Namchukia sana Mama yangu

Mh[emoji19] niCancel kuolewa, bint zangu wasije nichukia buure[emoji19][emoji19][emoji19] lakin kijana wa Yesu naomba unishauri mimi.....@ Mtu porii unazan mmama wa miaka 32 Ni sahihi kua single forever?
 
Kiroho pia sio kitu kizuri kuweka chuki moyoni,hii inaweza kukufungia baraka zako ukashindwa kufanikiwa kwenye maisha au hata ukawa na mikosi inakuandama...
 
Wewe humchukii Mamaako.
Kama walivyosema wengine ni kwamba hauna bond na mama yako.

Hiyo sio kwako tuu bali kwa wote waliolelewa na Watu wengine nje ya wazazi wao.

Usijilazimishe kumpenda kwa sababu upendo haulazimishwi.
Ukiulazimisha upendo ndio unazalisha Chuki.
Upendo huja automatically.

Kwa upande mwingine,

Hao wazazi wako hawakuwa na sababu ya kutamka maneno hayo mbele yako kuhusu mambo achague moja wewe au mume wake(Baba wa kambo)
Hata ingekuwa ni mimi au mtu yeyote kufanywa namba mbili lazima uumie. Binadamu anapenda kusikia anapendwa kuliko kitu chochote.

Umeshakua sasa achana na mambo yaliyopita
 
Hakuna bond kati yenu, ndio maana unafeel hivyo.

Kwa choices alizopewa, ilikuwa ni wazi wewe ndio wakuondoka. Unaweza kumlaumu ila jaribu kumuelewa. Usikae na kinyongo, jaribu kuflash ili maisha yaendelee.

Sema hao wazazi nao walikuwa mazuzu.
Haikuwa na sababu mtoto kujua mambo haya.

Ilikuwa ishu rahisi sana. Waongee wenyewé huko chumbani alafu makubaliano yao mtoto ataambiwa matokeo tuu kuwa,akaishi kwa Bibi kisha watoe sababu zingine kama kuna mambo wanaweka sawa.

Kumkataa mtoto mbele mtu ambaye sio mzazi wake ni jambo baya sana.

Ni sawa na Mwanaume amkatae mzazi wake mbele ya mkewe. Unafikiri inakuwaje?

Mama alipaswa aikimbie hiyo ndoa kama hekima ilishindikana
 
Pole sana mkuu Mungu akusaidie hiyo chuki iishe ni sawa kitokua na bond nae ila kumchukia sio sawa msamehe tu.
 
Mh[emoji19] niCancel kuolewa, bint zangu wasije nichukia buure[emoji19][emoji19][emoji19] lakin kijana wa Yesu naomba unishauri mimi.....@ Mtu porii unazan mmama wa miaka 32 Ni sahihi kua single forever?
sio sahihi kuwa single forever ila waweke wao mbele kabla ya ndoa yenyewe..kuwaacha nyuma n kuwatengenezea kilichotukuta sisi
 
Umeongea kwa hekima sana mkuu
 
Of course hapo ndio shida ilipoanzia. Mleta mada hajatwambia mazingira yalikuwaje, ila kwa namna alivyoelezea ni kama vile palikuwa na kikao ambacho na yeye alishiriki (au labda alisikia mazungumzo yao).

Rejection inauma, na inaumiza sana akili. So kinachomuumiza jamaa yetu ni hiyo rejection na kukosekana kwa bond kati yao.
 
Nadhani una kinyongo cha kulelewa kwa karibu na Bibi kuliko Mama kwa uli mdogo uliokua nao.

Baba wa kambo aliogopa kupigwa matukio na Baba yako mzazi hasa ukizingatia bado alikua akiwafatilia kama ulivyosema hapo juu kwenye kuwasomesha etc
 
Umeongea kwa hekima sana mkuu

Watu watamuona mtoa mada anakosea lakini ukija kwenye suala la ukweli na haki unamkûta yuko sahihi.

Kwanza hakupaswa kujua kuwa babaake wa kambo na mama wamepeana uchaguzi mgumu kama huo. Yeye alikuwa mtoto. Walimfangia ukatili mkubwa.
Fikiria mtoto anasikia Mamaake akimkana kisa mtu mwingine.

Mama kamsaliti mtoto kisa mume(baba wa kambo)
Ndio ile mtoto wa kiume anamfukuza Mamaake kisa Mkewe. Sio pouwa hiyo. Hakuna tofauti hapo.

Lazima chuki kali iwepo.

Hayo maelezo sijui hakumtunza ni Geresha. Ila ishu ni upendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…