Namlilia Julius Mtatiro... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namlilia Julius Mtatiro...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Mar 24, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Nimekuwa nikifikiria juu ya vijana ambao walikuwa ni wanamapinduzi wakubwa pale UDSM miaka ya hii ya 2000s...

  Moja wa vijana hao ni Julius Mtatiro ambaye kwasasa anakitumikia chama cha CUF....

  Naandika haya nikijua kuwa tumepoteza potential iliyokuwa ni manufaa makubwa kwa Taifa, kaingia chama kisicho na muelekeo, majungu kama taarabu ni kawaida yao.

  Napenda kuwaomba wanaJF ambao mna ukaribu na huyu jamaa tumrudishe kundini haraka kabla ajaangamia milele...
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu mbona kashaangamia!? Aje wapi? Labda kwenu NCCR, in CDM no room ya wajingajing. Usikurupuke- kwa lipi unamlilia mtatiro? Umedandia tran kwa mbele pole!
   
 3. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kulikuwa na thread iliyozungumzia wasifu wa Mtatiro.
  Pompo alisema kasoma nae sekondari Ifakara, akiwa kiranja wa msosi na Hapo chuoni Mlimani, na anamjua in-out.
  If what he said were truth, basi Mtatiro yupo mahala panapomfaa, anaganga njaa.
   
 4. K

  KANIALE Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mungu amempatia kila mtu akili sawa. Tunachotofautiana ni ule uwezo wa kutumia karama hii ya Mungu vizuri, na uwezo wa kuchambua mambo. Mtatiro kama mtanzania yeyote yule anayo haki ya kujiunga na chama chochote kadri ya matakwa yake. Kwani kwake CUF ni chama bora. "Ubora" huu unadhihirika pale kinapounga mkono CCM na sera zake na kuzorotesha upinzani. Mwanaharakati wa Marekani, marehemu Malcolm X alisema " Faint hearts never win decisive battles." akiwa na maana kuwa mioyo laini haiwezi kupigana vita mpaka ushindi. CUF wameishia njiani tuu. Na Baba Mandela alisema hivi " When the water starts boiling it is foolish to turn off the heat."akiwa na maana kuwa maji yanapoanza kuchemka ni upumbavu kuzima moto.

  CUF wameamua kuzima moto wakati huu ambapo watanzania wengi wanadai haki, maendeleo, na hali bora ya maisha yao. Wameamua kujiunga na serikali ambayo miaka hamsini baada ya uhuru bado kuna matatizo makubwa ya umeme nchi nzima, matatizo ya maji nchi nzima, elimu, afya, miundo mbinu, ajira, ubadhilifu wa mali ya umma, rushwa, ufisadi, aaaaah orodha ni ndefu.

  Naomba wananchi msameheni Julius Mtatiro. Iko siku atagundua makosa yake na kutubu na kurudi tena kwenye harakati za kuikomboa nchi hii kutoka katika mikono ya CCM.

  Mungu ibariki Tanzania.
   
 5. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Yupo kazini!
   
 6. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  You said it Arafat
   
 7. Butho Mtenzi

  Butho Mtenzi JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mtatiro -ve potencial.Hana issue kwa sasa mwache abaki kwenye chama chake tawala Zenj na upinzani Bara
   
 8. m

  marmoboy Member

  #8
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtatiro ni kati ya viongozi wachache vijana wenye upeo mkubwa mno,
  Ana uwezo mkubwa sana wa kupambana mazingira aliyomo, mie na wenzangu 700 pale udsm tuliokuwa under private sponsorship tuliwekwa kwenye mikopo kwa sbb ya juhudi za mtatiro,
  Nakumbuka kuna siku tulikuwa naye kwa waziri mkuu-alimbana pm had kikaeleweka,
  Wakati huo alikuwa waziri wa mikopo,baadaye akawa waziri mkuu na kisha katibu mkuu wa vyuo vikuu tanzania kabla ya kujiunga cuf na kuwa mkurugenzi wa haki za binadamu na sheria na baada ya mwaka ,moja amekuwa naibu katibu mkuu wa cuf.
  Mimi namtizama kwa jicho la msimamo sana,yeye ni role model kwa mtu ambaye si mnafiki,
  Mtatiro amefika hapo alipo kwa sbb ya kutoyumbayumba,kama angehitaji fedha na umaarufu angekwenda cdm au ccm lakini kwa mrizamo wangu mtatiro ana roho ngumu,anapigania mafanikio atakayoleta na siyo ya kuletewa.
  Na sidhani eti nafasi zote alizopitia amekuwa akibahatisha au kuzipata by chance,naamini anazipata kutokana na uwezo wake na nimeona kuna mchangiaji anasema alipokuwa high skul alikuwa kiongozi then amefika mliman pana wanafunz zaidi ya 20,000 wakamuamini na baadaye kuongoza vyup vikuu,
  wakati akiongoza vyuo vikuu tukumbuke ndiyo enzi zilizokuwa na harakati za hali ya juu vyuoni,wakati tuliposhuhudia vyuo vikuu wakiandamana kushinikiza bei ya nauli na gharama za umeme zishushwe,ni wakati tuliposhuhudia maandamano kupinga uchakachuaji wa matokeo kenya na mauaji,hizi ni enzi ambazo mtatiro aliwaelekeza wanafunzi wa vyuo vikuu kupigania maslahi ya watanzania,
  Na hata leo akiwa cuf tumeshuhudia moves zake nyingi-maandamano ya kupinga kuilipa dowans kwanza yalifanywa na mtatiro na chama chake kabla cdm hawajaanza,
  Mapambano ya kupeleka rasimu ya katiba waliyoiandaa n.k.
  So, mimi naona kama hapa jamvini watu wamekaa kishabiki mno lakini ukweli unabakia kuwa mtatiro ana uwezo mkubwa sana kupita vijana wengi walioko cdm na uwezo wake utasaidia sana kuiinua cuf.
  Hongera mtatiro,hukohuko uliko tafuta ukombozi wa watz.
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0


  WABUNGE NA VYAMA VINAVYOTAMANI KUHESABIWA UMAKINI TANZANIA:

  TAFUTENI HARAKA ELIMU SAHIHI JUU YA MAANA, CHANGAMOTO NA USHIRIKI WA MAFANIKIO NDANI YA MFUMO MPYA WA 'SIASA ZA USHINDANI' ILI MUENDELEE KUMUDUU NA KUDUMU


  Ingawaje mwenye kutundika thread hii katusababishia wengi kucheka mbavu kuuma lakini baada ya kicheko ni wazi kwamba kuna mambo mengi sana ambayo watu na vyama, kama washiriki, kwa bahati mbaya hawajagundua kwamba tayari yamebadilika kabisa na kamwe hayatokaa yarudi kuwa kama zamani kisiasa nchini.

  Kweli ni masikitiko makubwa sana kwamba watu wengine hufikiria kwamba mtu unaweza tu ukaingia kwa jambo lililoitwa 'jipya' lakini bado ukatumia tu mbinu zile zile, lugha zile zile, na kashfa zile zile na bado ukaendelea tu kufanikiwa; laa hasa!! Pindi usikiapo kuna mabadiliko, kwa wale watu wadadisi wa mambo, ni sharti utafute kujua ya kwamba (1) ni kitu gani hasa kilichobadilika, (2) kivipi kimebadilika, (3) kwa sababu zipi, (4) na huko nyuma hali ilikuaje na sasa yakoje, (5) je mimi mwenyewe naendana na au siendani na mfumo huo mpya kwa kiasi gani hasa, (6) nifanye jitihada zipi (si kwenda Mlingotini) zinazokubalika ili niendane na mfumo mpya kwa namna ambavyo nitapata uhakika wa kung'ara KIUTENDAJI (si ki-ndumba) ndani na nje ya chama changu kusudi nisiwe mzigo wa chama na wapiga kura wala kulazimika kupanda BP kila wakati ...

  ... na maswali kama hayo yafanyiwekazi KIUHAKIKA NA UNYENYEKEVU zaidi wa kutafuta kule upya wa KUJIVUA GAMBA LA ZAMANI kwa wakati mwafaka na kujivisha GAMBA MPYA NA INAYOKUBALIANA NA MAZINGIRA YALIOPO na kwa mtindo utakaompendeza zaidi yule bosi na au mlaji wako wa mwisho ambaye ni MHESHIMIWA MPIGA KURA.

  Bila kufanya hivo basi niwaambieni HABARI MBAYA SANA kwamba kwa kipindi cha miaka michache ijayo, kwa tafsiri yangu ya mambo kitaaluma, bunge letu huenda ikabahatika kupata ugeni mkubwa wa Wabunge Vijana zaidi, Wasomi zaidi, na hata wakawashangaza zaidi wazee kwa kushinda kwao Uchaguzi kiurahisi zaidi bila hata kuhitaji utajiri mkubwa wa kuhonga mtu alimradi mtu huyu aje asome ninayoyaandika humu, akayafanyia HOMEWORK ya kufa mtu ndani ya miaka miwili mitatu hivi na kisha anapojitokeza ulingoni atakuta anazungumza lugha inayooana zaidi na mazingira yaliopo, akawa anazungumza na baadaye kushughulikia zaidi matatizo hasa yanaokubaliana fika na matarajio ya mabosi wake; waheshimiwa wapiga kura.

  Nirudie kwamba kwa sasa hivi ni rahisi mno kwa mtu anayejua dhana ya SIASA ZA USHINDANI unaotegemea nguvu za idadi na U-smart wa watu wanaojitokeza kugombea ukilinganisha na kuendana kwao na mahitaji halisi ya wakati uliopo wa mlaji wa mwisho wa HUDUMA ZA KIUONGOZI anazotarajia kutoa akishinda.

  Ndio nasema kwamba wapo wanasiasa wengi ambao bado huendesha mambo yao kisiasa lakini kwa kutumia fikra na mbinu za zamani katika kipindi ambacho ni tofauti kabisa. Huko nyuma siasa za fitina, majungu, kuunda zengwe, kupiga domo na kumwaga hewa tupu, kununua vyeo na wapiga kura, mtoto kurithiswa chama cha siasa cha kufuata, kurithishana uongozi na mambo kama hayo yote yalihesabiwa kuwa ndio ujanja zaidi mtu kuitwa mwanasiasa mahiri. Hii hali inaelezea hasa kwa nini Tanzania tumejitawala wenyewe karibia miaka 50 na mambo bado ni ki-mishen tauni tu toka ngazi ya kata hadi ofisi inayostahili heshima ya hali ya juu inayoitwa ikulu nchini. Ajabu kote huko kumebakia woga tu na wala si heshma kwao.

  Kwa wale ambao walau tumewahi japo hata kusikia kitu 'MFUMO WA SIASA ZA USHINDANI' napenda niseme kwamba hii ni sayari nyingine kabisa ambayo pale bungeni kwetu Dodoma, kama sikosei, zaidi ya ile dadi kubwa ya wabunge karibia 400 huenda chini ya asilimia 10% tu ndio wanaoifahamu kwamba ni kitu gani hasa hiki. Lakini kwa kuwa siku zote wanasiasa huhesabika kuwa ni watu mashuhuri kwa kujua kila kitu (MR / MS I-KNOW-ALLS) naona nafasi ni finyu sana kwa wale wengine zaidi ya 360 kuhiari walau kujishusha na kwenda kutafuta elimu juu ya hili ili uwepo wao bungeni uendelee kuwa na uhakika pamoja na tija kwa jamii kutokana na yeye mwenyewe na au chama chake kama kundi zima.

  Guys, an imagination of a possible political landscape without CUF around just but most ungratifying to witness.

  The case would never be the same as it would apply to TLPs, NCCR-Mageuzis and the UDPs of this World that has practically been consigned into political Limbo courtesy of the prominently trenched Self-Seeking behaviour, The Politics of Double-Tongue lashing and Own Course Self-Agrandisement by many in their ranks.

  Niliposema kwamba Juliasi yule wa DARUSO enzi zile wala si huyu hapa na kwamba kwa bahati mbaya mno akina Maalim Seif wamemfichia mi-faili nyeti zenye kuonyesha (1) sura halisi ya CUF, (2) Malengo ndani ya sera yao mpya ya 'Kujiunga Muafaka na Nguruwe Kuchakaza shamba Mabua yote' na hatima yake.

  Ndio, na wamemficha pia Juliasi faili iliobeba (3) tafsiri za wananchi Bara na Visiwani kama kweli walichokua wanakitafuta CUF ilikuani UTULIVU tu Zanzibar au AMANI KAMILI kwa kurejesha kwanza HAKI NA MASLAHI KWA UMMA wa nchi hii.

  Si utani na mikutano ya wenzetu inapoondoka Kidongo Chekundu pale kweupe Mnazi Mmoja hadi kule mitaa ya Mwisho wa Lami Gongolamboto, Mtoni kwa Azizi Ali Mara Manzese Kwa Bibi Mfuga Nyau ... kweli hii ni a Big Change in the Wrong Direction; yes it is a most demoralising experience and transition that bothe CUF are currently walking dow the political memory valleys kwa kupingana tu na Maslahi ya Wapigakura nchini.

  In fact, a more compelling question that analysts would soon surrender to evader no more is that 'of what use is an army commander if all foot soldiers are long-gone?' I just tend to hope that the NOW apparent CUF Career Presidential Candidates Hon Maalim Seif Sharrif Hamad (Visiwani) and Prof Ibrahim Haruna Lipumba will, at least, seek an escape to some remote hotels may be around Uluguru Mountains and conduct a most sincere Worst-Scenario Self-Evaluation.

  Yes, they would certainly need to do that long before they could similarly seek an independent expert hand to equally do the same to the very CUF as a party and ultimately hand down the CUF Secret Files stored far away in Chake Chake - Pemba to Juliasi Mtatiro and other remnant youths to help chat out a possible next course of action - either to Revive or Survive their own way and a lot sooner the better!!

  To this end, I just DON'T see myself leaving out CHADEMA for a more freequent (4-Month Periodical Independent & Credible) monitoring and evaluation about their yesterdays, todays and tomorrows. Waberoya, Mwanakijiji and myself can most competetly string them to this own-face behind the mirror scene for a more re-assuring future.

  And this is where all political parties, just like any other business establishment known around, are bound to most willingly go or never!! The market-based COMPETITIVE POLITICS that we tirelessly seek to live to-date (Democratic Multipartism) is just but more dynamic, most enveloping and so demand both at group and personal levels such that a POLITICAL HERO / HEROES of yesterday is NEVER guaranteed tomorrow unless they 24 / 7 choose to obay Philip Kotler's dictates to keep their eyes to the ground to catch the most correct scale of the electorates' next-day heartbeats and seek to serve them in the best way possible on TIME and in a WAY that a competitor (another political Party or an opponent within your party or across) would never far easily pick a match.

  In a nutshell, after luoghing of my friend Julious Mtatiro's most impending political misfortunes, like is lately the case with CCM, with his political party CUF that daily diminishing in value in the eyes of the HONOURABLE ELECTORATES, may I point here that the Political Landscape is fast-adjusting with youth on the steerwheels, things turning high-tech almost in a speed of a click of a computer mouse away such that the yerteryears inherently incompetence and majungu / fitina in political arena shall soon NEVER be tolerated BUT only practical positive results in public goods to the general public that shal be mattering and not even a mere name of a political party of the neighbours shall ever count.

  Wazee, huku ndiko tunakokwenda; hakuna watu kulala tena bungeni na kujigeuza wataalam wa kuzungusha maneno badala ya matunda kuonekana. Huko katika ulimwengu ulioendelea utasikia pengine chama chake Obama kimeshinda kwa wingi leo na keshokutwa kwenye Mid-term elections ukasikia wamepigwa chini zaidi ya nusu na Waheshimiwa Wapiga kura kwa kutoridhisha kiutendaji.

  Nasema na ieleweke kwamba ule utamaduni wa 'HIKI NI CHAMA CHANGU NA FAMILIA YETU NZIMA tangu enzi za babu hivyo sitoweza kukihama' itakuja kutoweka bila hata ya wengi wetu kujua. Hatutopigia kura tena (1) SURA za watu, (2) MAJINA YA VYAMA bali tu (3) kwa kiasi Gani Wametuletea sisi Wapiga Kura Matunda tuliokua tukiyatarajia.

  Hizo ndizo misingi halisi za siasa za ushindani huko tunakoelekea ambapo VIJANA WENGI NA WASOMI nchini ndio idadi yao inaendelea kuwa kubwa nchini. Hivyo kitendo cha Chama kubahatika kupewa ka-nafasi ya kuongoza na kisitumie vizuri KUJING'ARISHA mbele ya macho ya wapiga kura; badala yake kikajiroga kwenye kujiingiza kwenye Vitendo vya Kifisadi, basi siku kikipoteza nafasi hiyo ujue fika chama hicho kitatiwa LOCK-UP na wapiga kura kwa muda usiojulikana sawa yake KANU wa Kenya ambacho hivi leo kisiasa wala hakizungumzwi hata kwenye nafasi ya nne ki-umaarufu.

  Na atakayesoma maoni haya ampitishie na kiongozi wake wa chama chake, kata, wodi, jimbo na taifa ili tukija kuwatia LOCK-UP kwa uwezo wa kura zetu wasije wakasingizia hawakuelewa kama sheria za mchezo wa siasa za ushindani ni tofauti kiasi hicho.

  Mwisho nimalizie kwa kusema kwamba enyi mlioko madarakani ambao bado ndio mnaoonekana wakubwa kwa sisi Wapiga kura, malizieni salama utamu huo kwa vile wengi wetu hawajaeleweshwa; tangu hapo 2015 na kuendelea MPIGA KURA NDIYE ATAKAYEGEUKA MFALME kwa kipindi chote na wala si kwa wakati wa wiki 2 au 3 za uchaguzi tu.

  Chukua hatua ewe unayefikiria kuja kua kiongozi wa ngazi yoyote hapo baadaye kidogo ili usije ukafa bure na shinikizo la damu kwenye mfumo mpya wa siasa ndani ya mipaka yetu!!
   
 10. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Hapo kka umenena, CUF ni chama tu cha wapemba , cdm kina mzee makani na mwenzake mtei walikubali kuachia chama kwa vijana akina mbowe, ndesamburo aliukataa uenyekiti na akamsihi na Dr Kabouru awaachie vijana , alikataa akagombea na mbowe akashindwa vibaya akahama na chama
  All in all kama CUf inataka ionekanae ni cham cha kitaifa kinatakiwa kiutoe upemba kwanza iwe hata mtu kama mtatiro awe na say kwenye chama ns si kila kitu maalim, Lipumba ni mwenyekiti wa Cuf asiye na uamzi ni sawa na DOwans kampuni ya kufua umeme ambayo haifui umeme

   
 11. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Utamaliza machozi bure mkuu,he is lost achana nae!
   
 12. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,933
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  Sijui UDSM ipi ambayo unaisema. Kwa maana 2000's Mtatiro hayupo kabisa kwenye orodha hiyo. Kuna wanamapinduzi ambao waliokuwepo mwaka 2000/01 walikuwa hodari sana. walikuwa wanaziimba fikra za kupigania haki mpaka wanafunzi wote wanakubali bila kushurutishwa. Kwa wale waliokuwepo mwaka 2000 ambapo kampeni zilipigwa mpaka vyuo vyote nchini viligoma na kufungwa kasoro MZUMBE pekee.
   
 13. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #13
  Mar 25, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mimi naamini ni suala la muda tu mtatiro julius niliyesoma naye udsm najua iko siku atajoin wapambanaji wa kwel - chadema. Ni suala la muda tu.
   
 14. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Muulize Ziito kabwe , Alberto Msando na wengineo tuliokuwepo Ud during 2000S mtatiro was not there
   
 15. m

  marmoboy Member

  #15
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tujulishwe hayo mafaili ya siri ya cuf ili mtatiro awekwe wazi, mie namuunga mkono sana and because of that cuf.
  But muhimu tuelezwe hizo siri za cuf.
   
 16. m

  marmoboy Member

  #16
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nadhani kwa level ya perfomance ya uwaziri mkuu mlimani mtatiro ali-play big role kuliko mawaziri wakuu wengi japokuwa kila waziria likuwa na zama zake.
   
 17. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #17
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Je unamsikitia kwa lipi?

  Au ulitaka aje Chadema
   
 18. R

  Renegade JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,770
  Likes Received: 1,075
  Trophy Points: 280
  asiye na muelekeo ni wewe na si chama, huna muelekeo kwa kuwa hujui matatizo ya watanzania yametokana na nini, aidha wewe ni mbumbumbu, mshabiki au ni mtu ambaye unaangalia maslahi yako katika chama unachokishabikia na si nchi.
   
 19. m

  marmoboy Member

  #19
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtatiro mtamlilia sana na hatokuja chadema, akina zitto wanawatosha huko,
  Mtamponda sana na kumpa kila jina lakini najua kwa namna alivyo na msimamo atakuwa hana muda nanyi, mie naunga chama chochote
  Wakati wowote ule iwapo chama kina hoja.leteni hapa hoja za kuwasaidia watanzania siyo mambo ya uzushi,nenda kawalilie wajapan kwenye tsunami,mtatiro bado hajafa.
   
 20. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #20
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuchemsha kwa Mtatiro kupo wapi?kuna watu wanaangalia chama makini,wengine wanaangalia mshiko!kama Mtatiro angekuwa Cdm angekuwa na cheo hicho?alichofata cuf yeye anajua,mnaweza kufikiri amechemsha ninyi,lakini yeye ni POPOTE BORA MKONO UENDE KINYWANI!
   
Loading...