Namlilia Julius Mtatiro...

Hapa naelewa kuwa ....MTATIRO AMEKUBALI KUWA CUF NI CCM B.... Sasa wanachofanya sasa ni kutaka kuonyesha kuwa "kitendo cha wao kufunga ndoa sii tatizO kwani hata chadema nao wanajaribu kufanya hivyo"
 
Safari ya chadema Ikulu imekuwa na mtazamo wa tofauti pale baada ya kada mashuhuri kushawishika kulifikiria hilo, hakika kuishi kwingi kuona mengi ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni.
........hapa cha msingi nilichogundua ni kwamba hata Mtatiro anajua kwamba wao CUF ni CCM B;
 
wanaenda kujitongezesha tu kule ikulu, kwa vile cuf wameolewa wao wanalilia wawekwe kimada (nyumba ndogo)
 
Sipendi kuamini kama Mtatiro ana mawazo ya kijinga kama mtuma thread anavyotaka kutuaminisha. Mimi natarajia siku sinyingi Mtatiro ataachana na CUF kwasababu siyo chama kitakachokidhi matamanio ya kisiasa ya kijana kama Mtatiro. Waasisi wa CUF walianzisha chama chao kutawala Zanzibar,haya mambo mengine yalitokea sababu sheria za nchi ziliwalizimisha,lakini hawakuwa na mpango mkubwa zaidi ya huo.
 
Namsikia ndugu JULIUS MTATIRO anafanyiwa mahojiano kuhusu mwenendo wa chama chake. Akiulizwa, hatoi majibu ila povu tu. Mkali mpaka waongoza kipindi wanamuogopa.
Kafu kazi ipo.
 
Namsikia ndugu JULIUS MTATIRO anafanyiwa mahojiano kuhusu mwenendo wa chama chake. Akiulizwa, hatoi majibu ila povu tu. Mkali mpaka waongoza kipindi wanamuogopa.
Kafu kazi ipo.

Kaulizwa nini, kafokaje. weka uhondo wa ngoma.
 
Msikilizaji kahoji kama CUF ni wapinzani, kwa nini bungeni hawatoi hoja zinazosadifisha upinzani, na badala yake kinashikamana na ccm? Jamaa majibu yake ni kuwa wao wanafanya hivyo bila kuangalia wengine wanafanyaje.
Kaulizwa pia na mtangazaji kuwa muundo wa SUK kuwa ni mzigo kwa wananchi kwa ukubwa wake, yeye majibu kasema kuhoji hivyo ni kusema wananchi hawana akili (logic iko wapi?).
Akasema maamuzi ya wananchi ni THABIT na sahihi hatakama wamekosea (??) watakuja kufanya masahihisho.
 
Tunamkumbusha Mtatiro akimaliza hayo mahojiano asisahau kusema 'WABILAH TAWFIQ'
 
Nimeshangaa sana pale mdau alipopiga sim kuulizia ndoa kati ya ssm na cuf zanzibar, Mtatiro alijibu kwa confidence kuwa wao hawajaungana ila wanashirikiana, nikajawa na maswali kivpi?lakini akaendelea kudadavua kama kawaida yake na kusema wao wako ok kwani ndoa nzuri ni ile ya uaminifu, yani hutoi siri,hutoki nje, kimsingi mnaelewana kwa mabaya na mazuri, nikaguna na kuongeza sauti ya tv, akasema watu tanzania wanachojali ni maendeleo hata kama kiongozi ni dikteta haina shida cha msingi elete maendeleo nikamfikiria gadafii na ukomavu wa kisiasa wa matatiro, nikakumbuka shule zinazotolewa juu ya democrasia na chama chakesa sikujua alimaanisha nini!
 
Julius Mtatiro ondoka huko CUF unapoteza muda wako kamanda...chama kinakufa na wewe unakufa kisiasa...
 
Jamani Mtatiro ni jembe kwa tuliofanikiwa kumjua akiwa udsm ni mazao ya Prof. Shivji na prof Baregu pia kina Mwaigomole na Prof Koda wa DS Department waliwekeza kwenye hiyo kichwa tatizo nw linalima wp? Mimi ni mmoja wa watu wanaoumia sana nikimtizama mtatiro na anayoyafanya huyu alitakiwa awe mbunge wa ilala na wala c kuhangaika.
 
Amerudi kundini
Nimekuwa nikifikiria juu ya vijana ambao walikuwa ni wanamapinduzi wakubwa pale UDSM miaka ya hii ya 2000s...

Moja wa vijana hao ni Julius Mtatiro ambaye kwasasa anakitumikia chama cha CUF....

Naandika haya nikijua kuwa tumepoteza potential iliyokuwa ni manufaa makubwa kwa Taifa, kaingia chama kisicho na muelekeo, majungu kama taarabu ni kawaida yao.

Napenda kuwaomba wanaJF ambao mna ukaribu na huyu jamaa tumrudishe kundini haraka kabla ajaangamia milele...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom