Namchukia sana Mama yangu

Namchukia sana Mama yangu

Nilipiga chini mtu kisa tu aliuliza mwanangu ataishi wapi, vi vema akae kwa mama yake au bibi yake.
Nikaona hii ni kenge maji.
Yaan hongera ulijiongeza mapema,,, ungelazimisha angemtesa sana mwanao
 
WanaJF

Mimi namchukia sana mama hata nsipowasiliana nae mwaka najiona sawa.

To sum up..
Mimi nmelelewa na bibi baada ya wazazi kuachana na mama akaolewa. Hivyo mimi nikiwa mtoto wa pili na mwisho ilibidi nikaishi na mama kulingana na umri wangu.

Baba wa kambo alitamka kauli moja anahitaji kubaki na mtu mmoja kama mama anaondoka mim nibaki na kama mimi naondoka mama abaki.

Maamuzi ya mwsho yaliamuliwa niondoke nikaenda kuishi na bibi huku mzee akiwa karibu na sisi tangu darasa la kwanza hadi tunamliza chuo.

Huwa naona mtandaoni watu wakiwasifia mama zao jins wanavowapenda ila kwangu imekuwa tofauti.

Nampenda sana bibi yaani sana hata nikiwa na kidogo bora apate bibi ila sio mama..Mama namuona kama. Sina maelezo mazuri ya kuelezea ila namchukia.

Nataman nimpende kama mzazi nifanyaje

Unadhani mama yako alifanya vile kwa kupenda? mama yako ni mama yako huna mwingine.Fika mahali uachilie tuu.Unaweza usijue,inawezekana maisha uliyoyapata kwa bibi ni mama yako alikiwa anasupprt.
 
Ongea na mkeo chumbani, eleza hofu yako, eleza suluhisho kisha toa maamuzi.
Kisha mama atekeleze sehemu yake kwa kuongea na kijana bila kuleta matàtizo.
Ili eneo ndio jamaa hajatufafanulia vizuri. Je hayo maneno aliyasikia akiwa wapi? Inawezekana wazazi walikuwa wanaongelea chumbani, ila mtoto akawa anawasikiliza.
 
Hiyo ndio duniani kila mtu anajali maslahi yake ,hapo mother wako kajali ndoa yake ila baadae akizeeka atakuja kudai umsaidie wakati alienda mbio.

Kila mtu anaangalia maslahi yake kwa wakati husika hata kuvunja ndoa wazazi watapata mbadala yule atao mwingine ataolewa,kimbembe kwa watoto ndio watapata tabu ila wazazi washatuliza nafsi zao.

Ukichunguza sana wazazi ni wanafiki sana tena watu wanaozaa kwa maslahi ,wakishazeeka basi mzigo unao haijalishi walikulea au lah...Hapo sasa kila mzazi anakaa kwake utoe msaada kwa wote wewe mmoja.
 
Mimi mwanzoni nilidhani mama ndiyo Kila kitu lakini nilivyoanza kuyaona maisha na kukaa sana na Mzee na kuchanganya akili zangu za kikubwa nikagundua kuwa kumbe mama nilikuwa nampa vyeo vingi sana hivyo basi nikaamua kuwa baba na mama nawapa wote vyeo sawa, yani 50/50 wote wawili.
 
Kutokukufinya ukiwa tumboni ama uzaliwapo ni dhahiri mama yako anakupenda,nani kama mama?
 
Hakuna bond kati yenu, ndio maana unafeel hivyo.

Kwa choices alizopewa, ilikuwa ni wazi wewe ndio wakuondoka. Unaweza kumlaumu ila jaribu kumuelewa. Usikae na kinyongo, jaribu kuflash ili maisha yaendelee.
Kabisa chief,
 
Hakuna mwanaume anaekubali kulea mtoto wa mwanaume mwenzie,, mshukuru bibi amekulea makosa uliopitia kwa wazazi wako hakikisha wewe unarekebisha. Hakikisha unachagua mtu sasa utakayeweza alie tayari kuhudumia na kulea wanao.
 
Hayo ni matumizi mabaya ya chuki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom