale samaki akamuambia aje na mwenzie ili watupeleke kwenye hayo makaburi ili kazi ya kuaga mizimu ichukue nafasi.


Inaendelea.................
 
Back
Top Bottom