Namchukia sana Mama yangu


Sema Baba wa kambo naye ni cherema(akili mgando) au ni ile sampuli ya wanaume makatili na wabinafsi.
Wale wanaume waropokaji na watumiaji.

Mwanaume aliyetimamu hawezi kuongea maneno ya hovyo mbele ya watoto hata wasio wake.

Ongea na mkeo chumbani, eleza hofu yako, eleza suluhisho kisha toa maamuzi.
Kisha mama atekeleze sehemu yake kwa kuongea na kijana bila kuleta matàtizo.
 
kumbe alikupeleka kwa bibi na bibi alikupokea vizuri.... naona bado hujakuwa huwezi kuelewa kitu...
Pia hajajua kama bibi na mamaake waliongea na wakakubaliana juu ya maisha yake, hivii anamchukiaje mama kwa kumpeleka kuishi kwa bibi!!
 
We jamaaa ni mjinga wa mwisho?

Kwa nini hukumlaumu baba yako kwa kutokuchukua?

Ukikua utaelewa huwezi elewa sasa
umri wa baba kuishi na watoto unaujua?..usiongee usilolijua
 
Yeah ni kweli.., Sometimes watoto hatutakiwi kujua hata kama wazazi wanagombanaga..
That’s why namshukuru Mungu kwajili ya wazazi wangu siku zote
 
Pia hajajua kama bibi na mamaake waliongea na wakakubaliana juu ya maisha yake, hivii anamchukiaje mama kwa kumpeleka kuishi kwa bibi!!
bibi upande wa baba unahis waliongea nn..In short bibi alichukua jukumu baada ya kuona hatuna mbele wa nyuma
 
Una childhood trauma sabbai ya tukio lililo tokea, mama aka aka ignore hilo tatizo limekuwa, umueleze why na nini kisababishi then safari ya ku heal ianzia hapo
 
Hiyo hali iliwahi kunipata nikiwa na umri kati ya miaka 14-18 hadi baba yangu alihisi kuwa nipo kwenye hali hiyo.
Licha ya kuwa yeye na mama hawakua na mawasiliano mazuri sana lakini alinieleza maneno haya "Lucha mwanangu yule ni mama yako , mama hakosei dunia hiii huwezi kumpata mama mwingine mpende sana mama yako pepo yako ipo chini ya nyayo za mama yako(kwa mujibu wa imani ya dini yetu tunaamini hivyo)"

Hiyo kauli ilinitoa machozi nilimtafuta mama yangu kwa simu nikawasiliana nae, lakini nasikitika hadi leo ule upendo wangu niliokua nao kwake kipindi nikiwa mdogo bado haujarudi kwa kiasi kile, siku moja nilimwambia mama kama una shida nieleze mimi ni mtoto wako mimi sina mama mwingine mama yangu alitoa machozi mbele yangu kwa mara ya kwanza mbele yangu.

Alhamdulillah kwa sasa ile chuki imeondoka kabisa duniani tunapitia mitihani mingi sana lakini amepata hasara yule ambae mama yake /baba yake ataondoka katika dunia hii hali yakua hana mahusiano nae mazuri Majuto huja wakati ambao huwezi kufanya nae suluhu au kuombana msamaha.

Nakusihi ndugu yangu msamehe mama yako na umpende sana maisha ni mara moja tu.
 
Dr siku hizi umekua na busara sana kuna vimaneno unaviandika navipenda.... Naomba kuja pm 😊
 
Msamehe, msamehe Mungu akutendee. Usilipe ubaya, msamehe
 
Mzazi ata akosee vip atabaki kuwa mzazi.
 
Hakuna bond kati yenu, ndio maana unafeel hivyo.

Kwa choices alizopewa, ilikuwa ni wazi wewe ndio wakuondoka. Unaweza kumlaumu ila jaribu kumuelewa. Usikae na kinyongo, jaribu kuflash ili maisha yaendelee.
Amen
 
Nimevaa viatu vyako nikajua unavyojisikia, pole sana ila bi mkubwa alizingua kinyama! Nyakati na majira vitakuponya. Vidonda vitapona yatabaki makovu na yenyewe yatapotea utasahau. Songa mbele hayo yameshapita.
 
Nimeipenda sana hii

Katika mafundisho ya kiislamu mama ana nafasi tatu ya nne ndio baba hii inaonyesha ni kiasi gani mama ana uzito mkubwa, na mafundisho yanasema ikitokea baba na mama wote wanakuita kwa wakati mmoja basi Muitikie mama kwanza

Ewe ndugu yangu hata mama yako aliumia pia alipokuacha uondoke lkn hakuwa na namna, kwahiyo ilibidi iwe hivyo,, ondoa hiyo dhana akilini mwako labda alimchagua mwanaume dhidi yako laa,,, ila ilitokea tu nawe aweze kuwa na mwenza.

Mpende mama yako kwa ajili ya Kutaka radhi za Mwenyezi Mungu

Ni swala la mda ukianza kumthamini kama mama utaona mapenzi yako kwake yanaongeza.

All the best chief
 
Pole sana kwa uliyo pitia, Mama ako sidhani kama alifanya ivo, kwa kukusudia ila naweza sema Ali fanya ivo kulinda maisha yake uhuenda alikua haoni future yake ingekuaje bila kua na mtu.

Kama umekua sasa fanya kujenga ukaribu nae kabla hujaja kujutia mama ni mama, hakuna kama mama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…