Naomba utambue tu kuwa mama alikuwa anapita changamoto kubwa sana. Wewe unafikiria tu yeye kukaa na wewe wakati hata cha kukulisha pengine alikuwa hana.
Na kwa kuwa alikupeleka kwa bibi (Mama yake) na hapo ukapata malezi ya kawaida. Jua tu kuwa mama anakupenda sana na alikutafutia sehemu mbadala ya kukaa
Kuna hawa watoto wana achwa wawe watoto wa mtaani hao ndio habari tofauti
Kumbuka tu kuwa; Wapo wengi sana hata hapa jukwaani ambao wamelelewa na Bibi zao na wazazi wao wakiwepo....
Jua tu kuwa, Maisha yanachangamoto nyingi na ngumu sana, nafikiri ukifikisha umri wa miaka 40 hivi; utanielewa. Msamehe mama yako namtambue kama mama
Mama ni mtu pekee ambaye hata ukimnunulia sabuni ya shs 500 anakushukuru na kukuombea neema (unataka nini cha ziada?)