mtatiro ni kati ya viongozi wachache vijana wenye upeo mkubwa mno,
Ana uwezo mkubwa sana wa kupambana mazingira aliyomo, mie na wenzangu 700 pale udsm tuliokuwa under private sponsorship tuliwekwa kwenye mikopo kwa sbb ya juhudi za mtatiro,
Nakumbuka kuna siku tulikuwa naye kwa waziri mkuu-alimbana pm had kikaeleweka,
Wakati huo alikuwa waziri wa mikopo,baadaye akawa waziri mkuu na kisha katibu mkuu wa vyuo vikuu tanzania kabla ya kujiunga cuf na kuwa mkurugenzi wa haki za binadamu na sheria na baada ya mwaka ,moja amekuwa naibu katibu mkuu wa cuf.
Mimi namtizama kwa jicho la msimamo sana,yeye ni role model kwa mtu ambaye si mnafiki,
Mtatiro amefika hapo alipo kwa sbb ya kutoyumbayumba,kama angehitaji fedha na umaarufu angekwenda cdm au ccm lakini kwa mrizamo wangu mtatiro ana roho ngumu,anapigania mafanikio atakayoleta na siyo ya kuletewa.
Na sidhani eti nafasi zote alizopitia amekuwa akibahatisha au kuzipata by chance,naamini anazipata kutokana na uwezo wake na nimeona kuna mchangiaji anasema alipokuwa high skul alikuwa kiongozi then amefika mliman pana wanafunz zaidi ya 20,000 wakamuamini na baadaye kuongoza vyup vikuu,
wakati akiongoza vyuo vikuu tukumbuke ndiyo enzi zilizokuwa na harakati za hali ya juu vyuoni,wakati tuliposhuhudia vyuo vikuu wakiandamana kushinikiza bei ya nauli na gharama za umeme zishushwe,ni wakati tuliposhuhudia maandamano kupinga uchakachuaji wa matokeo kenya na mauaji,hizi ni enzi ambazo mtatiro aliwaelekeza wanafunzi wa vyuo vikuu kupigania maslahi ya watanzania,
Na hata leo akiwa cuf tumeshuhudia moves zake nyingi-maandamano ya kupinga kuilipa dowans kwanza yalifanywa na mtatiro na chama chake kabla cdm hawajaanza,
Mapambano ya kupeleka rasimu ya katiba waliyoiandaa n.k.
So, mimi naona kama hapa jamvini watu wamekaa kishabiki mno lakini ukweli unabakia kuwa mtatiro ana uwezo mkubwa sana kupita vijana wengi walioko cdm na uwezo wake utasaidia sana kuiinua cuf.
Hongera mtatiro,hukohuko uliko tafuta ukombozi wa watz.