Wako wengi sana kama Wewe lakini wamefaulu kusamehe, it is a process, na hapo ulipofikia uko pazuri umeanza kujiuliza maswali mazuri haujaufunga moyo kutafuta majibu.
Namna nzuri ni kuvivaa viatu vyake, angalia hali yake ya umri alivyokuwa naye mpimie leo na umri vs maamuzi ya mtu wa umri wake, pima changamoto zake alizokuwa nazo, na uelewa pamoja na fursa alizokuwa nazo. Utamuelewa kwamba mwanadamu huwa ana deal na changamoto zake kulingana na uwezo upeo na wingi wa knowledge alionao kwa wakati huo.
Kwa kesi kama hiyo hiyo yako Kuna waliowapa watoto sumu wakafa, kuna waliotelekeza kwa kuwatupa au kuwaacha mahali wao wakatoweka.
Kuna waliokataa kuitwa mama wakaitwa dada.
Jambo la kumshukuru Mungu ulipata grand parents wazuri hawakukutesa, kuna walioteswa na walezi mateso na manyanyaso makubwa sana.
Msamehe mama,pateni muda wa kuongeza huwa inasaidia sana kuongeza yaliyotokea kuliko kuyazika moyoni. All the best.